UKURASA WA 378; Njia Ya Kweli Ni Moja, Njia Za Uongo Ni Nyingi.

By | January 13, 2016

Nilipokuwa nasoma sekondari, nilikuwa napenda sana somo la hesabu. Usijali kama ulikuwa hulipendi, leo nitakuelekeza kidogo sana, ili tuweze kwenda pamoja. Wakati tupo kidato cha pili, mwalimu wetu wa hesabu alikuwa akitoa mitihani, alikuwa ana mtindo tofauti wa kusahihisha. Kwa somo la hesabu lilivyo, njia unayotumia kufikia jibu lako ina (more…)

KURASA ZA MAISHA; Mtazamo Mpya Wa Maisha Ya Furaha Na Mafanikio.

By | January 12, 2016

KURASA ZA MAISHA; Mtazamo Mpya Wa Maisha Ya Furaha Na Mafanikio. Habari za leo rafiki? Naamini uko vizuri sana na unaendelea na harakati zako z akuboresha maisha yako zaidi. Najua mwaka 2016 ndio unaanza kukolea na nina hakika bado una ule moto wa malengo ambayo umejiwekea kwa mwaka huu 2016. (more…)

UKURASA WA 377; Kitu Kimoja Ambacho Huwezi Kukibadili, Hata Ufanye Nini.

By | January 12, 2016

Katika maisha yako, kuna maeneo ambayo una nguvu ya kufanya kitu au kuleta mabadiliko, na kuna maeneo ambayo huna nguvu kabisa. Kama jinsi ambavyo tunajua, maana tumekuwa tunajifunza sana hapa, hasa kupitia FALSAFA MPYA YA MAISHA, kila kinachotokea kwenye maisha yako kina kisababishi. Hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, kila (more…)

UKURASA WA 376; Acha Kujificha…

By | January 11, 2016

Ni asili ya binadamu kujificha pale anapokutana na jambo ambalo anaona haliwezi, au linamzidi, au hayupo tayari kuweka juhudi kubwa kwenye jambo hilo. Na kwa sababu hataki kuonekana na wengine kwamba jambo lile hawezi, au haweki juhudi, basi mtu hujificha. Unapoona unahitajika kuchukua hatua kubwa kwenye biashara yako na wewe (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Mchango Wa Falsafa Kwenye Ukuaji Wako Wa Kiroho.

By | January 10, 2016

Heri ya mwaka mpya mwana falsafa mwenzangu. Ni siku nyingi hatujakuwa pamoja hapa kwenye falsafa. Hii ni kwa sababu mwishoni mwa mwaka nilikuwa kwenye likizo ya wiki moja na wiki ya kwanza kabisa ya mwaka huu nilikuwa naandaa semina ya mwaka 2016 ambayo inaendelea kwa njia ya mtandao. Kama umepata (more…)

UKURASA WA 375; Fikra Potofu Kuhusu Mafanikio…

By | January 10, 2016

Kipindi cha nyuma, na hata sasa kwa kiasi fulani, watu wamekuwa wanaamini kwamba mafanikio na wema haviwezi kuwa pamoja. Ni labda uchague kuwa mwema au uchague kuwa na mafanikio. Na hivyo fikra za aina hii ziliwaweka watu wema njia panda na kuyaogopa kabisa mafanikio kwa sababu waliaminishwa kupata mafanikio kungeharibu (more…)

UKURASA WA 374; Hiki Unachotaka Hakijawahi Kutokea Kabisa Duniani….

By | January 9, 2016

Moja ya vitu ambavyo wewe kama rafiki yangu nakusihi sana uache ni kujidanganya. Ndiyo umekuwa unajidanganya sana, huenda unajidanganya ukijua au mara nyingi unakuwa hujui, ila umekuwa unajidanganya sana. Na hilo limekuwa linakugharimu kwa kiasi kikubwa sana, na kukuzuia kufikia mafanikio. Kuna mambo ambayo umekuwa unataka na kuamini unatakiwa kuyapata (more…)

UKURASA WA 373; Usiingilie Kazi Za Watu….

By | January 8, 2016

Wazungu wanasema MIND YOUR OWN BUSINESS, yaani jali shughuli zako mwenyewe. Lakini wengi tumekuwa tunajali sana kuhusu shughuli za wengine, hasa pale ambapo tunahisi zinahusiana na sisi. Na tumekuwa tunaingilia kazi za wengine, na hili limekuwa linaturudisha nyuma sana. Mfano wa kazi za wengine ambazo tumekuwa tunaingilia; Kuna watu wanaitwa (more…)

UKURASA WA 372; Kubali Kutokuwa Mzuri Mpaka Utakapokuwa Mzuri.

By | January 7, 2016

Mfanyabiashara mkubwa unayemuona leo, hakuanzia hapo, alianza chini kabisa, kwa kupata hasara lakini leo unamwona ana biashara kubwa. Mwanamuziki mashuhuri unayemuona leo, hakuanzia hapo alipo, alianza chini kabisa, nyimbo zake za kwanza watu hawakuzisikiliza. Mwandishi mashuhuri unayemuona leo hakuanzia hapo, ukipewa andiko lake la kwanza usome unaweza kuona ni mtu (more…)

UKURASA WA 371; Kufanikiwa Sio Kwa Ajili Yako Tu, Kuna Hawa Watanufaika Pia.

By | January 6, 2016

Kuna baadhi ya watu ambao kutokana na maisha waliyopitia wanaamini kufanikiwa sio muhimu kwenye maisha. Na hii pia inaathiriwa na maana ambayo wao wenyewe wameiweka kwenye mafanikio. Naomba tukumbushane jambo moja muhimu, kufanikiwa ni jambo muhimu sana kwenye maisha yako, nasema tena ni jambo muhimu. Haijalishi maana ya mafanikio ni (more…)