Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KINACHOKUSUMBUA NI KUKOSA MSIMAMO…

By | October 26, 2018

Hii ni siku nyingine mpya kwetu, Ni siku ambayo tuna nguvu ya kuitumia vile tunavyotaka. Tunaweza kuitumia siku ya leo kupiga hatua zaidi kuelekea kwenye ndoto zetu. Au tunaweza kuipoteza siku hii kwa kuwa bize na mambo ambayo hayana mchango wowote kwenye kufikia ndoto zetu. Kama utaianza siku ya leo (more…)

1394; Pima Kazi Yako Kwa Matokeo, Na Siyo Muda.

By | October 25, 2018

Kipimo bora sana unachopaswa kutumia kwa mafanikio yako, ni matokeo unayopata, na siyo nguvu wala muda, bali matokeo. Watu wengi wanapenda kutumia muda au nguvu wanazotumia kufanya kitu kama kipimo au kama njia ya kuonekana wanafanya sana. Ni rahisi kutumia njia hii, kwa sababu unaweza kuigiza kwa njia hii. Lakini (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOKIPUUZA, KITARUDI KWA NGUVU KUBWA.

By | October 25, 2018

“Whenever we give up, leave behind, and forget too much, there is always the danger that the things we have neglected will return with added force.” — Carl Jung Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda (more…)

1393; Kitu Kimoja Pekee Ambacho Watu Wote Waliofanikiwa Wanacho…

By | October 24, 2018

Siri za mafanikio na tabia za mafanikio ni maeneo ambayo yanashamiri sana zama hizi kwenye uandishi na mafunzo mbalimbali. Kwa kuwa mafanikio yana kanuni zake, fikra zetu ni kwamba kama tutafanya kile ambacho watu waliofanikiwa wamefanya, basi na sisi pia tutafanikiwa. Na hili limewafanya wengi kutafuta siri zaidi, kutaka kujua (more…)

1392; Watu Sahihi Kwako Kuwasikiliza…

By | October 23, 2018

Kwa chochote unachochagua kufanya kwenye maisha yako, watu hawatakaa kimya, kila mtu atakuwa na lake la kusema. Wapo ambao watakuunga mkono na kukupa moyo wa kuendelea kufanya. Lakini wapo ambao watakukatisha tamaa na kukuzuia usiendelee kufanya. Unapokuwa unaanza kufanya kitu, ukiwa bado hujapata uzoefu na unapokutana na changamoto, unaweza kujikuta (more…)

1391; Kadiri Unavyoshikamana Na Vitu Vingi, Ndivyo Unavyokosa Uhuru Wako…

By | October 22, 2018

Kila mmoja wetu anapenda kuwa na maisha yenye uhuru, kuweza kufanya kile anachotaka kwa wakati anaotaka. Lakini wengi pamoja na kuweza kupata uhuru wao kutoka kwa wengine, yaani kutowajibika chini ya wengine, bado wanakosa uhuru wao kutoka kwa wao wenyewe. Watu hawa wanakuwa watumwa wa nafsi zao wenyewe, na kujikuta (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KITU PEKEE UNACHORUHUSIWA KUAHIRISHA…

By | October 22, 2018

Pablo Picasso said, “Only put off until tomorrow what you are willing to die having left undone.” Siku mpya, Siku nzuri na ya kipekee sana kwetu. Ni nafasi nzuri kwetu sisi wanamafanikio kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana leo hii na hata siku zijazo. Kwa msingi (more…)

1390; Ufunguo Mkuu Wa Mafanikio Kwenye Kitu Chochote Ni Kukaa Kwenye Mchezo Kwa Muda Mrefu…

By | October 21, 2018

Kuna aina kuu mbili za mbio, kuna mbio fupi na mbio ndefu. Kwenye mbio fupi, mwenye kasi zaidi ndiye anayeshinda. Lakini kwenye mbio ndefu, anayekaa kwenye mbio muda mrefu zaidi ndiye anayeshinda. Ukiangalia mchezo wa mbio ndefu, huwa wanaanza watu wengi, lakini kadiri mbio zinavyokwenda, wengi wanaishia njiani. Mpaka kufika (more…)