Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Zingatia haya unapopeleka biashara yako sehemu mpya.

By | February 22, 2016

Pale biashara yako inapokua, unaanza kuona fursa nyingi zaidi za kukuza biashara hiyo. Haya ndiyo madhara mazuri ya kuendesha biashara yako kitaalamu. Na unapofika wakati wa kuikuza zaidi biashara yako, kufungua matawi sehemu mpya ni moja ya sehemu za ukuaji wa biashara yako. pamoja na kufanikiwa sana kwa biashara kwenye (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mtu Pekee Unayeweza Kumpa Furaha Kwenye Maisha Ni Huyu Hapa.

By | February 21, 2016

Karibu mwanafalsafa mwenzangu kwenye siku hii nyingine ambapo tunakutana pamoja katika kujenga falsafa bora sana itakayoongoza maisha yetu. Kupitia falsafa hii mpya tunapata mwongozo wa maisha bora, yenye furaha na mafanikio makubwa sana. Leo katika falsafa tutachimba ndani kuhusu furaha ya kweli kwenye maisha. Kumekuwa na upotoshaji mkubwa sana kwenye (more…)

UKURASA WA 417; Jinsi Ya Kujua Kitu Ambacho Sio Muhimu Kwako.

By | February 21, 2016

Kuna vitu vingi sana ambavyo huwa tunakuwa tunataka kufanya. Ila kwa sababu nguvu zetu na muda havitoshi, basi tumetengeneza njia nzuri sana ya kuweka pembeni vile ambavyo sio muhimu na kufanya vile ambavyo ni muhimu. Ila njia hii huwa hatuijui kwa sababu huwa inafanyika kwa mazoea. Na kwa njia hii (more…)

UKURASA WA 416; Sio Vyote Vitaenda Kama Utakavyo.

By | February 20, 2016

Lengo la kuweka malengo siyo uyafikie yote kwa asilimia 100. Lengo la kuweka mipango ya siku siyo kuikamilisha kwa silimia 100. Japo kuna wakati unaweza kufikia vyote kwa asilimia 100, lakini sio mara zote unaweza kufikia hivyo. Siyo vitu vyote vitaenda kama unavyotaka wewe. Sio kila kitu kitatokea kama ulivyotegemea. (more…)

BIASHARA LEO; Wewe Ndiye Unayeijua Biashara Yako Na Siyo Mteja, Timiza Wajibu Huu.

By | February 19, 2016

Kuna wakati ambapo wafanyabiashara huwa tunajisahau sana. Tunapitiwa kwa kufikiri kwa kuwa sisi tunaijua biashara yetu basi mteja naye anajua. Au tunafikiri kwa sababu tumeshaeleza kwa wateja basi ni jukumu la kila mteja kujua. Ni jukumu lako wewe kumweleza kila mteja kuhusu biashara yako, na sio wote watakaokuelewa. Hivyo kuwa (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; The Truth About Innovation (Ukweli Kuhusu Uvumbuzi).

By | February 19, 2016

Tunaishi kwenye dunia ambayo mabadiliko yanatokea kwa kasi kuliko kipindi chochote kuwahi kutokea. Ukiangalia tangu zama za mawe, ilichukua muda mrefu sana kufikia zama za chuma, na baadaye mapinduzi ya viwanda. Lakini tangu tumeingia kwenye zama hizi za taarifa, kugunduliwa kwa mtandao wa intaneti kumeleta mabadiliko makubwa na ya haraka (more…)

UKURASA WA 415; HISIA…

By | February 19, 2016

Katika matatizo yote unayopitia kwenye maisha yako, naweza kusema asilimia 90 yanasababishwa na hisia. Hisia sio nzuri kabisa kwenye ufanyaji wa maamuzi. Hisia na kufikiri haviwezi kwenda pamoja. Unapokuwa na hisia kali kufikiri kunakuwa chini sana. Na unapoweza kuzishusha hisia zako chini, ndio unaweza kufikiri sawasawa. Hisia ndio zimekuwa zinatufanya (more…)

Nazifunga Tena Makala Zote, Na Ombi Muhimu Kwako Wewe Rafiki Yangu.

By | February 18, 2016

Habari za wakati huu rafiki? Naamini unaendelea vizuri na kuyafanya maisha yako kuwa bora kila siku. Hii ndiyo habari ninayotaka kuisikia kutoka kwako kwa sababu dhumuni langu kwenye maisha ni kuwa sehemu ya mabadiliko chanya kwenye maisha ya wengine. Kupitia chochote ninachofanya, napenda kuona maisha ya wengine yakibadilika na kuwa (more…)

UKURASA WA 414; Vitu Viwili Ambavyo Vimekuwa Adimu Sana Kwenye Dunia Ya Sasa, Na Ukiwa Navyo Ni Mtaji Mkubwa.

By | February 18, 2016

Dunia inabadilika kwa kasi sana, kadiri siku zinavyokwenda vitu na watu wanabadilika sana. Na mabadiliko haya yanakuja na mambo mazuri na mambo mabaya pia. Kuna vitu viwili muhimu sana ambavyo vimekuwa adimu sana kwenye dunia ya sasa. Vitu hivi vina thamani kubwa sana na ni mtaji wa kukuwezesha kupata chochote (more…)

BIASHARA LEO; Usiwe Nafuu Kuliko Wote.

By | February 17, 2016

Linapokuja swala la kuongeza mauzo na kukuza biashara, wafanyabiashara wengi huangalia eneo moja rahisi, kupunguza bei, au kuuza bei rahisi kuliko wengine. Hii inaweza kuonekana kufanya kazi kwa muda lakini baadaye itakuumiza, hasa kama utakuwa ndio bei nafuu kuliko wengine wote. Kama lengo lako ni kutengeneza biashara itakayokua na kudumu (more…)