Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 932; Ukimya Na Kujidhibiti…

By | July 20, 2017

Ni silaha muhimu sana kwako katika zama hizi tunazoishi. Kwa sababu zimekuwa zama ambazo kila mtu anaweza kutoa maoni yake kwenye kila jambo, kila mtu anaweza kukosoa, kila mtu anaweza kulalamika. Na ni rahisi vitu hivyo kuwafikia wengi kupitia mitandao ya kijamii. Kwa kuwa unaweza kufanya hivyo, na kwa sababu (more…)

BIASHARA LEO; Faida Siyo Kusudi La Biashara…

By | July 19, 2017

Kuna watu huwa wanaingia kwenye biashara kwa kusudi la kutengeneza faida, kupata fedha za kuendesha maisha yao, ni kitu kizuri, maisha lazima yaende na fedha ni muhimu. Lakini umuhimu wake unaenda mpaka pale mtu anapoondoka kwenye hofu ya kukosa fedha, na hapo ndipo mtu anaona kuna kitu anakosa kwenye maisha (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UNATEGEMEWA KWA LIPI?

By | July 19, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwends kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Msingo wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTEGEMEWA… Kwenye dunia, (more…)

UKURASA WA 931; Kama Tatizo Halitatuliki…

By | July 19, 2017

Huenda ni njia unayotumia ndiyo inafanya tatizo lishindikane kutatulika. Kwa sababu ni kawaida kwetu sisi binadamu kupenda kufuata njia rahisi kwenye chochote tunachofanya. Tunaangalia wapi ambapo tunaweza kuweka nguvu kidogo au gharama kidogo ili kupata kile ambacho tunataka. Lakini matatizo makubwa, yanahitaji zaidi ya kuweka nguvu na gharama kiasi. Yanahitaji (more…)

BIASHARA LEO; Epuka Kosa Hili La Muda Unapoanza Biashara Yako.

By | July 18, 2017

Kuna kosa moja kubwa sana la muda ambalo watu wengi wanaoingia kwenye biashara huwa wanalifanya. Kosa hilo ni kujikadiria muda mdogo wa biashara kuweza kusimama yenyewe na kupata faida. Watu wengi huingia kwenye biashara wakitegemea kuanza kutengeneza faida ndani ya muda mfupi tangu wanapingia. Lakini uhalisia umekuwa ni tofauti na (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; GAMING THE SYSTEM…

By | July 18, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Umeianzaje siku hii nyingine nzuri ya leo? Umejipangaje kuhakikisha kwamba siku hii inakuwa bora zaidi kwako? Je msingi muhimu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA unaufanyia kazi kila siku? Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu GAMING THE SYSTEM… Kila jambo tunalofanya kwenye maisha yetu, lipo katika (more…)

UKURASA WA 930; Dunia Haihitaji Mwongeaji Mwingine…

By | July 18, 2017

Dunia tayari ina waongeaji wa kutosha, wale ambao wanajua nini kinapaswa kufanya, wanaosema watafanya, lakini haifiki hatua wakakaa chini na kufanya au wakaonesha mfano namna gani ya kufanya. Hivyo dunia kwa sasa, haihitaji tena mwongeaji mwingine, badala yake inahitaji watu wa kufanya kitu, hata kama ni kitu kidogo kiasi gani. (more…)

BIASHARA LEO; Changamoto kubwa kwenye kupata wateja…

By | July 17, 2017

Zipo changamoto nyingi za biashara, na kwenye kupata wateja zipo changamoto pia. Lakini ipo changamoto moja kubwa ambayo wafanyabiashara wengi, huwa hawaielewi. Hasa kwa wale wafanyabiashara wanaoanza, huwa hawaelewi changamoto hii kwa sababu bado wanakuwa hawajawaua wateja wa biashara zao. Changamoto tunayokwenda kuigusia leo ni kuchagua wateja wa biashara yako. (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; KUKIMBIZANA NA FURSA….

By | July 17, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao unatuwezesha kufanya makubwa kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu kukimbizana na fursa… Wapo watu ambao (more…)

UKURASA WA 929; Unaweza Kuacha Kitu Unachokipenda?

By | July 17, 2017

Unaweza kuacha kitu unachokipenda, ambacho unaipenda kweli kutoka ndani ya moyo wako? Unaweza kukata tamaa na kuacha kufanya kitu ambacho unakipenda kweli? Ukasema hutaki tena ile furaha na hali ya kujisikia vizuri inayotokana na kile unachofanya? Majibu hapo yatakuwa ni hapana, kwa sababu kitu unachokipenda, na kukijali kweli, utakifanya bila (more…)