Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 450; Sababu Mbili Za Kuweka Juhudi.

By | March 25, 2016

Mpaka sasa nina hakika unajua hili, ya kwamba ili kuweza kufikia mafanikio makubwa, unahitaji kuweka juhudi kubwa sana, yaani sana. Kama wenzako wanafanya kwa kawaida, wewe unahitaji kwenda mbali zaidi. Na kama mpaka sasa hukubaliani na hilo, usiendelee kusoma. Sasa kuna sababu mbili za kuweka juhudi kubwa sana. Sababu ya (more…)

UKURASA WA 449; Makosa Ya Wengine.

By | March 24, 2016

Makosa ya wengine ni kitu cha kipekee sana kwetu, Makosa ya wengine yanaonekana haraka sana, kuliko hata makosa yetu. Makosa ya wengine yanatupa vitu vya kujadili na kukosoa. Makosa ya wengine yanatupa ahueni kwamba angalau sisi tuko vizuri, kuliko hao wenye makosa hayo. Makosa ya wengine tunaweza kuamua kuyatumia tutakavyo, (more…)

BIASHARA LEO; Kitu Kimoja Unachoweza Kumpoteza Nacho Mshindani Wako Wa Biashara.

By | March 23, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nakuambia mara nyingi, kwenye biashara usiingie kwenye mashindano ya moja kwa moja na washindani wako, maana hii itakuumiza zaidi ya kukujenga. Unapoingia kwenye mashindano ya moja kwa moja, mshindani wako anaweza kufanya jambo lolote ambalo linaweza kuwaathiri wote wawili kwenye biashara zenu. Lakini pia nimekuwa nakushirikisha mbinu (more…)

UKURASA WA 448; Kejeli…

By | March 23, 2016

Watu huwa wanakejeli vitu ambavyo wanavihofia au ambavyo wao wenyewe hawawezi kuvifanya. Na hivyo wanapomwona mtu mwingine anafanya, inawaumiza na ili kujiondolea maumivu hayo wanakejeli. Wanatengeneza hadithi zao ambazo zitawafanya wao wawe sahihi kuliko yule ambaye amechagua kufanya kitu cha tofauti. Na watakuwa na maneno mengi ya kejeli. Vitu viwili (more…)

ONGEA NA COACH; Ni Nani Huyo Alikudanganya?

By | March 22, 2016

Habari za leo rafiki? Naamini uko vizuri sana, mimi pia niko vizuri sana na naendelea kuweka juhudi kuhakikisha maisha yangu na yako wewe rafiki yangu yanaendelea kuwa bora sana. Nina hakika na kwa upande wako unaendelea kuweka juhudi, hongera sana kwa hilo. Leo katika mazungumzo yetu haya nataka kugusia swala (more…)

UKURASA WA 447; Pamoja Na Hofu Zote….

By | March 22, 2016

Pamoja na hofu zote ulizokuwa nazo siku za nyuma kuhusu siku za sasa, nyingi hazijatokea. Na hata kama zimetokea mambo hayakuwa mabaya kama ulivyokuwa unafikiria. Nina hakika na hili kwa sababu bado upo na bado unaendelea kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi. Umekuwa ukihofia ya kwamba mambo yatakwenda vibaya, na (more…)

Mambo muhimu kuzingatia ukishapata mkopo wa biashara.

By | March 21, 2016

Moja ya njia za kupata au kuongeza mtaji wa biashara yako ni kuomba mkopo. Na siyo kila mtu anaweza kupata mkopo, hivyo unapokuwa na sifa za kupata mkopo, na ukapata mkopo unaohitaji ni jambo zuri kwa biashara yako. Lakini kama ambavyo unajua, au kama hujui unahitaji kujua leo, mkopo ni (more…)

UKURASA WA 446; Sehemu Isiyohitaji Usawa.

By | March 21, 2016

Kwenye maeneo mengi ya maisha yetu tunahitaji usawa, kwa sababu binadamu wote ni sawa, hivyo kila mtu anastahili kupata huduma sawa, hii ni kweli kabisa. Lakini kuna maeneo kwenye maisha yako ambayo huhitaji kabisa usawa na mtu mwingine yeyote. Yaani kwenye maeneo hayo ukikubali usawa tu umejipoteza mwenyewe. Kwa mfano (more…)