Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; KUSHINDWA SIYO TUKIO, NI MCHAKATO…

By | September 11, 2018

“Failure is not a single, cataclysmic event. You don’t fail overnight. Instead, failure is a few errors in judgment, repeated every day.” —Jim Rohn Siku mpya, Siku bora, Na siku ya kipekee sana kwetu wanamafanikio kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU (more…)

BIASHARA LEO; Aina Ya Uchumi Tunaoishi Sasa…

By | September 10, 2018

Watu wengi hawajui zama zimebadilika sana, na siyo tu kwenye sayansi na teknolojia, bali pia kwenye mahusiano. Sasa hivi hatuishi tena kwenye uchumi wa ujamaa au ubepari, bali tunaishi kwenye uchumi wa kujuana na wa huduma. Tunaishi kwenye uchumi ambao watu wanaojuana wanajaliana. Watu wananunua kutoka kwa watu wanaowajua, kwa (more…)

UKURASA WA 1349; Jinsi Ya Kutumia Uvivu Kwa Manufaa…

By | September 10, 2018

Nikiwa nasoma kitabu, mwandishi alitoa kauli hii, napenda sana kulala, hivyo kitu pekee kinachokatisha usingizi wangu inabidi kiwe kinalipa fedha ya kutosha. Kwa asili sisi binadamu ni wavivu, na uvivu wetu ndiyo uliotuwezesha sisi binadamu kuweza kudumu mpaka sasa. Uvivu ni njia ya akili kutunza nguvu zetu kwa kutukatisha tamaa (more…)

#TAFAKARI YA LEO; UNACHOWEZA KUFANYA, UNAWEZA KUTOKUFANYA…

By | September 10, 2018

“What lies in our power to do, lies in our power not to do.” — Aristotle Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU (more…)

BIASHARA LEO; Punguza Hatari Kwenye Biashara Yako…

By | September 9, 2018

Warren Buffett, mwekezaji mwenye mafanikio makubwa na mmoja wa watu matajiri sana duniani, anasema ana sheria kuu mbili za uwekezaji. Sheria ya kwanza ni usipoteze fedha na sheria ya pili ni usisahau sheria ya kwanza. Tunaweza pia kutumia sheria hii kwenye biashara zetu na ikatusaidia sana. Jiwekee sheria ya kutokupoteza (more…)

UKURASA WA 1348; Uwezo Wako Mkubwa Kwenye Maeneo Mengine Pia…

By | September 9, 2018

Wengi hufikiria mafanikio makubwa ni kuchagua eneo moja na kuwa vizuri kabisa, bila ya kujali maeneo mengine wapo vizuri kiasi gani. Na hili limetengeneza watu wengi ambao wapo vizuri sana eneo moja na maeneo mengine wapo vibaya sana. Kama umewahi kusikia ile watu wanasema mafanikio siyo kila kitu, jua hapo (more…)

BIASHARA LEO; Kuuza Ni Kuwa Na Msimamo…

By | September 8, 2018

Moja ya vitu muhimu sana unavyopaswa kujua ni kwamba, kuuza ni kuwa na msimamo. Kama huna msimamo huwezi kufanikiwa kwenye mauzo. Utauza kwa kadiri utakavyokuwa na msimamo. Kwa sababu mara ya kwanza utakapowaambia watu kitu hawatachukua hatua, mara ya pili pia hawatachukua hatua, utakwenda mpaka mara ya sita, ndiyo wengi (more…)

UKURASA WA 1347; Kinachozalisha Msongo Wa Mawazo…

By | September 8, 2018

Msongo wa mawazo ni tatizo linalowasumbua wengi. Na kwa dunia ya sasa, dunia inayokwenda kwa kasi na hakuna mwenye muda, msongo wa mawazo unaongezeka kila siku na kwa wengi. Lakini upo mfumo wa maisha ambao unachochea sana msongo wa mawazo kwa wengi. Mfumo huo ni kutokuwa na taarifa sahihi juu (more…)

#TAFAKARI YA LEO; JIWEKEE UKOMO…

By | September 8, 2018

Siku mpya, Siku nzuri, Na siku tuliyokuwa tunaisubiri sana imewadia. Ni ile siku ambayo tulijiambia kesho tutafanya hivi. Kesho ndiyo imeshafika na sasa ni wajibu kwetu kwenda kufanya kile tulichojiahidi kufanya. Msingi wetu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA (more…)