Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 818; Zaidi Na Zaidi…

By | March 28, 2017

Kwenye uchumi wa soko huria, unahitaji kuwa makini sana, kwa sababu unasukumwa kufanya vitu ambavyo havina faida kwako ila kwa wengine. Unalazimishwa kuona kwamba hapo ulipo hujakamilika mpaka upate kitu fulani, ambacho ni biashara ya wengine. Matangazo ya bidhaa na huduma mbalimbali yanatufanya tujione sisi bado hatuna maisha mazuri na (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MATOKEO GANI UNATARAJIA?

By | March 27, 2017

Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Hii ni fursa ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa. Tutumie muda wetu wa leo ili tuweze kufanya makubwa. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambazo ndiyo nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Asubuhi ya leo (more…)

UKURASA WA 817; Usimpe Mteja Majukumu Ambayo Siyo Yake….

By | March 27, 2017

Watu wengi wamekuwa wanafanya biashara kwa starehe sana, yaani kuna majukumu yao ambayo hawataki kuyafanya wao, bali wanataka wateja ndiyo wafanye majukumu hayo. Halafu ukiangalia majukumu hayo ni madogo sana, lakini hawayaelewi na hivyo kuwapotezea wateja. Siku moja nilikuwa napita mahali, nikaona pamewekwa tangazo tunauza mayai. Nikasimamisha gari na kwenda (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; TAKE ACTION OR MOVE ON.

By | March 26, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii ya kipekee sana ya leo. Ni siku ambayo hutaiona tena kwenye maisha yako, ni leo tu hivyo ni muhimu uitumie vizuri siku hii. Tukumbuke msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambao unatuwezesha kufanya makubwa kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu ku TAKE (more…)

UKURASA WA 816; Salama Ni Hatari Zaidi…

By | March 26, 2017

Ninachoendelea kujifunza kwenye haya maisha ni kwamba, unahitaji maarifa sana kuweza kufanikiwa kwenye haya maisha. Na baada ya maarifa unahitaji ujasiri wa hali ya juu sana ili kuweza kufika pale unapotaka kufika. Kwa kukosa vitu hivi viwili, utaishia kuwa ndani ya kundi, kundi ambalo halitaki maarifa wala halihitaji ujasiri, kwa (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; KITUMIE VIZURI WAKATI KIPO.

By | March 25, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo utaweza kufanya makubwa sana. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUTUMIA VIZURI WAKATI KIPO. Chochote ulichonacho sasa, kuna siku (more…)

UKURASA WA 815; Uangalie Ukweli…

By | March 25, 2017

Moja ya sababu kubwa zinazowazuia watu kufanikiwa, ni kukataa kuuangalia ukweli. Kwa kuwa ukweli haupo vile wanavyotaka wao, basi wanachofanya ni kutokuuangalia, bali wanaangalia kile kinachowafurahisha kwa wakati husika. Ukweli ni kwamba maisha ni magumu, na haijalishi wewe ni nani na unaanzia wapi, kila mtu ana magumu yake kwenye maisha, (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; FANYA ZAIDI…

By | March 24, 2017

Ni siku nyingine nzuri sana ya leo rafiki, Siku ambayo jana uliita keshom na kujiambia yapo mambo ambayo ungeyafanya leo hii. Nakukumbusha tu kesho uliyoisema ndiyo leo na hivyo hakikisha unafanya ulichosema, usije kuahirisha tena leo. Leo nenda kaweke juhudi kubwa ili uweze kupata matokeo makubwa. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU (more…)

UKURASA WA 814; Wamekijua Leo, Walikitaka Jana…

By | March 24, 2017

Mabadiliko makubwa yanayoendelea duniani, hasa enzi hizi za ukuaji wa sayansi na teknolojia, yanagusa kila kona ya maisha yetu. Sehemu inayoguswa zaidi na ambayo wengi hawaioni vizuri ni kwenye biashara. Njia za ufanyaji wa biashara zimebadilika sana. Kuanzia kutangaza biashara, kuwafikia wateja na hata mahitaji yenyewe ya wateja. Kabla ya (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NO GUARANTEE….

By | March 23, 2017

Hongera rafiki kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunaweza kufanya makubwa. Asubuhi ya leo tunatafakari kuhusu NO GUARANTEE. Tunapokwenda kununua vitu, tunapenda sana vile vitu ambavyo (more…)