UKURASA WA 916; Usiitabiri Kesho Yako, Bali Itengeneze…

By | July 4, 2017

Katika kitu kimoja ambacho tunaongoza kwa kushindwa, ni utabiri. Sisi binadamu siyo wazuri kwenye utabiri wa aina yoyote ile. Hakuna mtu ambaye ameweza kuwa na utabiri wa uhakika wa asilimia 100. Mara nyingi wanaotabiri na ikatokea, inakuwa ni bahati pekee na wala siyo uhakika. Pamoja na ubovu wetu huu kwenye (more…)

UKURASA WA 915; Hivi Ndivyo Unavyotengeneza Siku Mbaya Kwako…

By | July 3, 2017

Unajiambia kwamba una siku mbaya, hivyo tu, wala hakuna muujiza. Unapoianza siku, labda kwa changamoto fulani, kisha ukajiambia siku yangu imeshakuwa mbaya, basi utabiri wako lazima utimie. Siku hiyo lazima itakuwa mbaya sana, hata ufanye nini. Hii inatokana na ukweli kwamba kuanzia wakati huo, kila jambo utakalokutana nalo, utaona ubaya (more…)

UKURASA WA 914; Wakati Sahihi Wa Kuondoka….

By | July 2, 2017

Kwenye kila jambo tunalofanya kwenye maisha yetu, kuna wakati tunapaswa kuondoka. Kuondoka ama moja kwa moja na kwenda kufanya mambo mengine, au kuondoka kwa kubadilika na kufanya kwa njia mpya na viwango vipya. Lakini wengi wamekuwa hawajui upi wakati sahihi wa kuondoka, na hivyo kujikuta kwenye changamoto ambazo zinawarudisha nyuma, (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; NJIA YA MKATO, UTAISHIA NA MIKATO….

By | July 1, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwends kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Ni kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutakwenda kuweka juhudi kubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu NJIA (more…)

UKURASA WA 913; Vikwazo Vya Wengine, Ni Fursa Nzuri Kwako…

By | July 1, 2017

Watu wanasema, moja ya kazi kubwa ambayo kila mtu anayo hapa duniani, ni kuweza kuishi na wengine. Changamoto nyingi tunazokutana nazo kwenye maisha, zinahusisha watu wengine. Kuna wakati unaweza kuona kabisa kama wengine ndiyo wamekuweka hapo ulipo sasa, wanakuzuia usipige hatua. Labda ni mwajiriwa mwenzako ambaye amekuwa kikwazo kwako kwenye (more…)

UKURASA WA 912; Nunua Muda Kwanza….

By | June 30, 2017

Wazungu wanasema buy some time… Kuna wakati unajikuta kwenye hali ngumu, ambapo hujui ni maamuzi gani sahihi kufanya. Katika hali hiyo unakuwa huna taarifa za kutosha, na maamuzi yoyote ya haraka unayoweza kuchukua, yanaweza kuharibu mambo zaidi, kuliko kuyatengeneza. Huu ndiyo wakati ambao unapaswa kununua muda kwanza, kuacha muda upite (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; UJASIRI NA UTHUBUTU….

By | June 29, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili tuweze kupata matokeo bora kabisa. Ni kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari kuhusu UJASIRI NA UTHUBUTU… (more…)

UKURASA WA 911; Maamuzi Ya Mtu Mmoja….

By | June 29, 2017

Kama maamuzi ya mtu mmoja yanaweza kuharibu na kuvuruga kabisa maisha yako, nina habari mbaya kwako, huna maisha. Huo ndiyo ukweli, japo unaweza usiupende, kwa sababu ukweli huwa unaumizwa. Unapaswa kutengeneza maisha ambayo yanaweza kujiendesha vizuri, changamoto zipo na vikwazo vipo, lakini maamuzi ya mtu mmoja yanapokuwa na athari kubwa (more…)

BIASHARA LEO; Usikimbilie Kufanya Vitu Rahisi, Vitakupoteza Kibiashara…

By | June 28, 2017

Biashara ni ngumu, hilo halina ubishi, lakini ugumu mwingine tumekuwa tunautengeneza sisi wenyewe. Hasa pale ambapo tunakuwa tunatafuta njia rahisi ya kufanikiwa kwenye biashara. Kwa kuwa kufikiri ni kazi ngumu, na kwa kuwa njia bora za kuifanikisha biashara yako kutakuhitaji ufikiri, watu wanakwepa hilo. Na badala yake wanaangalia kipi rahisi (more…)