UKURASA WA 925; Hakuna Kuchelewa…

By | July 13, 2017

Umeshawahi kukutana na kitu kipya, labda maarifa au taarifa ambazo hukuzipata mapema na kusema laiti ungejua mapema ungekuwa mbali? Umeshawahi kuona kama umechelewa sana kuchukua hatua na hivyo kuona huna la kufanya? Umekuwa unajidanganya sana kwenye hilo la kuchelewa. Upo usemi wa wachina kwamba; muda bora wa kupanda mti ulikuwa (more…)

UKURASA WA 924; Malizia Kazi Pale Patamu…

By | July 12, 2017

Kama umewahi kuangalia tamthilia au maigizo yenye mwendelezo, najua unajua nini huwa kinatokea mwishoni mwa sehemu yenye mwendelezo. Huwa inakuwa ni sehemu nzuri sana, ambayo unataka kujua nini kilitokea? Halafu hapo hapo unaambia litaendelea wakati mwingine au WATCH PART 2. Unahamasika kusubiri wakati mwingine ili uone nini kilitokea, au unaenda (more…)

UKURASA WA 923; Anayekutawala Anakunyima Vitu Hivi Vitatu…

By | July 11, 2017

Kwenye hii dunia, wapo watu wengi sana ambao wanajaribu kukutawala, ili waweze kukutumia kwa madhumuni yao binafsi bila ya kujali wewe unataka nini. Na ili wafanikiwe kukutawala, wanahakikisha wanakunyang’anya au kukunyima vitu vitatu muhimu. Ukishavikosa vitu hivi tu, huna tena ujanja, lazima utakaa chini ya anayekutawala na hutakua na namna (more…)

UKURASA WA 921; Hakuna Ubaya Kwenye Kutaka Zaidi…

By | July 9, 2017

Kuna namna jamii inayotuzunguka inajaribu kuturudisha nyuma, na njia hii imekaa kisaikolojia zaidi hivyo wengi hawaioni. Njia hii ni kufanya kutaka zaidi kuonekane ni kubaya, kuonekane ni tamaa, ni roho mbaya. Kwa nini usiridhike na kidogo ulichopata! Hivi ndivyo jamii inajaribu kutuhadaa tusitake makubwa zaidi, tusipambane na tuishie kuwa kama (more…)

UKURASA WA 920; Ukweli Haumbadilishi Mtu Huyu…

By | July 8, 2017

Moja ya vitu unapaswa kuelewa kwenye maisha yako, ili uweze kuokoa muda na nguvu zako ni kwamba kuna watu hawawezi kubadilishwa, hata ungewapa ukweli kiasi gani. Wapo watu ambao watakataa au kupinga jambo, watakukataa au kukupinga kwa lolote, na huna namna unaweza kufanya kuwabadili. Hata ukiwapa ukweli, ukiwapa taarifa sahihi (more…)

UKURASA WA 919; Kama Isingekuwa Wewe…

By | July 7, 2017

Binadamu tuna tabia moja ya kushangaza sana, tukifanikiwa kufanya jambo zuri basi tunajiangalia sisi, tunaona namna gani tumejitahidi, jinsi gani tuna uwezo mkubwa, ni namna gani tuna bahati, na hata kujiambia na kuwaambia wengine kwamba tulijua tutaweza. Lakini tunaposhindwa kufanya jambo, au tunapoanguka, tunawaangalia wengine, tunaanza kuangalia nani amehusika kwenye (more…)

UKURASA WA 918; Kuwa Hapa Sasa…

By | July 6, 2017

Wakati unasoma hapa sasa hivi, mawazo yako yanafikiria wapi? Yaani unakazana kukimbilia wapi, unamaliza kusoma hapa haraka ili uende wapi au ufanye nini? Ni kawaida yetu binadamu kufanya mambo bila ya kuweka fikra na akili yetu yote kwenye jambo tunalofanya. Tunafanya kama tunapita, tukikimbilia kwenye jambo jingine. Lakini ukikaa chini (more…)

UKURASA WA 917; Tumia Njia Hii Kujijengea Nidhamu Binafsi…

By | July 5, 2017

Nidhamu binafsi ndiyo msingi mkuu wa mafanikio kwenye kila eneo la maisha yetu. Iwe ni kwenye afya, mahusiano, fedha, kazi na hata biashara. Bila nidhamu binafsi, huwezi kufika viwango vya juu vya mafanikio, kwa sababu changamoto ni nyingi na hata usumbufu pia ni mwingi. Watu wote waliofanikiwa, wana nidhamu binafsi (more…)