Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; FANYA MAJARIBIO MENGI ZAIDI…

By | June 7, 2018

“All life is an experiment. The more experiments you make, the better.” — Ralph Waldo Emerson Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA (more…)

UKURASA WA 1253; Kwa Nini Hatua Unazochukua Hazitakupa Mafanikio…

By | June 6, 2018

Watu wanasema kama kufanya kazi kwa nguvu na juhudi kungekuwa ni ufunguo wa mafanikio, basi punda wangekuwa na mafanikio makubwa sana. Ni kweli kwa asili, punda anabeba mizigo mizito sana na anaweza kustahimili mazingira magumu sana kama ya ukame. Lakini siyo mnyama mwenye mafanikio makubwa. Kwa upande wa pili, simba (more…)

UKURASA WA 1252; Matajiri Wa Kweli Hawafilisiki….

By | June 5, 2018

Kuna watu ambao huwa wanapata utajiri mkubwa, halafu wanafanya makosa fulani kwenye maisha yao, kisha wanapoteza kila kitu walichokuwa nacho, na kurudi sifuri kabisa. Kinachotokea baada ya kupoteza kila kitu ndiyo kinatuambia kama mtu alikuwa tajiri wa kweli au alikutana na utajiri kwa bahati. Tuanze na mfano, kuna mtu ambaye (more…)

#TAFAKARI YA LEO; NJIA SAHIHI YA KUFANYA KISICHO SAHIHI…

By | June 5, 2018

AMKA mwanamafanikio, Na siyo tu uamke kutoka kitandani, bali amka kutoka ndotoni, amka kutoka kwenye mawazo duni ya kifanya vitu kw mazoea, kufanya vitu kwa kawaida. Amka kutoka kwenye kujiandaa kuishi na amka uanze kuishi leo. Maana muda pekee ulionao ni huu, na unaweza kufanya chochote unachotaka na maisha yako, (more…)

UKURASA WA 1251; Njia Iliyo Ndefu Ni Njia Ya Mkato…

By | June 4, 2018

Unapoenda sehemu ambayo hujawahi kwenda, na kuna njia ambayo wengine wamepita wakafika huko, na wamekuonesha njia hiyo ni ipi, lakini wakati upo njiani, akatokea mtu na kukuambia njia hiyo unayopita ni ndefu, ipo njia ya mkato, pita hapa utafika kirahisi. Je utafuata njia ndefu ya uhakika au utafuata ya mkato? (more…)

UKURASA WA 1250; Kuna Maarifa Unayakosa…

By | June 3, 2018

Kama unajua kile unachotaka, na unaweka juhudi kubwa ili kuweza kukipata, lakini matokeo unayopata ni tofauti kabisa na matarajio, basi jua bila ya shaka yoyote kwamba kuna maarifa unakosa. Kuna kitu ambacho hukijui, ndiyo maana hupati kile ambacho unataka. Na wakati mwingine, kile unachojua kinaweza kuwa ndiyo kikwazo kwako kupata (more…)

#TAFAKARI YA LEO; SILAHA HATARI SANA DUNIANI…

By | June 3, 2018

“The most powerful weapon on earth is the human soul on fire.” —Marshal Ferdinand Foch AMKA mwanamafanikio, Siku nyingine, siku mpya na ya kipekee kwetu imeshaingia kwenye mikono yetu. Ni maamuzi yetu tunatumiaje muda tulionao kwenye siku hii bora na ya kipekee sana kwetu. Tunaweza kutumia muda huu kufanya makubwa (more…)

UKURASA WA 1249; Unajikadiria Vibaya…

By | June 2, 2018

Kitu kimoja ambacho sisi binadamu huwa tunakosea, ni pale tunapopata nafasi ya kujikadiria, huwa tunajikadiria vibaya, mara zote. Kama umewahi kupanga muda wa kumaliza kitu, au kupanga bajeti, umeshakutana na hili mara nyingi. Mara zote vitu huwa vinachukua muda mrefu kuliko tulivyokadiria, na pia vinachukua gharama kubwa kuliko tulivyokadiria. Upande (more…)