UKURASA WA 223; Hatua Moja Ndogo Kila Siku Ndio Kitu Pekee Unahitaji.

By | August 11, 2015

Watu huwa wanalalamika kwamba kuleta mabadiliko kwenye maisha yao ni vigumu sana. Lakini sio kweli. Sio kwamba ni vigumu kuleta mabadiliko, ila mpango wetu wa mabadiliko ndio unakuwa mgumu. Kwa mfano mtu anapanga kubadili milo yake ili awe na afya bora. Anaanza kula vizuri leo halafu anategemea kesho awe na (more…)

Zingatia haya kuendesha biashara yenye mafanikio.

By | August 10, 2015

Kama kuna kitu muhimu kwa kila mfanyabiashara, basi ni muda. Kuna wakati unatamani siku ingekuwa na masaa mawili au matatu ya ziada ili uweze kukamilisha majukumu yako ya kibiashara. Katika wakati huu unakuta umeacha kuimiliki biashara na biashara inaanza kukumiliki wewe. Hii ni hali ya hatari sana kwenye maisha yako (more…)

UKURASA WA 222; Unaweza Kutoa Majibu Au Unaweza Kutoa Sababu.

By | August 10, 2015

Unaweza kutoa majibu au unaweza kutoa sababu, lakini sio vyote kwa pamoja, na pia havina uzito sawa. Watu wengi tunapenda kutoa sababu, kwa sababu tunajua tukiwa na sababu tutasamehewa kwa kile ambacho tumeshindwa kufanya. Hivyo wakati unafanya kitu, tayari unatengeneza na sababu, kama itatokea ukashindwa. Tayari unakuwa na sababu ya (more…)

UKURASA WA 221; Kilichokufikisha Hapa, Hakitakupeleka Mbele.

By | August 9, 2015

Moja ya changamoto kubwa ambazo zinawazuia watu wengi kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yao ni wao kujiwekea kikomo. Ndio, karibu kila mtu anapenda kuwa na maisha bora, lakini kuna wakati unafika mtu anajiwekea kikomo mwenyewe. Na baada ya kujiwekea kikomo hiki hakuna tena jitihada kubwa zinazofanyika kujiondoa pale ambapo mtu (more…)

UKURASA WA 220; Punguza Nafasi Za Watu Kukuumiza Kwa Kufanya Hivi.

By | August 8, 2015

Sikutegemea kabisa kama angeweza kunifanyia hivi… Siku hizi amebadilika sana… Huyu ni msaliti…. Ni baadhi ya kauli ambazo watu hutumia baada ya kuumizwa na maamuzi ya watu wengine. Unaweza kutumia kauli hizo na nyingine kama hizo kujiridhisha kwamba ni kweli umeumizwa lakini hazina msaada wote kwako. Hata iwe umeumizwa kiasi (more…)

Unategemea Ulipwe Kwa Muda? Hiyo ilikuwa Mwaka 47, Amka.

By | August 7, 2015

Hakuna atakayekulipa kwa sababu tu umekuwa kwenye kazi muda mrefu au kwa sababu unaonekana unafanya kazi muda mrefu. Utalipwa kulingana na thamani unayozalisha. Ukilazisha thamani kubwa unapata malipo makubwa. Kama unazalisha thamani ndogo, au huzalishi kabisa thamani, unategemea nini? Leta mabadiliko leo, fanya kitu kwa utofauti na hakikisha unaongeza thamani. (more…)

UKURASA WA 219; Usiianze Siku Yako Bila Ya Kufanya Kitu Hiki Muhimu.

By | August 7, 2015

Kama kuna njia rahisi kabisa ya kuipoteza siku yako ni kuianza bila ya kufanya kitu hiki kimoja ambacho ni muhimu sana kwako na kwa maisha yako. Ni kitu ambacho kitakuwezesha wewe kufika kule unakotaka wakati wengine wanaendelea kuhangaika na maisha na wasijue wanaenda wapi. Kabla sijakuambia kitu hiki muhimu naomba (more…)

Usilalamike, Dunia Imekupa Kila Kitu, Ni Wewe Tu…

By | August 6, 2015

Dunia imeshakupa kila kitu ambacho wewe unataka. Kama unabisha angalia ni watu wangapi ambao wameanzia pabaya kuliko wewe lakini wameweza kufika mbali. Sasa na wewe unawezaje kufika mbali zaidi ya ulipo sasa? Acha kulalamika kwamba dunia haina usawa, Acha kulalamika kwamba kuna wengine wanapendelewa, Amua ni kitu gani unachotaka kwenye (more…)

Kama Unayapigania Mafanikio, Watu Watakuchukia, Usiumizwe na Hilo.

By | August 5, 2015

Wakati wewe unakazana kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio, kuna watu watakuchukia bila sababu yoyote ile. Wakati wao wanapoteza muda na wewe ukaacha kupoteza nao muda, watakuchukia. Wakati wao wanafanya matumizi makubwa kuliko vipato vyao na wewe ukakwepa hilo, watakuchukia. Wakati wao wanafanya kazi kwa kawaida tu na hawamalizi mpaka (more…)