Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 314; Umegoma Kuishi….

By | November 10, 2015

Kwa hali ilivyo hakuna namna nyingine ya kulisema hili bali kusema kwamba umegoma kuishi. Unapokazana kufanya mambo ambayo hayaendani kabisa na maisha, iwe unajua au hujui ni kwamba umegoma kuishi. Unapokazana kusema kwamba maisha hayako sawa, maana yake umegoma kuishi, kwa sababu nani alikuahidi kuwa yatakuwa sawa? Unapolalamika au kulaumu (more…)

Mbinu bora za kupata wafanyakazi sahihi wa biashara yako.

By | November 9, 2015

Ili biashara yako iweze kukua na kukuletea mafanikio makubwa, unahitaji watu makini sana wa kukusaidia kwenye biashara yako. na ili uweze kupata watu hawa makini ni lazima wewe mwenyewe uwe makini kwenye kuajiri. Wafanyabiashara wengi wamekuwa na malengo mazuri sana na biashara zao na wamekuwa wakijitoa sana ili biashara zao (more…)

UKURASA WA 313; Ni Leo Tu…..

By | November 9, 2015

Watu wengi wana malengo na mipango mizuri sana. Lakini sio wote wanaofikia malengo na mipango hii. Subiri, sio wote ambao hata wanaanza kuifanyia kazi. Kuna wengi wanaoishia kwenye hatua hii ya kupanga tu, lakini inapofikia utekelezaji wanasogeza mbele, nitafanya kesho, au nikiwa tayari, au kitu fulani kikiisha. Tabia ya kuahirisha (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kuwa Na Maisha Bora, Nenda Kinyume na Tabia Za Asili Za Binadamu.

By | November 8, 2015

Habari za leo mwanafalsafa? Karibu tena kwenye kipengele hiki cha FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo tunashirikishana maarifa muhimu ya kuweza kujenga maisha bora sana kwetu. Kama ambavyo wote tunajua, maisha tuliyonayo hapa duniani ni haya tu. Hatutarudi kuja kuishi tena baada ya kuondoka hapa duniani. Hivyo ni jukumu la kila (more…)

UKURASA WA 312; Giza Sio Kitu…. Hofu Sio Kitu…..

By | November 8, 2015

Giza sio kitu, bali ni ukosefu wa kitu. Giza sio kitu kwa sababu huwezi kulifanyia chochote, huwezi kulifanyia vipimo vya kitaalamu, ni giza tu basi huwezi kwenda zaidi. Giza sio kitu bali ukosefu wa mwanga, mwanga unapokuja, giza linaondoka, wala hakuna ushindani wowote, mwanga ukiwepo hakuna giza. Mwanga ni kitu, (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU THE TIME WARRIOR(SHUJAA WA MUDA).

By | November 7, 2015

Kitabu THE TIME WARRIOR ni kitabu ambacho kinatufundisha mbinu mbalimbali za kuweza kuwa na matumizi mazuri ya muda ili kuweza kukamilisha malengo na mipango yetu muhimu kwenye maisha. Kitabu hiki kinatoa njia za kuondokana na hali ya kuahirisha mambo, kutaka kuwaridhisha watu, kujishuku wewe mwenyewe, kujiwekea majukumu mengi na pia (more…)

UKURASA WA 311; Kusema Na Kufanya.

By | November 7, 2015

Wote tunajua kusema ni rahisi kuliko kufanya, hiyo sio habari. Habari ni hii, kuna watu wanasema na wanafanya, ila changamoto inaanzia hapa, wanachosema wanafanya sio kile wanachokwenda kufanya. Wanasema hiki na wanafanya kingine. Kwa kuanzia fikiri kila mtu anakwenda kufanya tofauti na kile anachosema atafanya, halafu angalia ni jinsi gani (more…)

UKURASA WA 310; Leo Tumalize Vitu….

By | November 6, 2015

Hakuna kitu kinakunyonya nguvu kama ambacho umefanya na kuishia njiani. Mawazo yako yanabaki kwenye kitu kile na hivyo kushindwa kusonga mbele zaidi. Kila utakapofikiria kufanya kitu kipya unajikumbusha kwamba kuna kitu hujamaliza. Na unapokuwa unafanya kitu halafu ukaishia kati kati, ni vigumu sana kuja kuanza tena, kuja kuanza tena kunaonekana (more…)

Maneno Mazuri Ya Ushindi Kutoka Kwa Rafiki Yetu.

By | November 5, 2015

Habari za leo rafiki? Nina imani unaendelea vyema sana na kufanyia kazi malengo na mipango yako. hongera sana kwa hilo na nikukaribishe kwenye mazungumzo yetu ya siku hii nzuri ya leo. Kwenye mazungumzo yetu ya leo mimi nitakaa pembeni kidogo na kwa pamoja tutamsikiliza na kujifunza kutoka kwa rafiki yetu (more…)

UKURASA WA 309; Kama Usingeacha….

By | November 5, 2015

Kuna matatizo makubwa mawili pale linapokuja swala la kuchukua hatua ili kuweza kufikia malengo na mipango yako. wengi huwa wanafikiri tatizo ni moja tu na hivyo wanapolivuka wanakuwa hawajajiandaa na tatizo lingine ambalo ni kubwa zaidi. Tatizo la kwanza ni KUANZA. Ndio watu wengi wana malengo na mipango mizuri sana. (more…)