UKURASA WA 567; Watu Utakaokutana Nao Siku Ya Leo…

By | July 20, 2016

Siku ya leo utakutana na watu wema, watu wenye roho nzuri na wenye kukutakia mema kwenye maisha yako na kile unachofanya.  Watu hawa watakufanya uone jinsi gani maisha ni mazuri na binadamu wanavyothaminiana. Watakupa hamasa ya kuendelea kufanya kile unachofanya kwa ubora zaidi. Siku ya leo pia utakutana na watu (more…)

UKURASA WA 566; Mafanikio Yanaanza Na Imani….

By | July 19, 2016

Kabla wengine hawajakuamini, ni lazima ujiamini wewe mwenyewe kwanza. Kabla wengine hawajaamini kwenye ile biashara unayofanya na kuwa wateja, ni lazima wewe mwenyewe uiamini biashara hiyo kwanza. Kabla wengine hawajakuamini kwamba unaweza na kukupa kazi au dili nzuri ni lazima wewe mwenyewe ujiamini kwamba unaweza. Imani inaambukizwa, unachoamini ndicho ambacho (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Sisi Ni Bora Kuliko Wao, Uongo Tunaojidanganya Mara Zote Na Kuharibu Mahusiano Yetu Ya Kijamii.

By | July 17, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni imani yangu kubwa kwamba unaendelea vyema huku ukiyaendesha maisha yako kwa misingi ya falsafa tunayojifunza kila siku. Maisha bora, yenye furaha na mafanikio yanaanza na wewe mwenyewe, kwa kuishi vile ambavyo unapenda kuishi, kwa kufanya kile ambacho unaweza kukifanya vizuri. Duniani tupo watu tofauti, (more…)

UKURASA WA 564; Kitakachokufanya Uwe Mtumwa Wa Wengine Ni Hiki…

By | July 17, 2016

Mafanikio makubwa kwenye maisha yako yanaanza na uhuru wako. Huwezi kusema una mafanikio kama huna uhuru. Uhuru ndiyo utakuwezesha kufanya kile ambacho unataka kufanya kwenye maisha yako, ambacho ndiyo kinakuletea furaha na mafanikio. Watu wengi bado wameendelea kuwa watumwa wa wengine, wameshindwa kuwa huru na hivyo kujikuta maisha yao yanaamuliwa (more…)

UKURASA WA 563; Jinsi Ya Kuepuka Wivu Wa Wengine Kuharibu Mipango Yako…

By | July 16, 2016

Moja ya tabia ambazo wanadamu tunazo ni wivu, tunachotofautiana ni namna gani tunaweza kudhibiti na kutumia wivu wetu. Kwa upande mmoja kuna ambao wanaweza kudhibiti wivu wanaoupata na hivyo kutokufanya jambo lolote baya, pia kuna wanaoweza kuutumia kama changamoto kwao kufanya makubwa zaidi. Kwa upande mwingine kuna ambao hawawezi kudhibiti (more…)

UKURASA WA 562; Nje Ya Uwezo Wako…

By | July 15, 2016

Linapokuja swala la maisha ya mafanikio, uwezo unaweza usitumike sana. Ndiyo tunajua ya kwamba kila mtu ana uwezo wa tofauti, uwezo mkubwa ambao upo ndani yake, ambao ndiyo unamwezesha kupata matokeo ya tofauti na wanayopata wengine. Lakini katika kufikia mafanikio makubwa, uwezo pekee unaweza usitoshe, badala yake unahitaji kuwa tayari (more…)

UKURASA WA 561; Tengeneza Sheria Zako Mwenyewe….

By | July 14, 2016

Unapoanza kufanya kitu chochote kipya kwenye maisha, unaanza kwa kuiga. Unaangalia wale ambao ni bora kwenye kile unachotaka kuwa bora, unaona wanafanyaje kisha na wewe unaanza kufanya kama wao. Kwa kuiga utapiga hatua kubwa, kutoka mtu ambaye hajui kabisa mpaka mtu anayejua kile anachofanya. Changamoto moja ya kuiga ni kwamba (more…)

UKURASA WA 560; Waliokuambia Hapana…

By | July 13, 2016

Kama kuna neno ambalo umeshalisikia mara nyingi kwenye maisha yako, huenda ni neno HAPANA. Hili ni neno ambalo wengi wamekuambia pale ambapo umekua unajaribu kufanya mambo ya tofauti au mambo makubwa kuliko ambavyo imezoeleka na wengine. HAPANA ni neno kali na linalokatisha tamaa hasa pale linapotoka kwa mtu ambaye unamwamini (more…)

UKURASA WA 559; Huu Ndiyo Uhuru Kamili Kwako…

By | July 12, 2016

Kila mtu anapenda kufanikiwa, lakini siyo kila mtu yupo tayari kulipa gharama za mafanikio. Ili kufanikiwa na kuishi maisha bora na yenye furaha, kitu cha kwanza kabisa unachohitaji kuwa nacho ni uhuru. Uhuru wa maisha yako na kuweza kufanya kile ambacho unakipenda na unajua ni muhimu kwako na kwa wanaokuzunguka. (more…)