Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#BIASHARA LEO; Viwango Vya Kuepuka Kwenye Biashara Yako.

By | February 12, 2016

Kwenye biashara yoyote unayofanya au unayoingia kufanya, kuna viwango ambavyo waliotangulia kufanya biashara hiyo walishaviweka. Kuna utaratibu fulani ambao karibu kila mtu anayefanya biashara ya aina hiyo huwa anaufuata. Lakini ukichunguza kwa makini, huoni maana au mantiki yoyote ya kufanya kitu hiko. Hivi ni viwango ambavyo unahitaji kuviepuka, hivi ni (more…)

UKURASA WA 408; Mara Moja Tu Na Sitarudia Tena…

By | February 12, 2016

Watu wote ambao ni waongo sana leo, hawakuanza kuwa waongo wakubwa siku moja, walianza kidogo kidogo na hatimaye wakajikuta katikati ya uongo mkubwa. Watu wote ambao ni wezi na matapeli wakubwa leo, hawakuanza wakiwa wezi na matapeli, walianza kidogo na kwa nia njema sana. Watu wote ambao ni walevi wakubwa (more…)

BIASHARA LEO; Jinsi Ya Kukabiliana Na Anayekuiga Kwenye Biashara.

By | February 11, 2016

Moja ya vitu ambavyo huwa nawashauri watu kwenye biashara na hata maisha ya kawaida ni kutokushindana. Ndiyo sisi binadamu tunapenda ushindani, lakini kushindana kwenye kazi, biashara na hata maisha ya kawaida huwa sio kuzuri. Sasa kama umeamua kutokushindana lakini ukaanzisha biashara kwa ubunifu wako mwenyewe na ukashangaa baada ya biashara (more…)

UKURASA WA 407; Kama Huna Muda Wa Kusoma Hapa, Soma Mara Mbili.

By | February 11, 2016

Tunaishi kwenye dunia ya mwendo kasi, kila kitu kinakwenda kwa kasi kubwa sana. Kwa mwendokasi huu tumeshapata dhana kwamba ukisubiri kidogo tu, unaachwa nyuma. Hivyo tumejikuta wote tunakimbia kimbia wakati mwingine hatuna hata uhakika tunakimbiza nini. Tunakimbia tu ili na sisi tuonekane tupo kwenye mbio. Katika kukimbia huku tumekuwa tunakosa (more…)

UKURASA WA 406; Mimi, Sisi, Nyinyi….

By | February 10, 2016

Kocha mmoja wa timu ya mpira alikuwa anapata matokeo mazuri sana kwa timu yake. Alikuwa anashinda michezo mingi na wachezaji wake walikuwa wanajituma sana uwanjani. Watu wengi walitaka kujua ni siri gani ambayo kocha yule amekuwa akiitumia na kusababisha timu yake kupata matokeo mazuri kiasi kile. Baadae iligundulika kwamba kila (more…)

ONGEA NA KOCHA; Tabia Moja Inayokuingiza Kwenye Matatizo Na Kukunyima Fursa Nyingi.

By | February 9, 2016

Habari za wakati huu rafiki? Karibu tena kwenye mazungumzo yetu haya kati yangu mimi na wewe rafiki yangu. Ni muda mrefu hatujapata nafasi ya kufanya mazungumzo haya, tangu mwaka huu uanze. Nimekuwa na mambo mengi kidogo tangu mwaka umeanza, tumefanya semina ya malengo kwa njia ya mtandao ambayo imekuwa na (more…)

UKURASA WA 405; Njia Ya Uhakika Ya Kumshawishi Mtu Yeyote Kufanya Kitu.

By | February 9, 2016

Maisha ni ushawishi, kwenye kila siku yako unahitaji kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani. Kama unafanya biashara basi unahitaji kuwashawishi wateja wanunue kile unachouza, au unahitaji kuwashawishi wanaokusaidia kuweka juhudi zaidi. Pia unahitaji kuwashawishi watu kuwekeza kwenye biashara yako. ni ushawishi kila siku na kila wakati. Kama umeajiriwa kila siku unahitaji (more…)

BIASHARA LEO; Chagua Wateja Kabla Ya Kuanza Biashara.

By | February 8, 2016

Moja ya changamoto ambayo wafanyabiashara wapya wanakutana nayo pale wanapoingia kwenye biashara, ni kukazana kwa kila kitu na hatimaye kuanza biashara, halafu wanakuta kwamba biashara haina wateja. Hii ni hali ambayo inaumiza sana hasa pale ambapo umejipanga kwa muda mrefu kuingia kwenye biashara husika. Hata kama upo kwenye biashara na (more…)