Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 855; Inayochukua Muda Ni Hatari Zaidi…

By | May 4, 2017

Mtu akiamka asubuhi, na ghafla akagundua anaharisha damu, atakimbilia hospitali mara moja. Kuharisha damu ni tatizo linaloonekana haraka. Lakini iwapo mtu huyu ataamka tu na tumbo likawa linauma na kuacha, hatakuwa na haraka, au kapata choo kimoja chenye rangi isiyoeleweka, ataendelea kusubiri. Inaweza kwenda hivyo kidogo kidogo, mpaka siku anakuja (more…)

Jinsi Ya Kuchagua Uwekezaji Unaokufaa Wewe Kulingana Na Mahitaji Yako.

By | May 3, 2017

Kila mtu ambaye yupo makini na fedha, anataka kufikia uhuru wa kifedha na utajiri, basi uwekezaji ni kitu cha lazima kufanya. Siyo kitu cha kujaribu na wala siyo kitu cha kuangalia kama unaweza, bali ni kitu ambacho unapaswa kujifunza, kukijua kiundani na kuwekeza. Hii ni kwa sababu kadiri umri wetu (more…)

UKURASA WA 854; Acha Kuzidisha Ugumu Wa Maisha Yako…

By | May 3, 2017

Maisha yenyewe ni magumu, lakini sisi wenyewe tumekuwa tunachagua kuyafanya kuwa magumu zaidi. Tunafanya hivi kwa namna tunavyochagua kuishi maisha yetu, na hata namna tunavyochukulia mambo yetu na mambo ya wengine. Kwa mfano kama mpo mnaimba kwaya, wote mnaimba kwa pamoja, utajuaje mtu ambaye haimbi vizuri? Au anakosea kuimba? Utajua (more…)

Tabia Moja Inayowaingiza Watu Wengi Kwenye Madeni Ya Kifedha, Na Namna Ya Kuiepuka.

By | May 2, 2017

Kijana mmoja ambaye alikuwa ndiyo ameajiriwa kama miaka miwili hivi, tukiwa kwenye maongezi aliniambia tangu ameajiriwa hajawahi kuchukua mkopo benki kwa kutumia mshahara wake. Nikamwambia hizo ni dalili nzuri, ni vyema akaendelea hivyo. Lakini yeye alikuwa akichukulia hilo kama siyo sawa, kwa sababu wenzake wote anaofanya nao kazi, wana mikopo (more…)

UKURASA WA 853; Njia Ya Kusikika Kwenye Kelele….

By | May 2, 2017

Kelele huwa zinaanzaje? Huwa hazianzi mara moja, kwamba kila mtu anajikuta anapiga kelele. Bali watu wanaanza kuongea kwa sauti ya chini, sasa wanapokuwa wengi wanaongea kwa sauti za chini chini, sauti zinaingiliana na hivyo hawasikilizani vizuri. Hii inapalekea kuanza kuongeza sauti kidogo kidogo ili wasikilizane vizuri. Kadiri wanafanya hivyo ndivyo (more…)

PESA NA BIASHARA; Misingi Mitatu Muhimu Ya Kuifuata Ili Kuwa Na Biashara Yenye Mafanikio.

By | May 1, 2017

Biashara ni sawa na kiumbe hai, na kama viumbe hai vyote vilivyo, huzaliwa na kufa, na ili kukua, basi kiumbe hai lazima kipate matunzo yote muhimu. Biashara inahitaji matunzo muhimu sana ili iweze kukua, na kama itapata matunzo yote muhimu kwa wakati, basi inaweza kuvunja sheria moja ya viumbe hai, (more…)

UKURASA WA 852; Kama Unataka Fedha….

By | May 1, 2017

Ndiyo kila mtu anataka fedha, Lakini je kila mtu yupo tayari kuweka juhudi ili kupata fedha hizo anazotaka? Au anasema anataka halafu anasubiri muujiza wa kuzileta fedha? Sasa nikukumbushe tu, japo najua unataka fedha, lakini nasema tena, kama unataka fedha, leta tofauti mahali. Angalia kile kinachokosekana kilete, angalia ambacho siyo (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MAISHA HAYATAKUWA RAHISI.

By | April 30, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Nafasi hii tuliyopata leo ni ya kipekee sana, twende tukaitumie vizuri ili tuweze kufanya makubwa kuelekea kwenye ndoto zetu. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku. Asubuhi ya leo tutafakari (more…)

UKURASA WA 851; Ni Matatizo Gani Unayotatua?

By | April 30, 2017

Swali muhimu mno kujiuliza kila wakati na kwa kila jambo unalofanya. Usifanye tu kwa sababu wengine wanafanya, wala usifanye ili uonekane na wewe unafanya. Swali la msingi ni tatizo au matatizo gani unayotatua? Ukianzia hapo, utaziona fursa nyingi sana, ambazo tayari zinakuzunguka ila tu wewe huzioni. Kama unamiliki biashara, je (more…)

💥 #TAFAKARI YA LEO; MWISHO WA TAFAKARI NA MONK MODE MORNING….

By | April 29, 2017

Hongera rafiki yangu kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo. Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa, ili kuweza kupata matokeo makubwa sana. Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA ambapo tutaweza kufanya makubwa sana leo na kila siku. Asubuhi ya leo hakutakuwa na tafakari, bali (more…)