Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#SheriaYaLeo (171/366); Wafanye wengine waje kwako.

By | April 20, 2022

#SheriaYaLeo (171/366); Wafanye wengine waje kwako. Pale unapoonekana kuwahitaji sana wengine na kwenda kuwafuata, unaishia kuonekana wa kawaida na hakuna anayekuthamini. Lakini pale unapowafanya watu waje kwako, kwa kuwa siyo rahisi wewe kupatikana, unakuwa wa tofauti na unathaminika. Kwa chochote unachofanya, wafanye watu waje kwako wakiwa na uhitaji. Wafanye waje (more…)

2666; Umetingwa na yapi?

By | April 19, 2022

2666; Umetingwa na yapi? Kutingwa au kuwa bize kama wengi walivyozoea kutumia ndiyo kuna nguvu kubwa ya kuamua matokeo ambayo mtu anayapata kwenye maisha yake. Kile kinachokuweka bize ndiyo kinachozalisha matokeo kwenye maisha yako. Matokeo unayopata sasa, iwe ni mazuri au mabaya yamezalishwa na yale yaliyokutinga huko nyuma. Usilaumu watu (more…)

#SheriaYaLeo (170/366); Usifanye mabadiliko makubwa kwa wakati mmoja.

By | April 19, 2022

#SheriaYaLeo (170/366); Usifanye mabadiliko makubwa kwa wakati mmoja. Sisi binadamu huwa tunapenda kusikia kuhusu mabadiliko, ila huwa hatupo tayari kubadilika. Watu wanajua kabisa umuhimu wa mabadiliko kwenye taasisi na hata mtu mmoja mmoja. Lakini pale mabadiliko hayo yanapowahusu wao binafsi na kuathiri maslahi yao huwa hawayafurahii. Mabadiliko ni mazuri na (more…)

2665; Unahitaji watu wa kukusukuma.

By | April 18, 2022

2665; Unahitaji watu wa kukusukuma. Pamoja na magumu na changamoto mbalimbali za dunia, bado asili ya binadamu huwa ina nguvu sana. Kwa mfano, ni asili yetu binadamu kuridhika na kile ambacho tayari tumeshakipata. Pamoja na kwamba dunia inabadilika na chochote kinachoturidhisha sasa hakiwezi kuturidhisha kesho, bado hatuwezi kulivuka hilo peke (more…)

#SheriaYaLeo (169/366); Tumia mwonekano kushawishi.

By | April 18, 2022

#SheriaYaLeo (169/366); Tumia mwonekano kushawishi. Watu huwa wanashawishika sana na mwonekano wa vitu ulivyo. Vitu kama rangi, muundo na mpangilio wa vitu vina nguvu ya kuwashawishi watu kwa namna fulani. Kwa mfano matumizi ya rangi nyekundu kwenye maandishi yanawafanya watu waone kitu ni muhimu na cha haraka hivyo kushawishika kuchukua (more…)

2664; Ni wewe umewafundisha.

By | April 17, 2022

2664; Ni wewe umewafundisha. Kama watu wanakuchukulia kwa namna ambayo hupendezwi nayo, wao siyo wa kulaumu, bali wewe ndiye wa kujilaumu. Kwani kwa vyovyote vile watu wanavyokuchukulia, ni wewe umewafundisha. Wewe ndiye umewaonyesha na kuwaruhusu kwa namna gani wanaweza kukuchukulia. Kama watu wanakudharau, ni kwa sababu umewaonyesha ni sawa wao (more…)

#SheriaYaLeo; (168/366); Dhibiti machaguo unayowapa watu.

By | April 17, 2022

#SheriaYaLeo; (168/366); Dhibiti machaguo unayowapa watu. Watu huwa wanapenda kuona wana uhuru wa kuchagua mambo yao wenyewe. Lakini machaguo yanapokuwa mengi, huwa inakuwa vigumu kwa mtu kuweza kuchagua. Anajikuta njia panda na kushindwa kuchagua kitu kimoja. Ili kuwasaidia watu kufanya maamuzi na wewe kuweza kupata kile unachotaka, dhibiti machaguo unayowapa (more…)

2663; Ambacho hutumii nguvu kufanya.

By | April 16, 2022

2663; Ambacho hutumii nguvu kufanya. Watu wamekuwa wanajiuliza sana ni njia ipi rahisi ya kufanikiwa. Ni kipi ambacho wakifanya watafanikiwa. Wamekuwa wakiwaangalia wale waliofanikiwa kwenye yale wanayoyafanya na kujaribu kuyaiga. Lakini bado hawafanikiwi. Hawafanikiwi kwa sababu wanajaribu kuiga vitu vya nje, Wakati mafanikio yanatokana na vitu vya ndani. Mengi yameandikwa (more…)

#SheriaYaLeo (167/366); Tumia sanaa ya kuwepo na kutokuwepo.

By | April 16, 2022

#SheriaYaLeo (167/366); Tumia sanaa ya kuwepo na kutokuwepo. Unapaswa kujua jinsi ya kupangilia kuwepo na kutokuwepo kwako. Sisi binadamu huwa tunadharau kitu kinachopatikana muda wote na kuthamini kile ambacho hakipatikani. Kwa ujumla, ni vyema kuegemea zaidi upande wa kutokuwepo/kutokupatikana ili pale unapokuja kuonekana watu wanakuwa na shauku kubwa. Ukifanya hilo, (more…)

2662; Kama Ninge….

By | April 15, 2022

2662; Kama Ninge…. Hakuna njia rahisi ya kuyaharibu maisha yako na kujizuia kufanikiwa kama kuwa na majuto. Kuangalia yale ambayo hukufanya au hukuchagua na kuona labda ndiyo yangekuwa bora ni uhakika unachofanya sasa hakiwezi kuwa bora. Uliacha kazi na kuingia kwenye biashara, lakini mambo hayaendi kama ulivyotegemea. Unaweza kujiambia, kama (more…)