Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Mambo Matano(5) Muhimu Ya Kujifunza Kwenye Kurasa 365 Za Mwaka 2015 Na Mazuri Yanayokuja 2016.

By | December 31, 2015

Habari za wakati huu rafiki yangu? Naamini uko vizuri sana na unaendelea vyema na mipango yako ya kuboresha maisha yako. Leo nimeandika ukurasa wa 365 katika kurasa 365 za mwaka 2015. Kuna mambo mengi nimejifunza kupitia kurasa hizi na nimeona ni vyema na wewe rafiki yangu ukayapata maana yatakusaidia sana. (more…)

UKURASA WA 365; Zaidi Na Bora.

By | December 31, 2015

Je ni nini ambacho unataka kwenye maisha yako? Unataka zaidi au unataka bora? Dunia na jamii zimekuwa zinatupeleka vibaya, zikituaminisha kwamba tunahitaji zaidi na zaidi na zaidi. Ubaya wa zaidi ni kwamba hauna mwisho, kadiri unavyopata ndivyo unavyohitaji zaidi. Lakini ili uwe na maisha unayoyafurahia na yenye mafanikio, huhitaji zaidi, (more…)

Malengo matano muhimu ya kibiashara ya kuweka kwa mwaka 2016.

By | December 30, 2015

Mwaka 2015 unakwisha na tunakwenda kuanza mwaka 2016. Je unaweza kusema kwa maneno machache mwaka 2015 ulikwendaje kwenye biashara yako? je unaweza kuangalia kwa mwaka wote 2015 na ukaona ukuaji uliotokea kwenye biashara yako? kwa sababu kama hakuna tofauti, basi ni vigumu sana kwa biashara yako kukua zaidi. Kila mwanzo (more…)

UKURASA WA 364; Ipe Dunia Uhuru…

By | December 30, 2015

Mara nyingi huwa tunaing’ang’ania dunia, huwa tunajishika nayo tukiamini ndio itatupa kile ambacho tunataka. Mara nyingi pia huwa tunafikiri tunaweza kuidhibiti dunia, kuifanya iende kama vile ambavyo sisi tunataka. Kutaka itupe kila ambacho tunataka. Lakini yote haya tunayofikiri hayawezekani, na kuendelea kuyafanya ni kuipa dunia nafasi kubwa ya kukuumiza wewe. (more…)

UKURASA WA 363; Dunia Nzuri Na Dunia Mbaya.

By | December 29, 2015

Wakati unasoma hapa kuna mambo mengi sana yanayoendelea duniani, zaidi ya mambo milioni. Na katika mambo hayo kuna ambayo ni mazuri na kuna ambayo ni mabaya. Kutokana na mambo hayo, wewe mwenyewe unaweza kuchagua kuiona dunia kuwa nzuri au kuwa mbaya. Kwa kufikiria zaidi yale mambo mabaya yanayotokea, utaiona dunia (more…)

UKURASA WA 362; Dunia Inakuhujumu, Na Hatua Za Wewe Kuchukua.

By | December 28, 2015

Ndiyo, dunia inakuhujumu. Na mambo mengi yanayofanyika hapa duniani, sio kwa faida yako, hasa ya muda mrefu. Fikiri kila unapopita kuna biashara nyingi sana, na zote zinakusisitiza wewe ununue. Wanatumia kila mbinu kukushawishi ununue, bila ya kujali kama unachonunua ni muhimu kwako au la. Simu uliyoibeba, nayo imejaa vitu vingi (more…)

UKURASA WA 361; Kusema Uongo Na Kutokutoa Taarifa Yote.

By | December 27, 2015

Kusema uongo na kutokutoa taarifa yote ni vitu viwili tofauti kabisa. Na japo ni muhimu sana kusema ukweli, haimaanishi ni lazima utoe taarifa yote. Kuna wakati unahitaji kutoa taarifa kiasi na sehemu nyingine ya taarifa ukaiacha. Hapa hudanganyi, bali unatoa ile taarifa inayomtosha mtu kwa wakati fulani na kuacha nyingine (more…)

UKURASA WA 360; Kanuni Rahisi Ya Furaha…

By | December 26, 2015

Dhumuni letu kubwa kwenye maisha ni furaha. Tunafanya kile tunachofanya kwa sababu tunajua kitatuwezesha kuwa na furaha zaidi. Hakuna mtu anayefanya kitu huku akijua ya kwamba kitamfanya asiwe na furaha. Tumeshajifunza mengi sana kuhusu furaha, na jambo la msingi kabisa ambalo unatakiwa kujua ni kwamba FURAHA INAANZIA NDANI YAKO MWENYEWE. (more…)

UKURASA WA 359; Ukweli Na Kubembeleza.

By | December 25, 2015

Maneno ya ukweli hayabembelezi… Na maneno yanayobembeleza sio ya kweli… Hivyo ni wajibu kwako kuchagua, unataka kutoa maneno ya kubembeleza au unataka kutoa maneno ya kweli? Ukitoa maneno ya kweli, watu hawatapendezwa, na wanaweza kukuchukia, ila ni kwa muda tu. Baadaye wataelewa, kwa sababu ukweli huwa haujifichi kwa muda mrefu. (more…)

UKURASA WA 358; Kwa Usalama Wako Binafsi Zingatia Hili…

By | December 24, 2015

Kwa usalama wako binafsi, zungukwa na watu wenye busara, watu ambao mnafikiri sawa, watu ambao mnakwenda mbali zaidi ya pale mlipo sasa. Na watu ambao wanaboresha kile wanachofanya na maisha yao kila siku. Kwa kuzungukwa na watu wa aina hii inakuwa ahueni kwako kuchukua hatua na kuendelea kuweka juhudi, hata (more…)