Matatizo yote kwenye biashara yanaanza na kitu hiki kimoja.

By | August 24, 2015

Wewe kama mfanyabiashara, kipato unachopata kinatokana na fedha ambazo mteja analipa. Gharama zote za kuendesha maisha yako zinazotokana na biashara ni kwa sababu kuna mteja ambaye ametoa fedha zake ili kupata huduma au bidhaa unazotoa. Kwa kifupi tunaweza kusema kwamba bosi hasa wa biashara yako ni mteja wako. Hii ni (more…)

UKURASA WA 236; Changamoto Mbili Kubwa Utakazokutana Nazo Wakati Wa Mabadiliko.

By | August 24, 2015

Kama unafanya kazi yoyote kubwa inayochochea mabadiliko kwa wengine, hongera sana. Ni kazi nzuri lakini ni ngumu na hivyo inahitaji moyo sana, vinginevyo ni rahisi sana kukata tamaa. Kama tunavyokubaliana, kwanza huwezi kumbadili mtu yeyote, watu hawapendi kubadilishwa, bali wanabadilika wenyewe. Hivyo lengo lako wewe sio kuwalazimisha watu wabadilike, ila (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kwa Nini Falsafa Mpya?

By | August 23, 2015

Habari za leo mpenzi msomaji? Karibu kwenye mfululizo huu wa makala za FALSAFA MPYA YA MAISHA. Kupitia makala hizi utapata kujifunza na kujijengea falsafa ya maisha yako ambayo itakuwezesha wewe kuwa na maisha ya furaha na yenye mafanikio. Lakini kabla hatujaingia ndani na kujifunza kutengeneza falsafa ambayo tutaishi nayo, ni (more…)

UKURASA WA 235; Acha Kukimbiza Fursa Mpya Kila Wakati.

By | August 23, 2015

Kama lengo lako litakuwa kukimbiza fursa mpya kila wakati, basi maisha yako yatakuwa ya mbio tu. Fursa mpya zipo na zinaendelea kuibuka kila wakati. Huwezi kuwa unarukia kila kitu kipya kinachokuja, utafanya hivyo mpaka lini? Ni kweli kunaweza kuwa kunakuja fursa nzuri sana. Kunaweza kuwa kunakuja fursa za kipekee ambazo (more…)

MAMBO 20 NILIYOJIFUNZA KWENYE KITABU 100 WAYS TO MOTIVATE OTHERS.

By | August 22, 2015

Kitabu 100 WAYS TO MOTIVATE OTHERS ni kitabu kinachokupa maarifa ya kuweza kuwahamasisha wengine ili kuweza kua na kufabya zaidi. Kumbuka kwamba mafanikio yako kwenye kazi na hata maisha yanategemea ni jinsi gani unaweza kuwahamasisha wengine ili waweze kutimiza majukumu yao. Hapa kuna mambo 20 nitakayokushirikisha kutoka kwenye kitabu hiki. (more…)

UKURASA WA 234; Maisha Ni Kujumlisha Na Kutoa.

By | August 22, 2015

Kama ambavyo tumekuwa tunakubaliana mara nyingi, maisha ni kichagua. Chochote kinachotokea kwenye maisha yako, basi umechagua mwenyewe, iwe ni sasa au siku zilizopita. Sasa mambo yote unayoweza kuchagua kwenye maisha yamegawanyika kwenye makundi mawili. Makundi haya ni kujumlisha(chanya, +) na kutoa(hasi-). Ukifanya jambo lolote ambalo ni chanya unajumlisha(kuongeza) kitu kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Wauzie Wanaoijua Thamani Unayotoa.

By | August 21, 2015

Moja ya njia unazotumia kupoteza muda na rasilimali nyingine kwenye biashara yako, ni kujaribu kumuuzia kila mtu kile unachouza. Ni vigumu sana kila mtu kuona thamani ya ile biashara ambayo unafanya. Hivyo katika harakati zako za kutafuta wateja utakutana na watu wengi. Kuna ambao wataiona thamani na kuchukua hatua haraka, (more…)

UKURASA WA 233; Ni Vikwazo Gani Unaendelea Kujiwekea Kwenye Maisha Yako.

By | August 21, 2015

Sehemu kubwa sana ya vikwazo vinavyokuzuia wewe kuishi yale maisha unayotaka vinatoka ndani yako mwenyewe. Hakuna mtu mwingine anayevisababisha ila wewe mwenyewe. Umekuwa unapanga vizuri kabisa ya kwamba utafanya kitu fulani, lakini unakuja na lakini ambazo unaweza kujishawishi vizuri sana. Unajishawishi ya kwamba kwa sasa hutaweza kwa sababu fulani na (more…)

UKURASA WA 232; Unachofanya Sasa Ndio Utaendelea Kufanya.

By | August 20, 2015

Watu wengi hukubali kwamba maisha yao yanahitaji mabadiliko…. Ndio inabidi nibadili jinsi ninavyofanya kazi zangu… Inabidi nibadili jinsi ninavyofanya biashara zangu…. Inabidi nianze kuweka akiba na kuwekeza kwa ajili ya baadae…. Inabidi niache kupoteza muda kwa kuzurura kwenye mitandao na hata kufuatilia habari zisizo na msingi… Lakini….. Lakini kwa sasa (more…)

Huoni Fursa Za Mafanikio Kwa Sababu Hii Kubwa.

By | August 19, 2015

Tunaona kile ambacho tunataka kuona, kile ambacho kimejaa kwenye akili zetu na mawazo yetu. Kama akili yako na mawazo yako yamejaa habari za kushindwa basi kila utakachokiangalia utaona kushindwa. Ukiwa na mawazo ya mafanikio kila utakachoangalia utaona mafanikio. Tatizo sio kile unachoangalia, bali tafsiri ambayo tayari unayo kwenye mawazo yako. (more…)