Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

MABORESHO ZAIDI KWENYE KISIMA CHA MAARIFA KUANZIA NOVEMBER 2015.

By | October 29, 2015

Kuanzia mwezi november mwaka huu 2015 kutafanyika maboresho zaidi kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Maboresho haya ni kuhakikisha wewe unapata maarifa bora zaidi yatakayokuwezesha wewe kuchukua hatua ya kuboresha kazi zako, biashara zako na hata maisha yako kwa ujumla. Kumbuka maarifa ni muhimu sana kwako kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwenye (more…)

UKURASA WA 302; Kushindwa Kunapatikana Sehemu Moja Tu, Na Kwa Bahati Nzuri Haupo Sehemu Hiyo.

By | October 29, 2015

Kuna sehemu moja tu ambayo kushindwa kunapatikana na sehemu hiyo ni kaburini. Ndiyo ni kaburini pekee ambapo kushindwa ndio kunapatikana. Kwa sababu unasoma hapa, naamini hujafika kaburini na hivyo hii ni habari njema kwamba bado hujashindwa. Mtu pekee ambaye tayari ameshashindwa ni yule ambaye ameshakufa, maana huyu hana njia yoyote (more…)

UKURASA WA 301; Dunia Mbili Unazoishi….

By | October 28, 2015

Katika wakati wowote kwenye maisha yako unaishi kwenye dunia hizi mbili, Dunia ya kwanza ni ile inayotengenezwa na maisha yako ya kazi. Hii inatokana na kile unachofanya ili kutengeneza kipato chako cha kuendesha maisha. Inaweza kuwa kuajiriwa, kujiajiri au kufanya biashara. Dunia ya pili ni ile unayotengenezwa na maisha yako (more…)

Watu wanakua, watu wanabadili mawazo.

By | October 27, 2015

Habari za leo rafiki? Unaendeleaje? Nina imani harakati zako za kuboresha maisha yako na ya wale ambao wanakuzunguka zinaendelea vizuri sana. Hongera kwa hilo. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya ya leo, tuendelee kupeana maarifa na mbinu za kuboresha maisha yetu. Kumbuka hakuna kilele cha ubora, kila siku kwenye maisha (more…)

UKURASA WA 300; Fanya Kazi Yako Na Tutakujua….

By | October 27, 2015

Kwa nini unanijua mimi? Kwa sababu ninaandika, ninaandika kitu unachoweza kusoma, ukaelewa, ukafanyia kazi na ukaona mabadiliko kwenye maisha yako. Sio kwamba ninakaa mahali na kuanza kuwaambia watu, naweza kweli kuandika, ninaweza kuandika vitu vizuri. Badala yake nakaa chini na kuandika, na wewe umenijua mimi kupitia hilo. Kwa nini unamjua (more…)

UKURASA WA 299; Chanzo Kikuu Cha Kuona Maisha Yako Ni Mabaya.

By | October 26, 2015

Kila mmoja wetu anapenda kuwa na maisha mazuri, maisha bora kulingana na vigezo vyake. Na kila mtu ana picha ya maisha mazuri kwake yana maana gani. Na picha hizi zinatofautiana. Lakini pia hakuna anayepata maisha yanayoendana na ile picha yako moja kwa moja, hasa wakati wa mwanzoni. Kuna baadhi ya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Usipigane Na Usichokitaka Na Jinsi Ya Kupata Unachotaka.

By | October 25, 2015

Habari mwanafalsafa? Karibu tena kwenye mfululizo wa makala hizi za falsafa mpya ya maisha ambapo tunaendelea kuongeza misingi muhimu kwenye falsafa yetu hii mpya ya maisha. Kumbuka misingi hii tunayojijengea ni muhimu sana na inabidi tuiishi ili kweli tuweze kuona mabadiliko makubwa kwenye maisha yetu. Katika moja ya misingi muhimu (more…)

UKURASA WA 298; Nusu Ya Matatizo Umesababisha Wewe Na Sio Mwenzako…

By | October 25, 2015

Kama umenifahamu kwa muda mrefu, namaanisha kama umekuwa unasoma makala ninazoandika, utakuwa unaujua msimamo wangu ambao uko wazi kabisa. HAKUNA KULALAMIKA, kama kitu hukipendi kibadili, kama huwezi kukibadili achana nayo. Hii ni njia rahisi sana ya kuishi. Ukiweza kuitekeleza vyema, utajipunguzia mizigo mingi na msongo wa mawazo. Lakini utaniambia siwezi (more…)

UKURASA WA 297; Punguza Hatua….

By | October 24, 2015

Kila mmoja wetu kuna mabadiliko ambayo angependa kufanya kwenye maisha yake. Lakini wengi huwa tunashindwa kutekeleza mabadiliko haya tunayotaka. Na moja ya sababu za kushindwa kubadili ni hatua nyingi ambazo zinahusika kwenye mabadiliko haya. Huwa tunaweka hatua nyingi sana ambazo kuzipitia tu ni changamoto tosha. Kwa mfano kama umeamua kuanza (more…)

UKURASA WA 296; Hofu Nimekuelewa Na Sasa Nasonga Mbele.

By | October 23, 2015

Hofu na moto ni vitu ambavyo vinafanana sana. Vyote vina faida kubwa sana na vyote pia vina hasara kubwa. Tuanze na moto.. Moto ni mzuri sana, tunatumia moto kupikia, tunautumia kupata joto, kuchemsha maji na mengine mengi. Lakini moto huu ni hatari sana, unaweza kuteketeza nyumba na vitu vyote. Lakini (more…)