UKURASA WA 231; Njia Kuu Mbili Za Kushinda.

By | August 19, 2015

Kuna njia kuu mbili za kushinda, njia zote ni muhimu sana kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa. Lakini cha kushangaza watu wengi wanajua njia moja pekee. Njia ya pili hawaijui, japo ndio njia muhimu kuliko ile inayojulikana na wengi. Njia ya kwanza ya kushinda ni kushinda. Ndio, ulipanga kufanya kitu fulani (more…)

Siku Mpya Ni Mbegu Mpya, Unaipanda Wapi?

By | August 18, 2015

Kila siku mpya ni mbegu mpya ambayo kama ukiweza kuipanda vizuri utakuwa na mavuno mazuri sana baadae. Usikubali siku yako iishe kama vile ambavyo wengine wanafanya. Wewe ichukulie siku yako kuwa ya kipekee, Ione kama nafasi ya kuionesha dunia ubora ambao uko ndani yako, ubora ambao dunia haijawahi kuuona. Na (more…)

UKURASA WA 230; Kipimo Cha Kujua Kama Kweli Unafanya Kile Ulichokusudiwa Kufanya.

By | August 18, 2015

Kila mmoja wetu kuna vitu amekusudiwa kufanya hapa duniani. Tuna uwezo na vipaji tofauti tofauti na hivyo kuweza kufanya vitu tofauti. Mafanikio makubwa yanakuja pale mtu anapofanya kile ambacho amekusudiwa kufanya, kile ambacho kinaendana na uwezo wake na hata vipaji vyake. Lakini kwa bahati mbaya sana, huwa hatuzaliwi na karatasi (more…)

Kama mteja ataacha kufanya biashara na wewe, ataenda wapi?

By | August 17, 2015

Ni rahisi sana kutabiri kama biashara yako itafanikiwa au haitafanikiwa. Japo watu wengi huwa hawachukui hatua hii muhimu. Kwenye biashara yako, kwa bidhaa au huduma unayotoa, wewe mwenyewe kwenye moyo wako unaweza kuwa unajua kama unatoa thamani kweli au hutoi thamani. Leo tutajadili swali moja muhimu sana unalotakiwa kujiuliza kila (more…)

UKURASA WA 229; Ukiwa Unakula Chakula Kitamu, Hujali Serikali Inafanya Nini.

By | August 17, 2015

Moja ya vitu vikubwa ambavyo huwa nawashauri watu wanaotaka kubadili maisha yao ni kuanza na zoezi hili la siku kumi. Zoezi lenyewe linakutaka wewe usilalamike kwa chochote kile kwa siku kumi mfululizo, na kama ikitokea umelalamika basi unaanza tena(ni zoezi zuri sana, kama hujalifanya bado bonyeza maandishi haya kulisoma). Sasa (more…)

UKURASA WA 228; Kusamehe Tu Haitoshi, Achilia.

By | August 16, 2015

Katika maisha yetu ya kila siku, kuna watu tunawakosea, kuna watu wanatukosea na pia tunajikosea wenyewe. Kwa vyovyote vile mambo haya matatu yanatuacha sisi na hisia za hasira. Kwa nini huyu mtu anifanyie hivi, kwa nini nimeshindwa kufanya kitu hiki au kwa nini nimemfanyia mtu kitu kama hiki. Hasira hizi (more…)

UKURASA WA 226; Akiondoka Kwako Atakwenda Kwa Nani?

By | August 14, 2015

Swali muhimu sana kujiuliza kama hutaki kumpoteza mtu ambaye ni muhimu kwako. Kama wewe ni mfanyabiashara jiulize swali hili kila siku. Je kama mteja uliyenaye sasa ataamua kuacha kufanya biashara na wewe, je atakwenda kwa mfanyabiashara mwenye sifa gani? Kama hutaki kumpoteza mteja huyo basi tengeneza sifa hizo atakazozifuata. Kama (more…)

UKURASA WA 225; Nikipata Muda Nitafanya.

By | August 13, 2015

Mtu akishatoa sababu kama hiyo jua kabisa hayupo tayari kwa ajili ya mafanikio. Kwamba mtu akipata muda atafanya kitu ambacho ni muhimu kwake. Labda pia kitu hiko sio muhimu. Ukweli ni kwamba hakuna mtu ambaye atapata muda zaidi ya alionao sasa. Hakuna mtu anayeweza kutengeneza muda. Tutaendelea kuwa na haya (more…)