UKURASA WA 213; Moja Tu Sio Mbaya.

By | August 1, 2015

Unajua ni kitu gani kinachokufanya unaendelea kufanya kile ambacho umepanga kuacha kufanya? Moja tu, sio mbaya. Umeamua kwamba hutaki tena kunywa pombe, lakini unapita karibu na baa au unakutana na marafiki zako wanakunywa, na wanakuambia kunywa moja tu, sio mbaya, hutakufa na wala hutaharibu chochote. Lakini moja tu inapelekea nini??? (more…)

UKURASA WA 212; Ukipata Mimi Nakosa (Zero-Sum-Game)

By | July 31, 2015

Kwenye uchumi kuna nadharia moja inaitwa ZERO-SUM-GAME. Kwa nadharia hii ni kwamba mmoja akipata, mwingine anakosa. Kuna kipindi nadharia hii ilikuwa inaaminika na wengi na hivyo watu kuchukiana na hata kuingia kwenye matatizo makubwa. Kwa mfano watu walikuwa wanaamini kwamba ili uwe tajiri lazima wengine wawe masikini. Au kama wewe (more…)

UKURASA WA 211; Fanya Bila Ya Ajenda.

By | July 30, 2015

Tukiweka unafiki pembeni, mambo mengi tunayofanya kwenye maisha yetu tunayafanya tukiwa na ajenda fulani. Mara nyingi umekuwa unafanya kitu au kukubali kitu kwa sababu unajua matokeo yatakayotokea baada ya hapo yatakunufaisha kwa kiasi fulani. Vizuri sana kama una hisia hizi, kwa sababu umedhibitisha kwamba ni binadamu. Ila unakuwa binadamu wa (more…)

UKURASA WA 210; Kitakachotokea Baada Ya Hapa…. Na Jinsi Kinavyoharibu Maisha Yako.

By | July 29, 2015

Unajua kwa nini watu wengi hawafurahii maisha? Unajua kwa nini watu wengi wanaonekana kuweka juhudi sana kwenye kazi au biashara lakini bado wanaonekana kabisa hawayapendi maisha yao? Ni kwa sababu hawapati muda wa kuishi maisha yao. Hawapati muda wa kuwa pale walipo. Kila mara wanafikiria kitakachotokea baada ya hapa. Unakuwa (more…)

USITUMIE OPERA MINI KUSOMA MTANDAO HUU.

By | July 29, 2015

USITUMIE OPERA MINI, TUMIA BROWSER NYINGINE, AU TUMIA BROWSER MPYA KAMA ULIYOKUWA UNATUMIA INASUMBUA.   Habari za leo mpenzi msomaji. Kwanza kabisa naomba niwatake radhi wasomaji wote ambao mmekuwa mnashindwa kusoma makala kwenye mtandao huu. Inaonekana kuna tatizo kati ya mtandao huu na browser ya opera mini. Tumekazana sana kufanyia (more…)

UKURASA WA 209; Unatumia Nguvu Kubwa Kulinda Unachodhani Ni Cha Thamani Wakati Unawaachia Watu Wachezee Kilicho Cha Thamani Zaidi.

By | July 28, 2015

Kule kwetu Moshi, ukitaka kujua vizuri mtu ni nani basi kama mmepakana ongeza mpaka wako uzidi ule wa kwake. Yaani ongeza hatua moja tu kwenye mpaka wako na yeye. Atafanya kila jambo kuhakikisha anarudisha hatua ile moja uliyoongeza. Atakushitaki, mtagombana na anaweza kuapa kwamba hata akifa usifike kwenye kaburi lake. (more…)