Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 1353; Kiwango Cha Fedha Kinachokupa Usingizi…

By | September 14, 2018

Kama hujui fedha ya kula kesho inatoka wapi, hutapata usingizi usiku kucha, utakuwa na mawazo sana kuhusu kesho yako na maisha yataendaje.   Kama hujui mwezi utaishaje, yaani kipato kimeshaisha kabla ya malipo mengine kufika, hutapata usingizi mzuri usiku, mara zote utakuwa na mawazo maisha yako yataendaje mpaka kipato kingine (more…)

BIASHARA LEO; Kuwapa Wateja Uhakika Wa Kile Unachowauzia…

By | September 13, 2018

Mbinu zote za kuwashawishi wateja kununua zimeshatumiwa sana kiasi kwamba wateja hawajui waamini kipi kati ya vingi wanavyoambiwa na kila mfanyabiashara. Sifa zote za bidhaa au huduma ambazo watu wanauza zimeshaelezwa mpaka mteja anakuwa na wasiwasi kama kweli sifa zinazoelezwa zipo. Lakini kuna kitu kimoja ambacho kinamshawishi kila mteja na (more…)

UKURASA WA 1352; Faida Za Kuchukua Hatua Kubwa Kwenye Maisha Yako…

By | September 13, 2018

Kanuni ya mafanikio tunayoiishi kwenye KISIMA CHA MAARIFA ni MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA. Hakuna mafanikio makubwa kama hakuna hatua kubwa ambazo zinachukuliwa. Na kuchukua hatua kubwa bila ya kuwa na maarifa sahihi, ni kujiweka kwenye hali ya hatari sana. Zipo faida nyingine nzuri sana za (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USITAFUTE KOSA, TAFUTA SULUHISHO…

By | September 13, 2018

“Don’t find fault. Find a remedy.” —Henry Ford Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA (more…)

BIASHARA LEO; Cha Kufanya Pale Wengine Wanapopunguza Bei…

By | September 12, 2018

Changamoto kubwa kwenye biashara ni pale ushindani unapowekwa kwenye bei. Pale wenzako wanapopunguza bei ili kupata wateja zaidi. Ni rahisi kukimbilia na wewe kupunguza bei, lakini hiyo siyo mbinu ambayo itakuwezesha kufanikiwa kwenye biashara. Kwa sababu unapopunguza bei, unapunguza faida na kadiri faidia inavyokuwa ndogo ndivyo huduma unazotoa zinavyokuwa za (more…)

UKURASA WA 1351; Tatizo La Kuwadanganya Wengine…

By | September 12, 2018

Ni kwamba utafika mahali na wewe uanze kujidanganya mwenyewe. Ukishawadanganya sana watu, wakaamini kile unachowadanganya, utaanza kushawishika kwamba huenda unachodanganya ni ukweli na unaanza kuamini uongo wako mwenyewe. Japo ndani yako kabisa utaendelea kujua ni uongo, lakini utayajenga maisha yako kwenye uongo huo na matokeo yake hayatakuwa mazuri. Tatizo jingine (more…)

BIASHARA LEO; Mkumbuke Mteja Mmoja Leo…

By | September 11, 2018

Leo fanya zoezi hili rahisi sana kwenye biashara yako, Mkumbuke mteja mmoja ambaye amewahi kununua kwako siku za nyuma, lakini siku za karibuni hujamwona akinunua tena. Ingia kwenye mawasiliano ya wateja wako, na chukua mteja mmoja, au wachache ambao hujawaona wakinunua mara kwa mara kisha fanya nao mawasiliano. Na mawasiliano (more…)

UKURASA WA 1350; Tabia Moja Ya Uongozi Itakayokuwezesha Kufanikiwa Sana Kwenye Maisha…

By | September 11, 2018

Mwandishi Simon Sinek, ambaye anaandika na kufundisha sana kuhusu uongozi, ana kitabu kinaitwa Leaders Eat Last, akiwa na dhana kwamba viongozi wazuri huweka maslahi ya wengine mbele kabla ya maslahi yao binafsi. Na ukichukulia kwa dhana hiyo ya kula, imekuwa inaaminika kwamba viongozi ndiyo wa kwanza kula. Lakini viongozi wazuri, (more…)