UKURASA WA 980; Uongo Unaingilia Masikioni, Na Kutokea Machoni…

By | September 6, 2017

Upo usemi maarufu kwamba kusoma huwezi, je picha nayo huoni? Tunaweza kuuboresha usemi huu na ukawa kusikia husikii, je hata kuona nako shida. Iko hivi rafiki, uongo wowote huanzia kwenye kusikia. Yaani watu watakuambia mambo mengi ambayo ni uongo. Unaweza kusikiliza na ukaamini kabisa unachoambiwa ndiyo kilivyo au ndiyo uhalisia. (more…)

BIASHARA LEO; Nenda Zaidi Ya Matatizo Na Mahitaji.

By | September 5, 2017

Unapoanzisha biashara, kitu kikubwa ni kuangalia matatizo au changamoto ambazo watu wanazo, kisha unakuja na suluhisho la matatizo na changamoto hizo. Hilo ndilo ambalo kila mfanyabiashara anafanya. Na kwa kuwa huna cha kuwazuia watu kufanya unachofanya wewe, kutegemea hilo pekee hakukuwezeshi kuwa na wateja waaminifu kwa biashara yako. Wateja waaminifu (more…)

UKURASA WA 979; Kubali, Kisha Chukua Hatua.

By | September 5, 2017

Watu wengi wanateseka katika maisha kwa sababu moja kubwa, kuna vitu hawataki kuvikubali. Huenda ni hali walizonazo, au pale ambao wamejikuta katika kipindi fulani cha maisha yao. Wengi hukazana kukataa, kuona kwamba wao hawastahili kupata kile ambacho wamepata. Wengine hutafuta nani wa kumtupia lawama, nani wa kumlalamikia katika hali za (more…)

#TAFAKARI YA LEO; TATIZO SIYO KUJUA NINI CHA KUFANYA…

By | September 4, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari (more…)

BIASHARA LEO; Anza Na Kitu Ambacho Watu Tayari Wanakihitaji.

By | September 4, 2017

Kwenye kitabu cha The Lean Startup, mwandishi Erick Ries anatushirikisha dhana ya MVP ambayo kirefu chake ni Minimum Viable Product. Dhana hii inaeleza kwamba unapoanza biashara, anza na bidhaa ambayo haujakamilika, lakini iwe na sifa ambazo inaweza kumsaidia mtu. Badala ya kutumia nguvu nyingi kuja na bidhaa au huduma kamili, (more…)

UKURASA WA 978; Mambo Mawili Muhimu Kuhusu Fursa.

By | September 4, 2017

Kwanza; fursa ni nyingi mno, na zitaendelea kuwa nyingi kila siku. Mbili; hakuna fursa ambayo ikikupita ndiyo basi tena, kwa kifupi huwezi kupitwa na fursa yoyote. Nimeanza na hayo mawili kwa sababu wengi hawayaelewi au hawayakubali na hilo limekuwa linawaingiza kwenye matatizo makubwa. Watu wengi wamekuwa wakiaminishwa kwamba kuna uhaba (more…)

#TAFAKARI YA LEO; WATU WABAYA KATIKATI YA WATU WABAYA…

By | September 3, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Msingi wetu wa mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU na KUJITUMA, ambapo tunaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu. (more…)

BIASHARA LEO; Kosa Kubwa Wanalofanya Wanaoanza Biashara…

By | September 3, 2017

Upo usemi kwamba mwanzo ni mgumu, na usemi huu unafanya kazi kwenye kila jambo, kuanzia ukuaji wetu mpaka shughuli zetu. Pata picha ya mtoto mdogo ambaye anajifunza kutembea, anasimama na kuanguka, anapiga hatua moja anaanguka. Lakini mtoto huyu hasemi kutembea ni kugumu basi naachana nako. Bali anaendelea na baada ya (more…)

UKURASA WA 977; Tawala Hasira Zako…

By | September 3, 2017

Kitu cha kwanza muhimu kabisa unachopaswa kufanya kwenye maisha yako, ni kutawala hasira zako. Kuhakikisha hasira zako zinakuwa mbali sana kiasi kwamba haziwezi kufikiwa kirahisi. Tawala hasira zako kiasi kwamba chochote kinachoweza kutokea, kinachosemwa au kufanyika unaendelea kubaki na utulivu wako. Hili ni muhimu kwa sababu; Wapo watu ambao watajaribu (more…)