UKURASA WA 331; Chelewa Kwa Makusudi….

By | November 27, 2015

Ni muhimu sana kujali muda na kuwahi kwenye kila kitu ambacho unahusika nacho wewe. Ila kuna maeneo ambayo unahitaji kuchelewa kwa makusudi. Kwa kuchelewa huku inakuwa ni faida kubwa kwako baadae. Jana katika makala hizi za kurasa tuliona jinsi ambavyo jamii inakuaminisha kwamba unapitwa na hivyo kukusukuma ununue kila kitu (more…)

UKURASA WA 330; Unapitwa….

By | November 26, 2015

Tunaishi kwenye dunia ambayo tunasukumwa sana kuwa wanunuaje, wateja. Tunalazimika kununua vitu vingi ambavyo hata hatuna matumizi navyo, na kama tunayo basi sio muhimu sana. Tunalazimika kununua kwa sababu tu tunaogopa tusipitwe. Na hapa ndipo utumwa mkubwa wa dunia unapoanzia. Sio vibaya kununua, ila kununua kwa msukumo ni utumwa mkubwa (more…)

WORLD CLASS; Mbinu Za Kisaikolojia Za Kuidanganya Akili Yako Ili Uweze Kufanya Kazi Zaidi Hata Kama Umechoka

By | November 25, 2015

Hakuna ubishi kwamba ili uweze kufikia mafanikio makubwa sana ni lazima uweze kufanya kazi zaidi ya kawaida. Ni lazima uweze kujitoa zaidi, kufanya kazi kubwa na kuwa tayari kwenda hatua ya ziada hata kama wengine hawawezi kufanya hivyo. Kama bado unakataa hili, kama bado hujalichukua hili kwenye nafsi yako, ninachoweza (more…)

UKURASA WA 329; Kama ungeweza kuona kitu hiki vizuri…

By | November 25, 2015

Kama ungeweza kuziona fursa haraka kama unavyoyaona makosa ya wengine, basi ungekuwa mbali sana. Kama ungekuwa unachukua hatua haraka kama unavyochukua kuwakosoa wengine, maisha yako yangekuwa bora sana. Lakini hufanyi hivyo, kwa sababu labda hujajua jinsi ya kufanya, na nitakushirikisha hapa. Urahisi wa kuona makosa ya wengine. Ni rahisi sana (more…)

Swali moja muhimu sana ninalojiuliza kila siku asubuhi.

By | November 24, 2015

Habari za leo rafiki? Naamini upo vizuri sana na maisha yako yanaendelea kuwa bora kadiri siku zinavyokwenda. Vizuri na hongera sana kwa hilo. Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya mazuri na muhimu sana, ambapo tunashirikishana mambo mbalimbali yanayohusu mafanikio na kuwa na maisha bora. Leo nitakushirikisha swali moja muhimu sana (more…)

UKURASA WA 328; Kuwa ‘Bize’ Vs Kuzalisha.

By | November 24, 2015

Kuwa bize na kuzalisha ni vitu viwili tofauti kabisa. Mara nyingi wale wanaoonekana kuwa bize sana huwa wanakuwa na uzalishaji mdogo sana, japo wao wanaweza kufikiri kinyume chake. Kila mtu anaweza kuwa bize, lakini ni wachache sana wanaoweza kuwa na uzalishaji mkubwa. Unaweza kuwa bize kwa kufanya mambo ambayo hayana (more…)

Je unajenga biashara au unafanya biashara? Soma hapa kujua kipi muhimu kwako.

By | November 23, 2015

Mafanikio ya biashara yoyote ile yanaanza na mafanikio ya mfanyabiashara mwenyewe. Biashara itakuwa kwa kiasi kile ambacho mmiliki wake amekua, na haiwezi kwenda zaidi. Wafanyabiashara wengi wamekuwa wanashindwa kukuza biashara zao kwa sababu wao wenyewe hawakui. Na hili limekuwa tatizo kubwa la biashara nyingi kushindwa au hata kudumaa kabisa. Unakuta (more…)

UKURASA WA 327; Wewe Ni Mtumwa Wa Nani?

By | November 23, 2015

Pamoja na kuishi kwenye dunia yenye uhuru mkubwa, bado watu wengi wanaishi maisha ya kiutumwa. Watu wengi wanaishi maisha ambayo hawana uhuru wa kuamua wafanye nini na maisha yao. Jambo lolote ambalo ni muhimu kwao kufanya, hawawezi kulifanya mpaka mtu au watu ambao amechagua kuwa mtumwa kwao walidhibitishe. Kama wakiona (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Nguvu Kubwa Inayokurudisha Nyuma Na Jinsi Ya Kuishinda.

By | November 22, 2015

Habari za leo mwanafalsafa? Karibu tena kwenye makala zetu hizi za falsafa mpya ya maisha ambapo tunapata maarifa sahihi ya kuishi maisha yetu kwa furaha na mafanikio. Kila mmoja wetu anastahili maisha bora, ya furaha kwake na mafanikio makubwa. Lakini wengi hawapati nafasi ya kuishi maisha hayo kutokana na kukosa (more…)