Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 582; Tofauti Kubwa Ya Jana Na Leo…

By | August 4, 2016

Kama ulichofanya jana kinaonekana kikubwa kuliko ulichofanya leo, basi leo hujafanya kitu kikubwa. Na tunaweza kusema bila ya shaka kwamba leo hujafanya chochote, kama lengo lako ni kuwa na mafanikio kwenye maisha. Kama umekuwa unawaambia watu na kujiambia mwenyewe kwamba enzi zako ulikuwa unafanya makubwa, basi unadhihirisha kwamba sasa hivi (more…)

BIASHARA LEO; Hakuna Kitakachotokea Kwenye Biashara Yako Mpaka Ufanye Vitu Hivi Viwili…

By | August 3, 2016

Hakuna kitakachotokea kwenye biashara yako mpaka pale utakapofanya vitu hivi viwili muhimu sana na kwa mfuatano sahihi. Kwanza muuzie mtu kile unachotoa, iwe ni huduma au bidhaa. Pili mtu aridhishwe na kile ulichomuuzia. Hii ndiyo misingi inayobeba biashara yako. Mengine yote unayofanya kwenye biashara kama hayaipeleki biashara kwenye misingi hii (more…)

UKURASA WA 581; Huenda Tatizo Siyo Juhudi…

By | August 3, 2016

Wote tunajua ya kwamba ili kufanikiwa kwenye jambo lolote, juhudi zinahitajika. Na tena siyo juhudi tu, bali juhudi kubwa. Hili halina ubishi. Lakini kuna watu wengi ambao wamekuwa wanaweka juhudi kubwa sana na hawayafikii mafanikio waliyokuwa wanayatazamia. Wapo watu wamefanya kazi siku saba za wiki, miezi 12 ya mwaka kwa (more…)

UKURASA WA 580; Kama Hutaki Kubaki Kwenye Kundi….

By | August 2, 2016

Ni kitu ambacho wote sasa tunajua ya kwamba huwezi kufanikiwa kama unafuata kundi la watu. Hii ina maana kwamba kama unaendesha maisha yako kama kila mtu anavyoyaendesha, kwa kufanya kile ambacho wengi wanafanya na kwa namna wanavyofanya, itakuwa vigumu kwako kufikia mafanikio makubwa. Kwa nini? Kwa sababu watu wengi hawapendi (more…)

UKURASA WA 579; Hamasa Ni Moja Ya Kazi Zako…

By | August 1, 2016

Safari hii ya kuelekea kwenye mafanikio siyo safari rahisi. Imejaa changamoto na vikwazo vya kila aina. Kuna wakati utajikuta upo njia panda na unaelekea kukata tamaa. Huu ni wakati mgumu sana kwa mtu yeyote yule, na usipokuwa makini wakati huo unaweza kuwa ndiyo mwisho wa safari yako ya mafanikio. Kitu (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mbio Za Sakafuni, Zisizofika Ukingoni.

By | July 31, 2016

Mbio za sakafuni huishia ukingoni, huu ni usemi wa wahenga ambao una ukweli halisi. Kwa sababu kila sakafu ina ukingo, unapokimbia kwenye sakafu ukifika kwenye ukingo wa sakafu mbio zimeishia pale. Maisha yetu ni mbio za sakafuni, kwa sababu kila mmoja wetu anajua kwamba hatoishi milele, siku moja wote tutakufa, (more…)

UKURASA WA 578; Epuka Vitu Hivi Vinavyoua Ubunifu Wako….

By | July 31, 2016

Tunahitaji sana ubunifu kwenye maisha yetu ya kila siku. Kwa chochote tunachofanya kwenye maisha yetu, tunahitaji ubunifu ili kupata matokeo bora na ya tofauti. Ni kupitia matokeo haya ndiyo tunaweza kujijengea mafanikio makubwa. Pamoja na juhudi kubwa tunazoweka ili kuwa na ubunifu, kuna vitu ambavyo vimekuwa vinaua ubunifu wetu. Vitu (more…)

UKURASA WA 577; Vipo Ndani Ya Uwezo Wetu….

By | July 30, 2016

Vitu tunavyotaka kukamilisha kwenye maisha yetu, vipo ndani ya uwezo wetu. Vile ambavyo tunataka kuwa kwenye maisha yetu ipo ndani ya uwezo wetu. Malengo makubwa ambayo tunataka kuyafikia kwenye maisha yetu, yapo ndani ya uwezo wetu. Ndoto kubwa tunazoota kwenye maisha yetu, taswira ya amisha bora tunayoipata ni kitu ambacho (more…)

BIASHARA LEO; Kuwa Sehemu Sahihi Kwa Wakati Sahihi…

By | July 29, 2016

Moja ya vitu ambavyo unahitaji kwenye biashara ni kuwa na taarifa sahihi kwa wakati sahihi. Na taarifa hizi zitakuwezesha wewe kufanya maamuzi sahihi kwa pale ulipo kibiashara ili kuweza kusonga mbele zaidi. Mafanikio ya biashara yanategemea wakati uliopo na kile unachofanya. Kwa mfano mtu aliyekuwa anajua matumizi ya kompyuta wakati (more…)

UKURASA WA 576; Muda Mfupi Na Muda Mrefu…

By | July 29, 2016

Ni tabia ya binadamu kupenda vitu vya muda mfupi, vitu vinavyoonekana haraka. Ni sheria ya asili kwamba vitu vizuri haviji haraka, na mambo yote bora yanatokea kwa muda mrefu. Hapa ndipo unapoanzia mkanganyiko ambao unawazuia wengi kupata kile wanachotaka. Kumbuka mara zote unapokwenda kinyume na sheria za asili, unapoteza. Unapoangalia (more…)