Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 413; Ukweli Unaonekana Vizuri Kuliko Unavyosikika…

By | February 17, 2016

Kama kuna kitu ambacho unaamini ni kweli, na una uhakika kabisa ni kweli, lakini watu wengine hawakubali wala kuamini kwamba ni kweli, una njia mbili za kuwafanya wakubali na kuamini. Njia ya kwanza ni kuwafanya wasikie, yaani kuwaambia. Na kwa sababu ukiwaambia watakubishia, basi utahitaji kubishana, na katika kubishana utahitaji (more…)

BIASHARA LEO; Mbinu Kumi Anazoweza Kutumia Mfanyabiashara Mchanga Kuongeza Mauzo.

By | February 16, 2016

Uhai wa biashara ni sawa na uhai wa binadamu. Ili mtu uendelee kuwa hai ni lazima mzunguko wa damu uwe sawa. Na ili biashara iendelee kuwa hai ni lazima mzunguko wa fedha uwe sawa. Mzunguko wa fedha ndiyo damu ya biashara yoyote ile. Mzunguko wa fedha kwenye biashara unaanzia kwenye (more…)

ONGEA NA KOCHA; Kila Kitu Ni Kibovu, Inategemea Uko Upande Upi.

By | February 16, 2016

Habari za leo rafiki? Naamini uko vizuri na unaendelea kuweka juhudi kwenye kile ulichochagua kufanya kwenye maisha yako, maana hakuna namna nyingine bali kuweka juhudi na maarifa huku ukijijengea nidhamu ya hali ya juu. Kwa njia hii hakuna chochote ambacho kitakushinda. Leo katika mazungumzo yangu mimi na wewe nataka tuguse (more…)

UKURASA WA 412; Mpaka Waache Kukupuuza…

By | February 16, 2016

Unapoanza kufanya kitu chochote kipya, na ukajitoa kukifanya kwa ubora wa tofauti kabisa, watu wataanza kwa kukusifia, lakini baada ya muda mfupi wataanza kukupuuza, yaani kutojali sana kile unachofanya. Na pengine watakuambia una wazo zuri lakini kwa hapa haliwezekani, au kuna wengine walianza kama wewe lakini walishindwa. Au unachojaribu kufanya (more…)

BIASHARA LEO; Usimpe Mteja Anachotaka, Mpe Hiki.

By | February 15, 2016

Kwanza kabisa, kabla hatujachanganyana, unapoanza biashara, anza na biashara ambayo wateja wako tayari kununua. Hivyo ni lazima ujue matatizo ambayo watu wanayo na uje na suluhisho. Sasa pamoja na kuwa na kitu ambacho watu wanataka, bado usimpe mteja kile ambacho anataka yeye, bali mpe kile ambacho ni bora zaidi. Mteja (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; Simply Parenting (Malezi Bora Ya Watoto).

By | February 15, 2016

Linapokuja swala la malezi bora ya watoto, kila mzazi anakuwa njia panda kwa sababu hakuna mtaala maalumu unaotolewa wa kuwaandaa watu kutoa malezi bora. Kama hiyo haitoshi, watoto pia hawaji na kitabu cha maelekezo kama ambavyo ukinunua kitu kipya unapewa. Na kufanya mambo kuwa magumu zaidi, watoto wanatofautiana na hivyo (more…)

UKURASA WA 411; Haitaondoka Yenyewe…

By | February 15, 2016

Tukiangalia kwa undani kabisa, kama utaamua kuweka sababu nyingine zote pembeni ni kwamba kuna kitu kimoja tu kinachokuzuia wewe kuishi yale maisha ambayo unajua unataka kuishi. Nina uhakika una picha fulani ya maisha ambayo unajua ni bora kwako. Unaona kabisa kama maisha yako yangekuwa hivi basi mambo yangekuwa mazuri. Na (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Umuhimu Wa Ukuaji Wa Kiroho.

By | February 14, 2016

Kama kuna eneo muhimu kwenye maisha yetu, ambalo limesahaulika sana ni ukuaji wa kiroho. Tunajali kuhusu afya zetu za mwili, na kujali kiasi kuhusu afya za akili, lakini tunasahau kuhusu afya ya kiroho. Kila mmoja wetu ana maisha yake ya kiroho, bila ya kujali dini aliyonayo, kabila analotokea au nafasi (more…)

UKURASA WA 410; Unachotaka Kuficha Ndicho Wanachotaka Kuona…

By | February 14, 2016

Kile kitu unachotaka kuficha, ndicho ambacho dunia inataka kuona. Na hii ni kwenye kazi, biashara na hata maisha. Kuna vitu vingi ambavyo unajua unataka kufanya, lakini kwa sababu vitu hivyo ni vipya na hujawahi kufanya tena, unakuwa na hofu kubwa. Kwa kuwa na hofu hii unalazimika kuficha kile ambacho ulitaka (more…)

UKURASA WA 409; Ukishaingia Kwenye Matatizo, Tulia.

By | February 13, 2016

Changamoto, vikwazo na matatizo ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. Hakuna maisha yaliyonyooka tu, ambayo hayakutani na vitu hivyo. Kuna kitu kimoja ambacho kimekuwa kinawapata watu wanaoingia kwenye matatizo. Tatizo moja ni kama linazaa matatizo mengi zaidi. Yaani mtu anaanza na tatizo moja na hatimaye anajikuta kwenye matatizo (more…)