Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

UKURASA WA 357; Maumivu Na Mateso.

By | December 23, 2015

Maumivu hayakwepeki… Umepata hasara kwenye biashara… Nyumba yako imeungua…. Mtu wako wa karibu amefariki… Ulichotegemea hujakipata… Hii ni kwa sababu kuna mambo mengi ambayo hatuwezi kuyaathiri, na hivyo hatuwezi kukwepa maumivu. Yaani maumivu yapo na yanatujia mara kwa mara. Mateso ni kuchagua, tofauti na maamuzi, wewe ndio unaamua uteseke au (more…)

UKURASA WA 356; Kujali Kunakoumiza…

By | December 22, 2015

Moja ya vitu vinavyotufanya tunaendelea kuwepo duniani kama binadamu ni kujali. Ndio tunajali sana kuhusu sisi wenyewe na hata wale wanaotuzunguka. Tunapenda kuona tupo kwenye hali salama na hata wale wa karibu yetu pia tunapenda kuona wapo salama. Lakini kujali huku pia kunakuja na hasara zake, kuna kujali ambapo kunakuumiza (more…)

UKURASA WA 355; Kazi Iliyo Ngumu Sana, Lakini Muhimu Kufanya.

By | December 21, 2015

Kwa asili yetu binadamu hatupendi kufanya vitu vigumu. Na kama inatubidi kufanya basi huwa tunatafuta njia ya kurahisisha kufanya kitu hiko. Hii ndio imeleta mapinduzi makubwa sana kwenye teknolojia ukianza na zama za mawe, zama za chuma, mapinduzi ya viwanda na mpaka sasa zama za taarifa. Kwa kuwa vitu vingi (more…)

UKURASA WA 354; Hatari Moja Ambayo Huwezi Kuikwepa….

By | December 20, 2015

Kuishi ni hatari, ndio kila siku tunakutana na hatari mbalimbali, lakini hatuachi kuishi. Katika maisha tunakutana na hatari mbali mbali, kuna ambazo tunaweza kuziepuka na kuna ambazo hatuwezi kuziepuka. Kuna hatari moja ambayo wengi wetu huwa tunafikiri tunaweza kuiepuka au kuikwepa na hivyo kukazana kuikwepa, na mwishowe tunajikuta tunahangaika na (more…)

UKURASA WA 353; Kipimo Sahihi Cha Mafanikio Yako….

By | December 19, 2015

Pamoja na changamoto nyingi zinazotuzuia kufikia mafanikio, kipimo nacho kimekuwa ni changamoto kubwa. Kipimo unachotumia kwenye kupima mafanikio yako, kinaweza kukusukuma zaidi au kinaweza kukukatisha tamaa. Aina za vipimo vya mafanikio. Kuna aina mbili za vipimo vya mafanikio, moja inakusukuma kwenda mbele na nyingine inakukatisha tamaa. Aina ya kwanza ni (more…)

UKURASA WA 351; Majuto Kama Kichocheo….

By | December 17, 2015

Kila mmoja wetu kuna kitu fulani alishajutia, yaani ulishafanya kitu fulani na baadaye ukagundua ya kwamba ulikosea. Kila mmoja wetu. Lakini majuto haya hayafanani kwa kila mmoja wetu, hasa jinsi ambavyo tunayatumia kwa baadae. Kama ningejua, ningechukua ile fursa mapema…. Kama ningejua nisingeingia kwenye hii kazi au biashara…. Kama ningejua (more…)

Njia tano za kukuza biashara yako kwenye msimu huu wa sikukuu.

By | December 16, 2015

Kila mwisho wa mwaka na mwanzo wa mwaka ni kipindi ambacho watu wengi wanakuwa na mapumziko. Ni wakati ambao watu wengi wanakuwa na sikukuu na pia wengi hufanya sherehe zao katika kipindi hiki. Kutokana na hali hii ya mapumziko na sikukuu, watu wengi huwa kwenye hali ya kufanya manunuzi mengi. (more…)

UKURASA WA 350; Mgogoro Wako Na Nafsi Yako…

By | December 16, 2015

Kila mmoja wetu anapitia hali hii katika kipindi fulani kwenye maisha yake, wapo wanaopata mgogoro huu kwa muda mfupi, wapo wanaoishi na mgogoro huu maisha yao yote. Huu ni mgogoro kati yako wewe na nafsi yako. Huu ni mgogoro mkubwa sana, ambao unaleta hasira kubwa kwako. Hivyo mapema utakapousuluhisha, ndivyo (more…)

UKURASA WA 349; Aina Mbili Za Maamuzi…

By | December 15, 2015

Maamuzi yoyote tunayofanya kwenye maisha yetu, yamegawanyika katika aina mbili. Aina ya kwanza ni maamuzi tunayofanya kwa kusukumwa na hofu, unafanya maamuzi kwa sababu unahofia kitu fulani kitatokea au hakitatokea. Aina ya pili ni maamuzi tunayofanya kwa kusukumwa na mapenzi au ukuaji, hapa unafanya maamuzi kwa sababu unataka kukua zaidi. (more…)