Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

#TAFAKARI YA LEO; USIKOSE CHA KUFANYA KILA WAKATI…

By | June 2, 2018

Without constant activity, the threats of life will soon overwhelm the values.” —Jim Rohn Mwanamafanikio, Leo tena tumeipata siku mpya, siku bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora kabisa. Nafasi tuliyoipata leo, haitajirudia tena kwenye maisha yetu, hivyo tunapaswa kuitumia vizuri ili kuweza (more…)

UKURASA WA 1248; Kuwa ‘Bize’ Na Kuzalisha…

By | June 1, 2018

Ni vitu viwili tofauti kabisa, visivyo na uhusiano wa karibu. Wengi hufikiri wakiwa bize, wakionekana wana mambo mengi basi ndiyo wanakuwa na uzalishaji mkubwa. Lakini uhalisia ni kwamba, kuwa bize ni kiashiria cha uzalishaji mdogo. Watu wanaokuwa bize mara nyingi huwa wanashindwa kupangilia vipaumbele vyao, na hilo linawafanya kuwa na (more…)

UKURASA WA 1247; Uhuru, Utu Na Utajiri…

By | May 31, 2018

Hivi ni vitu vitatu ambavyo kila mtu anavipigania, vitu vitatu ambavyo vinayafanya maisha ya yeyote kuwa bora sana. Kila mtu anapenda kuwa huru, kufanya maamuzi yake, kuendesha maisha yake, kufanya kile ambacho ni muhimu kwake. Lakini uhuru hauji bure, uhuru unahitaji kufanyiwa kazi na pia unakuja na majukumu. Wakati mwingine (more…)

#TAFAKARI YA LEO; USITEGEMEE CHOCHOTE, ILA WEKA JUHUDI…

By | May 31, 2018

“Expect nothing, and you will enjoy everything!” Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana. Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda (more…)

UKURASA WA 1246; Ukuaji Wowote Unahitaji Muda…

By | May 30, 2018

Kwa asili, ukuaji wowote unahitaji muda, tena muda wa kutosha na haraka haijawahi kusaidia. Tukianza na sisi wenyewe binadamu, mimba inatungwa, inakaa tumboni kwa miezi tisa, baada ya hapo anazaliwa mtoto, ambaye hawezi kujilisha wala hata kusema anataka kujisaidia, inamchukua miaka mitano kuweza kupata ufahamu wa kawaida wa kufanya mambo (more…)

UKURASA WA 1245; Hamasa Ya Kazi Inapoishia…

By | May 29, 2018

Siku ya kwanza ya kitu chochote, ni siku ambayo watu huwa wanakuwa na hamasa kubwa sana. Si unaikumbuka siku ya kwanza kwenda shule, huenda hukulala, ulisubiri kwa hamu kuamka na kwenda shule. Kadhalika siku ya kwanza kusafiri kwenda mahali ambapo hujawahi kwenda. Kumbuka pia siku yako ya kwanza ya biashara, (more…)

UKURASA WA 1244; Jinsi Ya Kuongea…

By | May 28, 2018

Nilishakushirikisha jinsi ya kusikiliza, leo nakwenda kukushirikisha jinsi ya kuongea. Unaweza kushangaa kwamba kuongea nako inapaswa kujifunza? Si unatoa tu maneno uliyonayo? Ni sababu hiyo ndiyo inapelekea wengi kuingia kwenye matatizo, kuongea kwa sababu tu wanaweza kuongea. Sasa tujifunze jinsi ya kuongea. Ongea kwa sababu una kitu MUHIMU cha kuongea, (more…)

UKURASA WA 1243; Ujumbe Uliopo Ndani Ya Kushindwa…

By | May 27, 2018

Huwezi kufanikiwa kwenye maisha bila ya kupitia kushindwa. Na tunaweza kusema kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni kushindwa. Kila anayejaribu kufanya chochote kwenye maisha, lazima akutane na kushindwa. Kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wasiofanikiwa ni kinachotokea baada ya kushindwa. Wasiofanikiwa, huacha baada ya kushindwa, huchukulia kushindwa kama kikwazo kikuu cha kufikia ndoto zao, (more…)