Category Archives: KURASA ZA MAISHA

Kila siku mpya kwenye maisha yako ni sawa na ukurasa mpya wa kitabu.
Kwa kila siku mpya unachagua ufanye nini na maisha yako.
Kupitia makala hizi za KURASA ZA MAISHA, utajifunza mambo muhimu ya kufanya ili uwe namaisha bora zaidi.
Makala hizi za kurasa zinakujia kila siku.

1770; Unapoteza Muda Wako Kujifunza Na Kusoma Vitabu…

By | November 5, 2019

Unapoteza muda wako kujifunza na kusoma vitabu, kama mwisho wa siku unaendelea na maisha yako kama yalivyokuwa kabla hujajifunza. Lengo la kujifunza vitu vipya siyo kujua vitu hivyo vipya na kujisifia kwamba unajua sana. Bali kutumia yale uliyojifunza kuweza kuwa bora zaidi. Hivyo ukishajifunza unapaswa kubadili maisha yako na kufanya (more…)

1769; Hakuna Tatizo Jipya…

By | November 4, 2019

Watu wengine wanapokuwa na matatizo ni rahisi kuwafariji na kuwashauri kwamba wasijali mambo yatakwenda vizuri. Ila sisi wenyewe tunavyokuwa na tatizo kama hilo hilo, huwa tunaona kwetu ni la tofauti na hivyo ushauri kama ambao tulikuwa tunawapa wenzetu kwetu haufai. Hiyo ni kujidanganya. Hakuna tatizo jipya hapa duniani, matatizo ni (more…)

1768; Ni Kitu Gani Wanajua Ambacho Wewe Hujui?

By | November 3, 2019

Tunapoona watu wengine wanapiga hatua kubwa kuliko sisi, huwa tunakimbilia kujiambia kwamba watu hao wana bahati au wamekutana na upendeleo fulani ambao sisi hatujakutana nao. Haya ni majibu ya kujifariji, pale ambapo wengine wanapiga hatua na sisi hatupigi. Wakati mwingine tunakuwa watu wa kwanza kukosoa hatua wanazopiga wengine, japo ni (more…)

1767; Kuona, Kufikiri Na Kuongea…

By | November 2, 2019

Mtu mmoja mwenye busara amewahi kusema maneno haya; “katika watu 100 wanaoweza kuongea, ni mmoja pekee anayeweza kufikiri, katika watu 1000 wanaoweza kufikiri, ni mmoja pekee anayeweza kuona”. Ni kauli ngumu na tata ambayo huwezi kuielewa kwa sababu ya alichokieleza mtu huyo. Kwa kifupi ni kwamba kila mtu anaweza kuongea, (more…)

1766; Punguza Hiyo Mizigo, Ndiyo Inayokuzuia Usifanikiwe…

By | November 1, 2019

Maisha ni magumu, lakini kuna wakati huwa tunayafanya yawe magumu kuliko yanavyopaswa kuwa. Na tumekuwa tunafanya hivyo kupitia kujibebesha mizigo isiyo kuwa na maana wala manufaa yoyote kwetu. Kwa asili, kitu chochote kisichokuwa na matumizi kwenye mwili huwa kinaondolewa. Ndiyo maana utakula chakula ambacho ni kitabu mno, ambacho huenda umekigharamia (more…)

1765; Wazo Lako Linahitaji Muda…

By | October 31, 2019

Wazo bora ni kama mvinyo, kadiri muda unavyokwenda, ndivyo mvinyo unavyokomaa na kuwa bora zaidi. Wazo bora pia ni kama uwekezaji, kadiri muda unavyokwenda ndivyo uwekezaji unakua thamani. Usitegemee kupata wazo siku moja, kuchukua hatua halafu kupata matokeo makubwa unayotarajia. Mafanikio huwa hayaendi hivyo. Unapata wazo ambalo unaamini ni bora (more…)

1764; Kutokupata Kila Unachotaka Ni Manufaa Kwako…

By | October 30, 2019

Ipo kauli moja ya utani kwamba pale Mungu anapotaka kutuadhibu, huwa anatupa kila tunachotaka. Kauli hiyo siyo tu ya utani, bali imebeba ukweli mkubwa sana kuhusu maisha. Unaweza kuona maisha yako hayajakamilika kwa sababu kuna vitu unataka lakini bado hujavipata, lakini hilo lina manufaa kwako. Kwa kukosa baadhi ya vitu (more…)

1763; Hakuna Kizuri Kinachodumu Milele…

By | October 29, 2019

Kuna kitabu kimoja kifupi na kizuri sana ambacho kinaelezea tabia yetu sisi binadamu kuyapinga mafanikio. Kitabu hicho kinaitwa WHO MOVED MY CHEESE, ambacho kinaeleza hadithi ya panya wanne ambao walizoea kupata jibini kwenye eneo walilozoea, siku moja wakaenda eneo hilo na kukuta hakuna tena jibini. Kuna ambao walisonga mbele na (more…)

1762; Watu Wananunua Matumaini…

By | October 28, 2019

Unafikiri ni kitu gani kinapelekea mtu kucheza bahati nasibu ya shilingi mia tano au elfu moja? Wachezaji wengi wa bahati nasibu hizi wanajua kabisa kwamba hawawezi kushinda, kwa sababu washindi ni wachache na wachezaji ni wengi. Lakini kinachowasukuma kucheza bahati nasibu hizi ni yale matumaini wanayokuwa nayo kwamba huenda nao (more…)

1761; Kabla Hujafikiria Kuibadili Dunia…

By | October 27, 2019

‘Nataka kuibadili dunia…’ Ni kauli maarufu kwa wengi, huwa tunajiwekea lengo kubwa kiasi hicho kupitia chochote tunachofanya, na kufikiria tunaweza kuwa na mchango mkubwa hapa duniani kama tutaweza kuibadili. Lakini hilo ni lengo ambalo siyo tu hatuwezi kulifikia, bali pia tunajidanganya, kwa sababu ni kitu ambacho kipo nje ya uwezo (more…)