UKURASA WA 558; Hatua Tatu Za Kupata Chochote Unachotaka…

By | July 11, 2016

Kupata unachotaka kwenye maisha yako inawezekana, ila siyo kitu rahisi. Na hii ndiyo sababu ni wachache sana ambao wameweza kupata kile wanachotaka, wengi wanapokutana na ugumu wanaacha na kukubali kile ambacho wamekipata. Hakuna kitu kizuri na chenye thamani ambacho kinapatikana kwa urahisi, unahitaji kuweka juhudi, kuwa mvumilivu na kutokukata tamaa. (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; TATU MARA TATU, Vitu Vitatu Vyakufanya Kila Siku Ili Kuwa Na Maisha Bora Yenye Furaha Na Mafanikio.

By | July 10, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Unatumiaje yale unayojifunza kupitia falsafa hii mpya ya maisha kufanya maisha yako kuwa bora zaidi kila siku? Hili ni swali muhimu unalopaswa kujiuliza kila siku. Mwanafalsafa Plato amewahi kunukuliwa akisema unexamined life is note woth living, akiwa na maana kwamba maisha ambayo hayachunguzwi, hayana thamani (more…)

UKURASA WA 557; Wale Waliopo Chini, Hiki Ndiyo Kinawaweka Chini…

By | July 10, 2016

Kwenye kila eneo la maisha, kuna watu ambao wapo chini. Watu ambao wana maisha magumu sana kuliko wengine wote. Watu ambao kipato chao ni kidogo sana na wakati mwingine ni watu ambao wanafanya mambo mengi sana. Lakini bado wapo chini na wanaendelea kuwa chini. Ni kitu gani kinawafanya waendelee kuwa (more…)

UKURASA WA 556; Gharama Ya Bei Unazoweka Kwenye Biashara Yako…

By | July 9, 2016

Kila kitu kwenye maisha yetu kina gharama. Kuna gharama fulani unatakiwa kulipa ili uweze kupata kile ambacho unataka. Gharama hii inaweza kuwa kwenye mfumo wa fedha, muda, juhudi na hata utu binafsi. tunalipa gharama kwenye kila eneo la maisha yetu, kuanzia kwenye familia, kazi, biashara na hata kwenye jamii tunazoishi. (more…)

UKURASA WA 555; Hofu Inavyotumika Kukunyanyasa…

By | July 8, 2016

Moja ya hisia kali sana kwetu binadamu ni hofu. Hofu inaweza kutuzuia kuchukua hatua kubwa kwenye maisha yetu na pia hofu inaweza kutufanya tuchukue hatua ambazo siyo bora kwetu. Kwa watu kujua hili, wamekuwa wakitumia hofu kunyanyasana wao kwa wao. Pale ambapo mtu anataka ufanye kitu na hana njia ya (more…)

UKURASA WA 554; Kabla Hujasema Haiwezekani Angalia Hiki…

By | July 7, 2016

Kufikia mafanikio makubwa, kupata kile ambacho hujawahi kupata, ni njia ngumu sana ambayo hujawahi kupita. Katika ugumu huu kuna wakati unaweza kushawishika siyo tu kwamba njia unayopita ni ngumu, bali kile unachofanya hakiwezekani. Na ukishajishawishi kwamba haiwezekani unajua ni nini kinafuata, unaacha kufanya na malengo yako yote yanakuwa yameishia hapo. (more…)

KITABU; MIMI NI MSHINDI, Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu.

By | July 7, 2016

Karibu rafiki upate kitabu MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu. Kitabu mimi ni mshindi kinakuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi, maisha ambayo yanakutofautisha wewe na wengine wengi ambao wanashindwa kufikia mafanikio makubwa. Ukiangalia maisha ya washindi na maisha ya wale ambao wanashindwa yapo tofauti kabisa. Kuna namna ambavyo (more…)

UKURASA WA 553; Ni Lazima Ukubali Kwanza…

By | July 6, 2016

Mtu ambaye hajui kama anakosea, huwezi kumrekebisha, kwa sababu anahisi yupo sahihi kwa kile anachofanya. Hivyo hata kama utamrekebisha namna gani, ataendelea kufanya kile anachofanya, kwa sababu anajua yupo sahihi. Hapa ndipo changamoto nyingi hasa za mahusiano na mafanikio zinapoanzia. Kama wewe mwenyewe hukubali kwamba unakosea, huwezi kubadili kile unachofanya, (more…)

UKURASA WA 552; Mchango Wako Ni Jinsi Ulivyo…

By | July 5, 2016

Kama kuna mchango wowote unaoweza kutoa kwenye dunia hii, basi unautoa kwa jinsi ulivyo wewe. Na siyo kwa jinsi unavyofikiri au kusema utatoa mchango gani kwenye dunia hii. Jinsi ulivyo, haiba yako na matendo yako ndiyo vinavyotoa mchango kwenye dunia hii kwa kuanzia na wale wanaokuzunguka. Mchango wako unatokana na (more…)

UKURASA WA 551; Kushindwa Ni Sehemu Ya Kukua…

By | July 4, 2016

Mtoto hawezi kujua kutembea sawasawa bila ya kuanguka. Anayejifunza kuendesha baiskeli hawezi kujua kuendesha kama hatoanguka mara kadhaa. Watu wote ambao tunawaona leo wameweza kufanya mambo makubwa, hawakuanza kuyafanya mambo hayo tangu awali, bali walishindwa sana na kujifunza kupitia kushindwa kwao. Hivyo basi kushindwa kwenye kile unachofanya siyo jambo baya (more…)