UKURASA WA 493; Sifa Kuu Ya Uongozi Unayotakiwa Kuwa Nayo…

By | May 9, 2016

Tofauti ya uongozi na usimamizi ni kwamba kwenye uongozi watu wanachagua kukufuata, wanachagua kufanya kile ambacho unawashawishi wafanye. Kwenye usimamizi ni watu wanalazimika kukufuata, hawana namna ila lazima wafanye kile unachowataka wafanye. Bila ya shaka uongozi unakufikisha mbali kuliko usimamizi. Maana watu wanapochagua wao wenyewe wanajitoa kuliko unapowalazimisha. Sasa kuna (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Dhibiti Fikra Zako, Njia Ya Kupata Uhuru Wa Uhakika.

By | May 8, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Karibu tena kwenye kipengele chetu cha FALSAFA MPYA YA MAISHA ambapo kwa pamoja tunatengeneza falsafa itakayofanya maisha yetu kuwa bora zaidi. Leo tunakwenda kuangalia njia ya uhakika ya kuwa na uhuru na maisha yetu. Kitu muhimu sana tunachotaka kwenye maisha yetu, ili tuweze kuyafurahia na (more…)

UKURASA WA 492; Tatizo Siyo Fursa…

By | May 8, 2016

Tunaishi kwenye dunia ambayo mtu aliyekufa miaka 100 iliyopita, akifufuka leo ataona kila kitu ni kigeni. Maana miaka 100 iliyopita hakukuwa na kompyuta, simu za mkononi, mtandao wa intaneti, tv, redio na vingine vingi ambavyo kwa sasa tunavichukulia kama vitu vya kawaida. Mtu huyu akifufuka leo atashindwa kabisa kuamini kama (more…)

UKURASA WA 491; Ulichonacho Na Usichokuwa Nacho…

By | May 7, 2016

Tunapokuwa wenyewe na kupata nafasi ya kufikiria maisha yetu, huwa tunafikiria vile vitu ambavyo tunavitaka lakini bado hatujavitapa. Tunafikiria kwa kina jinsi gani maisha yetu yatakuwa bora kama tutapata vitu hivyo ambavyo hatuna. Lakini tunasahau ya kwamba kuna vitu ambavyo tunavyo sasa, ambavyo tunavichukulia kwa ukawaida, lakini kama vikiondoka tutavikosa (more…)

BIASHARA LEO; Fursa Ipo Ndani Yako, Na Jinsi Ya Kuitumia.

By | May 4, 2016

Dunia imekuwa inatudanganya kitu kimoja, ya kwamba fursa zipo nje yetu na hivyo ni sisi kuhakikisha tunazitafuta na kuzitumia. Ukweli ni kwamba fursa hazipo nje yetu bali zipo ndani yetu. Tunapozijua fursa zilizopo ndani yetu,mkitu chochote kinachotuzunguka kinakuwa fursa kubwa kwetu. Tutaweza kukitumia na kuweza kufanya mambo makubwa. Lakini kama (more…)

UCHAMBUZI WA KITABU; The Essentials Of Business Etiquette. (Tabia Muhimu Za Kuzingatia Kwenye Mahusiano Ya Kibiashara)

By | May 4, 2016

Tabia zetu zina athari kwenye biashara au kazi tunazofanya. Kuna baadhi ya mambo tunaweza kuwa tunafanya na yakawa yanaharibu sana sifa zetu kwenye biashara na hata kazi. Mwandishi na mshauri Barbara Pachter anatushirikisha tabia za kuzingatia kwenye maeneo yetu ya kazi na hata biashara katika kitabu chake The Essentials Of (more…)

UKURASA WA 489; Tuzo Na Adhabu…

By | May 4, 2016

Tangu zamani kumekuwa na njia kuu mbili za kutengeneza au kurekebisha tabia. Njia hizi ni za kisaikolojia na zimekuwa zinaleta majibu mazuri lakini pia zisipotumiwa vizuri zinaleta majibu mabaya. Njia hizo mbili ni Tuzo/zawadi na Adhabu. Tuzo/zawadi; Hapa mtu anatuzwa au kupewa zawadi kwa kitu kizuri alichokifanya. Mtu anatambuliwa kwa (more…)

UKURASA WA 488; Nani Anakuamini?

By | May 3, 2016

Kuna vitu vingi sana unavyotakiwa kujali kwenye maisha haya, vitu ambavyo vinatakiwa kukuumiza kichwa kuhusu shughuli unazofanya na maisha kwa ujumla. Lakini kuna kitu kimoja unatakiwa kujali zaidi, kuna kitu kimoja ambacho kinatakiwa kukuumiza zaidi kuliko vitu vingine. Kitu hiko ni wanaokuamini. Anza na swali ni nani anayekuamini? Ni watu (more…)

Tabia Tano (5) unazohitaji ili kuwa muuzaji bora.

By | May 2, 2016

Biashara haijakamilika kama mtu hajanunua kitu. Mambo yote unayofanya kwenye biashara yako ni kwa ajili ya kukamilisha kitu hiki muhimu sana, ambacho ni kumuuzia mteja wako kile ambacho unauza. Pale mteja anaporidhika na kutoa fedha yake ili apate bidhaa au huduma unayotoa ndio biashara inakuwa imekamilika. Katika maeneo mengi muhimu (more…)