Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#SheriaYaLeo (157/366); Waweke watu kwenye shauku ya kukufuatilia.

By | April 6, 2022

#SheriaYaLeo (157/366); Waweke watu kwenye shauku ya kukufuatilia. Watu huwa wanapenda kufuatilia vitu ambavyo vinawaweka juu juu. Vitu ambavyo hawana uhakika vitakwendaje. Vitu ambavyo ni tofauti kabisa na mazoea na hivyo havitabiriki. Kwa kila unachofanya, kifanye kwa namna hiyo na siyo kwa mazoea. Wafanye watu wawe wanajiuliza kipi kingine utafanya (more…)

2652; Kuchuma matunda ya chini.

By | April 5, 2022

2652; Kuchuma matunda ya chini. Ukiingia kwenye shamba jipya la matunda kama miembe au michungwa, inakuwa rahisi kuchuma matunda hayo. Kwa sababu yanakuwa yananing’inia kwa chini na karibu kabisa kufikia kwa mkono. Utaona hiyo ni fursa na kuifurahia, kwa kuwa unayapata matunda kirahisi kabisa, bila ya kutumia nguvu kubwa. Lakini (more…)

#SheriaYaLeo (156/366); Tumia udhaifu wa watu kuamini mwonekano wa nje.

By | April 5, 2022

#SheriaYaLeo (156/366); Tumia udhaifu wa watu kuamini mwonekano wa nje. Ni asili yetu binadamu kuamini kwa haraka kile ambacho tunakiona. Huwa hatuna muda wa kuchunguza kwa undani na kujua nia halisi ya mtu. Hivyo unaweza kutumia udhaifu huu kukubalika na wengine na kupata kile unachotaka. Unachopaswa kufanya ni kutengeneza mwonekano (more…)

2651; Lile wazo limepotea.

By | April 4, 2022

2651; Lile wazo limepotea. Hizi kurasa huwa naandika kutokana na yale ninayokutana nayo kila siku. Kuanzia kujifunza, kukochi wengine na mawazo yanayonijia kulingana na mambo ninayokutana nayo. Jana wakati niko safarini kuna wazo la kuandika lilinijia, nikawa nimelifikiria vyema kwa namna ya kuliandika. Lakini kutokana na uchovu sikuandika wazo hilo (more…)

#SheriaYaLeo (155/366); Dhibiti mwonekano wako.

By | April 4, 2022

#SheriaYaLeo (155/366); Dhibiti mwonekano wako. Kwenye maisha watu wanakuhukumu na kukuchukulia kutokana na mwonekano wako. Kwa kuwa watu hawana muda wa kuchunguza kwa ndani, wanachukulia mwonekano wako wa nje ndivyo ulivyo kwa ndani. Ili watu wakuchukulie kwa namna sahihi kwako, unapaswa kutengeneza mwonekano wa nje ambao unawajengea picha hiyo. Jiweke (more…)

2650; Hujakitaka kweli.

By | April 3, 2022

2650; Hujakitaka kweli. Hadithi tulizokuwa tunaambiwa utotoni zilikuwa na mafunzo makubwa kuhusu maisha ambayo haikuwa rahisi kuyaelewa kwenye kipindi cha utoto. Chukua mfano wa sungura aliyeziona ndizi na kuanza kuzirukia. Mwanzo aliona ndizi ni nzuri na zinamfaa. Kaanza kuzirukia lakini akawa hazifikii. Karuka tena na tena ila hakuzifikia. Mwisho akaamua (more…)

#SheriaYaLeo (154/366); Tumia uhaba kuongeza thamani.

By | April 3, 2022

#SheriaYaLeo (154/366); Tumia uhaba kuongeza thamani. Ni kanuni ya msingi kabisa ya uchumi kwamba kitu kinapopatikana kwa wingi, thamani yake inapungua na hivyo bei yake kuwa chini. Lakini kitu kinapopatikana kwa uhaba, thamani yake inakuwa kubwa na bei yake kuwa juu. Ili kuongeza thamani yako binafsi na ya kile unachofanya, (more…)

#SheriaYaLeo (153/366); Vaa barakoa sahihi.

By | April 2, 2022

#SheriaYaLeo (153/366); Vaa barakoa sahihi. Kwenye safari ya mafanikio na maisha kwa ujumla, unahitaji kubadilika ili kuendana na hali na watu mbalimbali. Ili uweze kuwashawishi watu, inabidi uendane nao kwa namna fulani. Na hapo ndipo uvaaji wa barakoa unapokuja. Hapa haimaanishi kuvaa barakoa tulizozoea za kujikinga na magonjwa. Bali inamaanisha (more…)

2648; Kama inabidi uwatishie siyo sahihi kwako.

By | April 1, 2022

2648; Kama inabidi uwatishie siyo sahihi kwako. Kama inabidi uwatishie watu ndiyo wafanye kile wanachopaswa kufanya, basi jua hao siyo watu sahihi kwako. Kama umempa mtu kazi, lakini haifanyi mpaka umtishie kumfukuza au kutokumlipa siyo mtu sahihi kwako. Kama kuna mtu unashirikiana naye, lakini hatekelezi wajibu wake mpaka umlazimishe au (more…)