Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 295; Ndio Tumezoea Kufanya Hivi….

By | October 22, 2015

Sehemu kubwa ya maisha yetu inaendeshwa na tabia, ambazo tumejijengea kwa muda mrefu. Tabia zinatusaidia tuweze kuweka mawazo yetu kwenye yale mambo ambayo ni muhimu zaidi. Kwa mfano kila siku unapiga mswaki, lakini sio kwamba kila siku utakuwa kama ndio unaanza. Ukishachukua tu mswaki basi mengine yanafuata kama ulivyozoea. Tabia (more…)

UKURASA WA 294; Unachotaka Kwako, Taka Na Kwa Wengine.

By | October 21, 2015

Dunia sio mapambano ya kupata au kukosa. Sio kweli kwamba kuna uhaba kama tunavyoaminishwa. Sio kweli kwamba ili wewe uwe tajiri ni lazima wengine wawe masikini. Chochote unachotaka, kipo cha kukutosha wewe na wengine wengi wanaokitaka pia. Unapoiruhusu akili yako kuwafikiria wengine pia, unairuhusu kufikiri kwa ukubwa zaidi, unaimarisha ushirikiano (more…)

UKURASA WA 293; Maisha Ya Mashaka…

By | October 20, 2015

Ngoja nikuambie kitu, maisha ni mazuri sana. Ila maisha yanakuwa mazuri kama utayaishi kwa viwango vyako mwenyewe. Kama utaamua kuishi maisha yako kwa viwango vya wengine, maisha yako yanakuwa ya hovyo na yanakuwa maisha ya mashaka. Njia moja ambayo wengi wanatumia kuishi maisha yao kwa viwango vya wengine ni kujilinganisha (more…)

Kwa nini mchanganuo wa biashara yako ni muhimu sana kwako.

By | October 19, 2015

Wafanyabiashara wengi huwa hawaandai michanganuo ya biashara yao kwa matumizi yao wenyewe. Wengi hulazimika kuandaa michanganuo pale ambapo wanahitajika kufanya hivyo na taasisi mbalimbali. Labda mfanyabiashara anataka kuchukua mkopo na moja ya vigezo na masharti ya mkopo ni kuwasilisha mchanganuo wa biashara na jinsi mkopo huo utakavyotumika. Wafanyabiashara wengi huandaa (more…)

UKURASA WA 292; Mpango Wa Mabadiliko….

By | October 19, 2015

Tunapenda sana mabadiliko kwenye maisha yetu, lakini hakuna viumbe wagumu kubadili kama sisi wenyewe. Ni rahisi sana kuona wengine ndio wanahitaji kubadilika. Ni rahisi sana kuongea kuhusu mabadiliko. Ni rahisi sana kulalamika na kulaumu pale unapoona mambo hayaendi sawa. Lakini inapofika kwamba unahitaji kubadilika, hapo ndipo ugumu unapoanzia. Sasa sikiliza, (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Hii Hapa Ni Njia Iliyo Wazi Kabisa Kwako Kufikia Mafanikio Makubwa.

By | October 18, 2015

Tunaendelea kuongeza misingi kwenye falsafa yetu hii mpya ya maisha. Kumbuka kila mara kufuata misingi hii. Usiache hata siku moja kufuata misingi. Misingi hii tunayoiweka kwenye falsafa yetu mpya ya maisha ni misingi ambayo imedhibitishwa kuleta matokeo mazuri kwenye maisha. Ni misingi ambayo imetumiwa enzi na enzi na imekuwa inaleta (more…)

UKURASA WA 291; Maisha Ni Maigizo, Je Wewe Unaigiza Nini?

By | October 18, 2015

Maisha ni maigizo. Ukienda kwenye msiba, hata kama mtu sio wa karibu kwako, ni lazima utakuwa na huzuni. Hata kama una furaha kiasi gani siku hiyo, utaiweka furaha yako pembeni na kuvaa uhusika wa msiba, ukitoka hapo unaweza kurudi kwenye furaha yako. kama haya sio maigizo ni nini? Hata kama (more…)

UKURASA WA 290; Uwe Unapenda Kweli, Iwe Inatoka Moyoni.

By | October 17, 2015

Kama unavyojua mpaka sasa, mafanikio hayatakuja kwa wewe kufanya vitu vya kawaida na kwa njia za kawaida. Mafanikio yatakuja kwa wewe kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Kwa kifupi ni kufanya kazi sana, sio kidogo. Na lazima uwe tayari kwenda hatua ya ziada, kwenda zaidi ya wengine walivyozoea kwenda, kutoa (more…)

UKURASA WA 289; Vaa Viatu Vya Wengine…

By | October 16, 2015

Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho, ni kwamba kila mtu mzima na mwenye akili timamu anataka kuwa na maisha bora zaidi ya aliyonayo sasa. au kama aliyonayo sasa ni bora, basi yaendelee kuwa hivyo. Lakini katika kufikia maisha haya bora, ndio kunakuja changamoto nyingi sana kwenye dunia yetu. Kuna ambao (more…)

Hiki Ni Kitu Kimoja Nakuhakikishia Utakutana Nacho Mara Kwa Mara.

By | October 15, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Naamini uko vizuri sana, mimi pia nipo vizuri. Karibu tena leo kwenye mazungumzo yetu haya muhimu, ambapo mimi na wewe tunazungumza kama marafiki. Leo nataka nikuambie kitu kimoja ambacho nakuhakikishia utakutana nacho mara kwa mara. Na siku utakayoacha kukutana nacho, ni siku utakapoondoka kwenye dunia (more…)