Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

1435; Nguvu, Akili Na Muda Zaidi…

By | December 5, 2018

Watu wamekuwa wakibishana ni namna gani unapaswa kufanya kazi, na mabishano huwa yamekuwa kwenye maeneo mawili, nguvu na akili. Wapo wanaosema unapaswa kufanya kazi kwa akili zaidi na siyo nguvu zaidi. Na wapo wanaoamini kwamba kazi bora ni ile inayofanywa kwa akili zaidi na nguvu zaidi. Wale wanaosema wanatumia akili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WATAFUTE WANAOCHOCHEA MOTO…

By | December 5, 2018

“Set your life on fire. Seek those who fan your flames.” ~ Rumi Amka mwanamafanikio, Amka siyo tu kutoka kwenye usingizi, bali kutoka kwenye maisha ya kawaida, maisha ambayo hayana uelekeo na amka uweke sawa uelekeo wa maisha yako. Amka ujikumbushe malengo yako makubwa kwa kuyaandika, Na amka uipangilie siku (more…)

1434; Usianze Biashara Upya Kila Wakati…

By | December 4, 2018

Kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wengi wanalifanya ni kuanza biashara zao upya kila wakati. Kila mara wanatafuta wateja wapya kama vile hawajulikani kabisa. Tatizo hili linatokana na wafanyabiashara wengi kukosa mpango endelevu wa kibiashara. Kwao biashara ni kutafuta wateja wapya kila wakati. Hivyo wakishamhudumia mteja wanayempata, wanaachana naye na kuanza kutafuta (more…)

1433; Njia Ya Kuongeza Kipato Kwenye Ajira…

By | December 3, 2018

Watu wengi walioajiriwa huwa wana njia moja tu ya kuongeza kipato chao kupitia ajira waliyonayo. Njia hiyo ni kuomba kuongezewa mshahara. Na pale maombi yanapokataliwa, basi wanaanza kufanya kazi chini ya kiwango, kwa sababu wanaona hakuna haja ya kufanya zaidi. Njia hiyo iliyozoeleka na wengi ni njia mbovu sana na (more…)

1432; Mchezo Hatari Wa Kuepuka Kwenye Mahusiano…

By | December 2, 2018

Kujenga mahusiano bora, hasa yale ya karibu zaidi kama mahusiano ya ndoa au mahusiano ya kifamilia inahitaji kazi. Kujenga mahusiano bora siyo kitu rahisi kama wengi wanavyofikiri, siyo kitu kinachotokea tu bali ni kitu kinachofanyiwa kazi hasa. Upo mchezo mmoja hatari sana ambao wengi wamekuwa wanaufanya kwenye mahusiano. Mchezo huu (more…)

1431; Kinachoathiri Maamuzi Muhimu Unayofanya…

By | December 1, 2018

Kuna wakati unajikuta unafanya maamuzi fulani kwenye maisha yako, na huwezi kusema kwa nini umeyafanya. Unajikuta umeyafanya moja kwa moja bila hata ya kufikiri kwa kina. Yaani ni kama akili yako ilishakariri namna fulani unavyofanya mambo yako na kuendeleza hivyo. Mazingira yetu yanaathiri sana maamuzi tunayoyafanya, tukishayazoea mazingira tuliyopo, tunaanza (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WATU WASIO NA MUDA…

By | December 1, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri ambayo tumeipata leo. Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na (more…)