NENO LA LEO; Maana Halisi Ya Vikwazo.

By | December 4, 2014

Obstacles are those frightful things you see when you take your eyes off the goal. –Henry Ford Vikwazo ni yale mambo ya kutisha unayoyaona pale unapoondoa macho yako kwenye malengo yako makubwa. Ukishaweka malengo na mipango yako usiangalie tena pembeni, utaona mambo mengi ambayo yatakukatisha tamaa. Nakutakia siku njema. (more…)

Dakika 20 Kwa Siku Zinakutosha Kuwa Bora Duniani(WORLD CLASS)

By | December 3, 2014

Moja ya mahitaji makubwa ya kila binadamu ni kukubalika kwa kile anachofanya. Tuna njaa kubwa sana ya kuona watu wakitukubali kutokana na mambo tunayofanya. Unapenda watu wakuone wewe ni mfanyakazi bora au kiongozi bora au mfanyabiashara bora. Pamoja na watu wengi kupenda kukubalika kwa kile wanachofanya bado ni wachache sana (more…)

NENO LA LEO; Njia Moja Ya Uhakika Ya Kuepuka Kupingwa.

By | December 3, 2014

There is only one way to avoid criticism: do nothing, say nothing, and be nothing. –Aristotle Kuna njia moja pekee ya kuepuka kupingwa; usifanye chochote, usiseme chochote na usiwe chochote. Vinginevyo chochote utakachofanya lazima kuna mtu atakupinga au kukukosoa. Fanya kile unachoona ni sahihi kufanya na komaa nacho mapaka ufikie (more…)

TABIA ZA MAFANIKIO; Jinsi Ya Kuondoa Tabia Ya Kuahirisha Mambo.

By | December 2, 2014

Karibu tena msomaji wa KISIMA CHA MAARIFA katika kipengele hiki cha jinsi ya kujijengea tabia za mafanikio. Kwa zaidi ya miezi sita sasa tumekuwa tukijadili jinsi ya kujijengea tabia ambazo zitatuwezesha kufikia mafanikio. Moja ya sababu kubwa kwa nini watu wengi hawafanikiwi licha ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa (more…)

NENO LA LEO; Jinsi Ya Kuua Hofu

By | December 2, 2014

If you hear a voice within you say “you cannot paint,” then by all means paint and that voice will be silenced. –Vincent Van Gogh Kama unasikia sauti ndani yako inayokuambia huwezi kuchora basi kwa njia yoyote ile hakikisha unachora na sauti hiyo itanyamazishwa. Usikubali kukatishwa tamaa na nafsi yako (more…)

SIKU YA UKIMWI DUNIANI; Mambo Kumi Unayotakiwa Kujua Kuhusu Ukimwi.

By | December 1, 2014

Kila tarehe 01/12 ya kila mwaka dunia inaadhimisha siku ya UKIMWI. Siku hii imepewa heshma yake kutokana na madhara yake makubwa kwa watu wanaoupata. Wakati tukiwa kwenye siku hii ya UKIMWI jiongeze na mambo haya kumi muhimu. 1. UKIMWI HAUUI. UKIMWI maana yake ni upungufu wa kinga mwilini. Hivyo kinga (more…)

Umuhimu wa taasisi za fedha kwenye maendeleo ya mjasiriamali.

By | December 1, 2014

Fedha ndio damu ya biashara au ujasiriamali wa aina yoyote. Baada ya kuwa na wazo zuri la kijasiriamali kinachofuata ni utekelezaji ambao unahitaji fedha. Na kwa kuwa fedha hazipatikani kirahisi inawalazimu wajasiriamali wengi kuanza kidogo na kuendelea kukua kadiri siku zinavyozidi kwenda. Leo tutajadili umuhimu wa taasisi za fedha kama (more…)