Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

BIASHARA LEO; Je kinafanya kazi?

By | June 25, 2017

Unapokuwa mfanyabiashara, maisha yako unayajenga kwenye msingi wa kuuza vitu, yaani unapata kipato cha kuendesha maisha, kupitia kile unachouza. Sasa kwa kuwa hayo ni maisha, lazima uwe makini sana kwa sababu kosa dogo unaloweza kufanya, litakuwa na madhara makubwa sana kwako. Wapo watu ambao wameharibu biashara zao kwa makosa madogo (more…)

UKURASA WA 907; Njia Nyingine Ya Kuishinda Hofu Ni Hii…

By | June 25, 2017

Kuielewa hofu, ni hatua muhimu sana ya kuweza kuishinda, isikuzuie kuchukua hatua ya mafanikio. Kwa sababu kwenye kila jambo ambalo unataka kufanya, hasa linapokuwa jipya na kubwa, hofu hutawala. Hofu hii inachangiwa na mengi, kwa kuanza na wewe binafsi, wanaokuzunguka na hata mazingira. Hii inatokana na ugeni wa jambo, mtazamo (more…)

BIASHARA LEO; Kamwe Usimlalamikie Mteja….

By | June 24, 2017

Ndiyo kuna wateja wasumbufu, wateja ambao wanayafanya maisha yako kibiashara kuwa magumu mno. Wateja wanaotaka kunufaika wao bila ya kujali biashara yako. Wateja wanaotaka kupata zaidi kwa kutoa kidogo. Wateja wanaokopa na hawalipi. Wateja ambao wakishakopa wanahama kabisa. Lakini nisichotaka wewe ufanye ni kukaa na kuanza kuwalalamikia wateja wa aina (more…)

UKURASA WA 906; Jipe Sababu Ya Kujithamini…

By | June 24, 2017

Kuna watu wanajichukia wao wenyewe, Wapo pia ambao hawajithamini kabisa, Kwenye kila jambo wanajiona kabisa hawawezi, au wameshashindwa kabla hata hawajaanza. Hakuna sumu kubwa ya mafanikio kama hii. Kwa sababu kama hujithamini, hutaweka juhudi kuweza kufanya makubwa. Kwenye kila jambo utajirudisha nyuma wewe mwenyewe. Kwenye kazi utajiweka nyuma, hutathubutu kusimama (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; KUJIJENGA KAMA MTU NI KAZI….

By | June 24, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii bora sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo bora. Ni kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana kwenye maisha yetu. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu KUJIJENGA KAMA MTU…. Mafanikio hayatokani na kile (more…)

BIASHARA LEO; Kikwazo Cha Elimu Kubwa Kwenye Mafanikio Ya Biashara….

By | June 23, 2017

Watu wengi wenye elimu kubwa wamekuwa wakishindwa kwenye biashara, huku wenye elimu za kawaida au za chini kabisa wakifanikiwa sana kwenye biashara. Hii ni kwa sababu, kufanikiwa kwenye biashara, haihitaji akili nyingi, na wakati mwingine akili nyingi zinakuwa kikwazo. Watu wenye elimu kubwa wamekuwa wakifikiria na kuchambua sana mambo, kiasi (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; ANDIKA MANENO HAYA SITA LEO NA KILA SIKU….

By | June 23, 2017

Habari za asubuhi ya leo rafiki? Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Tutumie nafasi hii vizuri rafiki. Asubuhi ya leo tunakwenda kutafakari kuhusu maneno sita muhimu yanayotuongoza kwenye maisha yetu ya (more…)

UKURASA WA 905; Kulalamikia Nguvu Ya Mvutano….

By | June 23, 2017

Kinachotuzuia sisi binadamu kuruka kama ndege, ni kwa sababu hatuna njia ya asili ya kuweza kuishinda nguvu ya mvutano ya dunia. Ndiyo maana ukiruka juu, lazima utashuka chini, kwa sababu dunia inakuvuta. Hii pia ndiyo ilikuwa changamoto ya kutengeneza ndege ya kwanza kuruka angani. Ilikuwa lazima kuweza kutengeneza mfumo wa (more…)