1424; Kabla Hujabadili Biashara Yako, Jua Kwanza Kiwango Chake Sahihi.

By | November 24, 2018

Shida ya wengi kwenye biashara huwa inakuja pale wanapobadili biashara zao. Mwanzoni biashara inakuwa inafanya vizuri sana, na wanaona hapa sasa wanaweza kuikuza zaidi. Ni pale wanapokuza biashara ndiyo wanakaribisha matatizo ambayo hawakuwahi kuyafikiria hapo awali. Mwingine anaweza kuwa na biashara kubwa ambayo inamsumbua, anaona suluhisho ni kuishusha chini ili (more…)

#TAFAKARI YA LEO; HATUA NDOGO KUELEKEA HATUA KUBWA…

By | November 24, 2018

“An achievement is a bondage. It obliges one to a higher achievement.” —Albert Camus Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA (more…)

1423; Kipimo Sahihi Cha Ukomavu Wa Kimaisha…

By | November 23, 2018

Wanasema nahodha mzuri hapimwi kwa utulivu wa bahari, na hili ni kweli kwenye kila eneo la maisha. Pale mambo yanapokuwa vizuri, kila mtu anaweza kufanya anachosema atafanya. Pale kila kitu kinapokwenda sawa, kila mtu anaweza kuishi kwa namna anavyopaswa kuishi. Pale ambapo hakuna misukosuko yoyote, kila mtu anaweza kuishi kwa (more…)

1422; Ni Matatizo Yao, Siyo Yako…

By | November 22, 2018

Moja ya kosa kubwa sana ambalo wafanyabiashara wengi wamekuwa wanafanya na linawagharimu, ni kufikiria zaidi matatizo yao binafsi kuliko wanavyofikiria matatizo ya wateja. Wengi hujisahau na kufikiri kwamba mteja amekuja kununua kwa sababu wao wanauza, kitu ambacho siyo sahihi. Mteja haji kununua kwako kwa sababu wewe unauza, au kwa sababu (more…)

1421; Dunia Itakulipa Kulingana Na Thamani Yako…

By | November 21, 2018

Mwandishi mmoja amewahi kuandika, dunia haikulipi kile unachostahili kulipwa, bali inakulipa kile unachokubali kulipwa. Hii ina maana kwamba, kipato ulichonacho sasa, siyo kile unachostahili kupata, bali kile ambacho umekubali dunia ikulipe. Na kama umekuwa na kipato cha aina hiyo kwa muda mrefu, hakiongezeki, basi wewe umekubaliana kabisa na dunia kwamba (more…)

#TAFAKARI YA LEO; KAWAIDA INAUMIZA…

By | November 21, 2018

Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi nyingine nzuri sana tuliyoipata leo. Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila (more…)

1420; Usikimbilie Kujitetea…

By | November 20, 2018

Watu wanapoleta malalamiko kwetu, au kutokuridhika na namna ambavyo tumewatendea, hatua ya kwanza huwa tunakimbilia kujitetea. Na katika kujitetea huko, huwa hatukosi kitu cha kuelezea au kulaumu kama sababu ya malalamiko yaliyoletwa kwetu. Lakini kukimbilia kujitetea hakuna manufaa kwa yeyote, hakumsaidii yule anayelalamika na wala hakukusaidii wewe unayelalamikiwa. Kukimbilia kujitetea (more…)