NENO LA LEO; Kama Hujui Unakoenda Utaishia Hapa.

By | April 4, 2015

“If you don’t know where you are going, you’ll end up someplace else.” ― Yogi Berra Kama hujui ni wapi unakoenda, utaishia sehemu yoyote ile. Hasara kubwa kwenye maisha ni kuishi maisha ambayo hujui yanakupeleka wapi. Haya ni maisha ambayo hayana malengo na mipango. Ni maisha ya kufanya chochote kinachojitokeza (more…)

BIASHARA LEO; Umuhimu Wa Hadithi Ya Biashara Yako.

By | April 3, 2015

Tunaishi kwenye dunia ambayo watu hawanunui kwa sababu tu unauza. Zamani biashara ilikuwa rahisi, uza na watakuja kununua. Fungua biashara na watu watakuja. Tangaza biashara yako kwenye vyombo vinavyowafikia wafikia wengi na utapata wateja wengi. Ila sasa hivi mambo mengi yamebadilika. Watu hawanunui tena kwa sababu wewe unauza, hii ni (more…)

UKURASA WA 93; Linda Sana Mawazo Yako.

By | April 3, 2015

Maisha yako yanatokana na mawazo yako. Kitu chochote ambacho unakifanya au unakutana nacho, hakitokei tu kwa bahati mbaya, ila kinaanzia kwenye mawazo yako. Mawazo yako yana nguvu kubwa sana ya kuumba. Na ndio yameumba kila kitu kinachoendele akwenye maisha yako. Kama mawazo yako ndio yanayotengeneza maisha yako, hii ina maana (more…)

NENO LA LEO; Hapa Ndipo Alipo Anayetaka Kukurudisha Chini.

By | April 3, 2015

“Whoever is trying to bring you down is already beneath you.” ― Habeeb Akande Yeyote anayekazana kukurudisha chini, tayari yupo chini yako. Angalia kwa makini kwenye maisha yako, kazi yako na hata biashara yako. Angalia wale watu ambao wanajaribu kukurudisha chini, angalia wale watu ambao wanakukatisha tamaa, angalia wale watu (more…)

BIASHARA LEO; Lengo La Biashara Sio Kupata Faida, Bali Ni Hili Hapa.

By | April 2, 2015

Unajua lengo la biashara ni nini? Lengo la biashara sio kupata faida, lengo la biashara sio kupata mafanikio makubwa, haya yote ni matokeo ya lengo kuu la biashara. Yaani ukiweza kutimiza lengo hili kuu la biashara, haya mengine yote yanatimia bila ya tatizo lolote. Biashara nyingi zinashindwa kuendelea, kupata faida (more…)

UKURASA WA 92; Usipoteze Muda Kwa Vitu Vidogo Vidogo.

By | April 2, 2015

Tunaishi kwneye dunia yenye kelele nyingi sana. Maendeleo makubwa yaliyokuja kwenye teknolojia pia yameleta usumbufu mkubwa sana. Kwa simu hizi za kisasa tunazotumia, unaounganishwa na dunia nzima kwa masaa 24 kwa siku. SOMA; BIASHARA LEO; Ondoka, Hakuna Aliyekuita Hapa. Unaweza kuona ni kitu kizuri, kuweza kupata kila taarifa inayotokea masaa (more…)

NENO LA LEO; Hiki Ndio Chanzo Cha Wivu.

By | April 2, 2015

“Envy comes from people’s ignorance of, or lack of belief, in their own gifts.” ― Jean Vanier Wivu unatokana na ujunga wa watu, au kushindwa kuamini zawadi zao wenyewe. Unapokuwa na wivu kwa watu wengine maana yake unaona wewe huwezi. Kama unaona huwezi maana yake bado hujajua zawadi iliyopo ndani (more…)

BIASHARA LEO; Ondoka, Hakuna Aliyekuita Hapa.

By | April 1, 2015

Karibu tuendelee kupeana dondoo muhimu sana za wewe kufanikiwa kupitia biashara unayofanya. katika dondoo hizi tunaangalia makosa yanayofanywa na wafanyabiashara wengi na yanayowazuia kupata mafanikio. Pia tunaangalia changamoto zinazowazuia wafanyabiashara wengi kushindwa kufanikiwa kupitia biashara zao. Jinsi unavyotoa huduma au bidhaa zako kwa wateja, jinsi unavyozungumza nao, jinsi unavyowapokea, kunaeleza (more…)

UKURASA WA 91; Utashi, kitu muhimu kwako kufikia mafanikio.

By | April 1, 2015

Kuna vitu viwili muhimu sana unavyohitaji kuw anavyo ili uweze kufikia malengo na mipango uliyojiwekea na kufikia mafanikio makubwa. Vitu hivi viwili vinatoka ndani yako na vinaweza kukujenga au kukuangusha. Vitu hivi viwili ni nidhamu na utashi. Nidhamu tulishaijadili kwenye ukurasa wa nane. Kama hukupata nafasi ya kusoma kuhusiana na (more…)

MIAKA MIWILI YA AMKA MTANZANIA; Kwa Nini Ipo Na Itaendelea Kuwepo Na Mambo Mazuri Yanayokuja.

By | April 1, 2015

Tarehe 31/03/2013 ilikuwa ndio siku ya kwanza kwa makala ya kwanza kwenda hewani kwenye mtandao huu wa AMKA MTANZANIA. Kipindi hiko wakati naanzisha mtandao huu mambo hayakuwa kama sasa, watu walikuwa na muamko mdogo wa kusoma habari za aina hii na hata kujisomea vitabu. Leo hii miaka miwili tu mbele, (more…)