UKURASA WA 243; Baada Ya Kufanya Kazi Iliyo Bora Sana.

By | August 31, 2015

Baada ya kufanya kazi iliyo bora sana kwa uwezo ulionao. Baada ya kutoa huduma iliyo bora sana kwa wateja wako. Baada ya kuandika makala/kitabu kilicho bora sana kwa uwezo wako. Baada ya kuweka kila ulichonacho kwenye kitu ambacho unafanya. Na bado watu wasione kama umefanya kitu kikubwa. Unahitaji kuendelea kufanya (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Huwezi Kuidanganya Dunia, Acha Kujidanganya.

By | August 30, 2015

Karibu sana rafiki tuendelee kujijengea falsafa mpya ya maisha ambayo tutaishi nayo maisha yetu yote. Falsafa hii itafuata misingi yote ya dunia na hivyo kutuweka kwenye nafasi nzuri sana ya kushinda. Moja ya vitu ambavyo watu wengi tumekuwa tunajidanganya ni kufikiri kwamba sisi tunaweza kuwa wajanja kuliko dunia yenyewe. Huwa (more…)

UKURASA WA 242; Pokea Na Tumia Zawadi Hii Vizuri.

By | August 30, 2015

Kila siku mpya inapoanza, kuna zawadi kubwa na nzuri sana ambayo kila mmoja wetu anapewa. Zawadi hii ina thamani kuliko kitu chochote kuwahi kutokea kwenye maisha yetu. Zawadi hii tunapewa kwa usawa wote hapa duniani na hakuna anayepunjwa au kusimangwa. Pamoja na zawadi hii kuwa kubwa, ya muhimu na ya (more…)

UKURASA WA 241; Ukweli Utabaki Kuwa Ukweli.

By | August 29, 2015

Mara nyingi watu huwa hawapendi kuujua ukweli kwa sababu ukweli unauma. Hasa pale ambapo ukweli huo unakuwa unahusu mapungufu ya mtu moja kwa moja. Haijalishi hutaki kuusikia ukweli kwa kiasi gani, lakini hili halitabadili ukweli. Ni bora ukabadili mtazamo wako kuhusu kupokea ukweli na hili litakusaidia sana. Njia moja muhimu (more…)

UKURASA WA 240; Sababu Nzuri Na Sababu Halisi.

By | August 28, 2015

Mtu yeyote anapofanya au anaposhindwa kufanya jambo, anakuwa na sababu mbili. Sababu ya kwanza ni sababu nzuri ya kwa nini amefanya au ameshindwa kufanya. Hii ni sababu nzuri kwa maana kwamba ndio atakayotumia kuwaambia wengine kuhusu kile alichofanya au alichoshindwa kufanya. Sababu ya pili ni sababu halisi. Hii ndio ile (more…)

Naanza Kujifunza Lugha Ya Kilatini Na Kwa Nini Nafanya Hivyo.

By | August 27, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Naamini uko vizuri sana, na najua unafanyia kazi yale ambayo unajifunza ili maisha yako yaweze kuwa bora sana. Hongera sana kwa hilo, na ninakusihi sana usifike mahali na kuona kwamba haiwezekani halafu ukarudi kwenye yale maisha ya zamani. Kama umechagua maisha mapya hakikisha unaendelea nayo (more…)

UKURASA WA 239; Tegemea Makubwa Na Usitegemee Chochote.

By | August 27, 2015

Inapokuja kwenye mipango yako ya maisha, tegemea mambo makubwa sana. Tegemea kufanya mambo makubwa ambayo yatabadili kabisa maisha yako. Tegemea kazi yako kuwa bora sana kiasi kwamba itaongeza thamani na kipato chako kitaongezeka pia. Tegemea kuwa na biashara kubwa ambayo itawasaidia watu wengi kutatua matatizo yao. Vitu hivi viko ndani (more…)

UKURASA WA 238; Unaona Nini?

By | August 26, 2015

Unapoyafikiria maisha yako, kuna picha ambayo unaiona. Unapofikiria siku zinazokuja, kwenye kazi yako, biashara yako na hata maisha yako kwa ujumla, kuna taswira ambayo huwa inakujia kwenye akili yako. Mara nyingi taswira hii huwa ni hasi, kujiona umefukuzwa kazi, au kazi inazidi kuwa ngumu na huku kipato hakitoshelezi. Au kujiona (more…)

Usidharau Ushindi Mdogo Mdogo Unaoupata Kila Siku, Ni Muhimu Kwa Mafanikio Yako.

By | August 25, 2015

Habari za wakati huu rafiki? Naamini uko vizuri sana, hongera kwa hilo. Na hata kama haupo vizuri usiwe na shaka, mambo yatakwenda vizuri. Kikubwa ni wewe uendelee kufanya yale ambayo umepanga kufanya. Kabla hatujaingia kwenye mazungumzo yetu ya leo naomba kuna mambo mawili muhimu ya kukuambia; Kwanza nashukuru sana wewe (more…)

UKURASA WA 237; Siku Sio Nyingi….

By | August 25, 2015

Siku sio nyingi wanaokuambia kwamba huwezi wataachana na wewe na kuendelea na maisha yao, au kutafuta mtu mwingine wa kumwambia hivyo. Siku sio nyingi wanaokunyooshea kidole watachoka na kuendelea na mambo yao mengine. Siku sio nyingi wanaokuambia utajuta kwa maamuzi uliyofanya watachoka kuendelea kukuambia hivyo na watatafuta mambo mengine ya (more…)