Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Teknolojia Pekee Mteja Anayojali Kwenye Biashara Yako Ni Hii.

By | July 23, 2017

Kila ninapokuwa nawauliza watu nini kinawazuia kuingia kwenye biashara, majibu huwa yananishangaza mno. Watu huwa wanataja vitu ambavyo unashangaa vinawezaje kumzuia mtu asiingie kwenye biashara anayotaka kuingia. Watu wengi wamekuwa wakisubiri mpaka wawe kamili kwa kila kitu, mpaka waandae na vipeperushi vya kuwavutia wateja ndiyo waanze biashara rasmi. Lakini unajua (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UNACHOKOSA SIYO APP, BALI NIDHAMU…

By | July 23, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki yangu? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya nakubwa sana leo na kila siku. Asubuhi (more…)

UKURASA WA 935; Mapenzi Yanapotawala Maamuzi, Ndiyo Chanzo Cha Maafa…

By | July 23, 2017

Hisia na fikra huwa zinaenda kinyume, hisia zikiwa juu, fikra zinakuwa chini. Hii ndiyo sababu watu wote wanaofanya maamuzi wakiwa na hisia kali, kama za furaha au hasira, huja kujutia maamuzi yao, mara zote. Kumbuka kama hujawahi kufanya maamuzi ukiwa na hasira, lakini baada ya hasira kuisha, ukatamani usingefanya maamuzi (more…)

BIASHARA LEO; Ipe Biashara Muda, Usikimbilie Hatua Kubwa Haraka…

By | July 22, 2017

Kwa muda wote ambao nimekuwa najifunza biashara, kupitia mafunzo mbalimbali na hata kufanya biashara, nimekuwa nafananisha biashara na kitu kimoja muhimu; maisha ya mwanadamu. Nashawishika, bila ya shaka yoyote kwamba biashara ina sifa kama ya mwanadamu, kabisa. Biashara zinazaliwa, biashara zinakua, na biashara zinakufa, kama ilivyo kwa binadamu. Ili biashara (more…)

UKURASA WA 934; Tofautisha Kukosa Na Kutokutaka…

By | July 22, 2017

Akili zetu zinapenda uzembe sana, kwa sababu hazitaki kusumbuka, ndiyo maana watu wengi huwa wanatafuta njia rahisi na ya mkato ya kupata chochote wanachotaka. Unakumbuka ile hadithi ya sizitaki mbichi hizi? Kwamba sungura aliziona ndizi, akaanza kurukia, karuka mpaka kachoka, halafu mwisho akajiambia kwanza ndizi zenyewe ni mbichi, wala hata (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujafanya Maamuzi Kutokana Na Maoni Ya Watu, Fikiria Hili…

By | July 21, 2017

Unapofanya biashara, hasa kwa mazingira yetu ambayo kila mtu ni mshauri wa biashara, utapata maoni mengi sana kutoka kwa kila mtu. Hata mtoto wa shule ya msingi anaweza kukushauri ni namna gani bora ya kufanya biashara yako. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanakimbilia kufanya maamuzi makubwa ya biashara zao kwa sababu ya (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NAFASI YA KUWA BORA ZAIDI….

By | July 21, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Umeianzaje siku hii nzuri sana ya leo? Hii ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA msingi bora na muhimu sana kwetu kwenda kupata matokeo bora kabisa. Asubuhi ya leo tutafakari (more…)

UKURASA WA 933; Watu Wataendelea Kuhukumu Kitabu Kwa Ganda La Nje…

By | July 21, 2017

Japokuwa watu wanapenda kusema usihukumu kitabu kwa ganda la nje, lakini kila mtu ndiyo kitu anachofanya, katika maamuzi yake mengi kwenye maisha. Pale ambapo hatujui kitu, au hatuna uhakika nacho, basi tunatumia zaidi mwonekano wake wa nje katika kufanya maamuzi. Ni rahisi kusema huna haja ya kufanyia kazi mwonekano wa (more…)

BIASHARA LEO; Jifunze Kwenye Kila Aina Ya Biashara…

By | July 20, 2017

Moja ya kosa kubwa ambalo wafanyabiashara wengi huwa wanafanya, ni kutokujifunza kupitia biashara nyingine. Na hata kama wakijifunza, basi hujifunza kwenye biashara zinazofanana na zile ambazo tayari wanazifanya. Kwa njia hii huwa hawaji na kitu kipya, badala yake kuiga kile ambacho tayari wengine wanafanya. Njia bora kabisa ya kujifunza kwenye (more…)