Author Archives: Dr. Makirita Amani

About Dr. Makirita Amani

Dr. Makirita Amani ni daktari wa binadamu, mwandishi, mhamasishaji na mjasiriamali. Dhumuni lake kubwa kwenye maisha ni KUWASAIDA WATU KUBORESHA MAISHA YAO NA KUFIKIA MAFANIKIO MAKUBWA KUPITIA KAZI ANAZOFANYA. Mawasiliano 0717396253 email makirita@kisimachamaarifa.co.tz

Mabadiliko Kwenye Blog Zinazoendeshwa Na AMKA CONSULTANTS.

By | June 5, 2015

Habari za leo mpenzi msomaji wa blog za AMKA CONSULTANTS, naamini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. AMKA CONSULTANTS ipo pamoja na wewe kwenye safari hii ya kuboresha maisha yako na inakupatia maarifa na ushauri muhimu utakaokusaidia kwenye safari hii. Kwa kuwa lengo (more…)

BIASHARA LEO; Biashara Inayolipa Kuliko Hiyo Unayofanya Sasa.

By | June 4, 2015

Katika wakati wowote kwenye maisha yako ya kibiashara, kuna biashara ambayo itakuwa inalipa kuliko biashara unayofanya wewe. Katika hali hii unaweza kushawishika kwamba biashara uliyopo wewe sio nzuri na kutamani kuwepo kwenye biashara ile ambayo inalipa. Na kuna baadhi ya watu huamua hata kufanya maamuzi ya kubadili biashara na kuhamia (more…)

UKURASA WA 155; Hii Ndio Sababu Kubwa Inayokufanya Ushindwe Kutatua Matatizo Yako.

By | June 4, 2015

Tumewahi kujadili hapa kwamba matatizo uliyonayo umeyatengeneza wewe mwenyewe. Hii inatokea kwa sababu kwa kila tatizo ulilonalo, unapojaribu kulitatua unatengeneza tatizo jingine. Kila suluhisho linakuja na tatizo jipya kabisa. Hivyo unaweza kuchagua ni matatizo ya aina gani unafanya. Kuna wakati mtu anaweza kuwa kwenye matatizo makubwa sana na akawa hajui (more…)

BIASHARA LEO; Sababu Moja Kwa Nini Biashara Yako Haina Soko.

By | June 3, 2015

Kama biashara haina soko kuna jambo moja tuna uhakika nalo, itakufa. Hakuna biashara ambayo itaweza kujiendesha bila ya kuwa na wateja. Mafanikio yako wewe kama mfanyabiashara ni kiasi gani cha soko umeshika. Kuna biashara nyingi sana ambazo zinakufa kwa kukosa soko. Leo nataka nikupe sababu moja kwa nini biashara yako (more…)

UKURASA WA 154; Jinsi Ya Kuwinda Fedha Zako Mwenyewe Ili Kufikia Uhuru Wa Kifedha.

By | June 3, 2015

Kwenye makala ya siku mbili zilizopita tuliona kwamba kila mtu anawinda fedha zako wewe. Kila mtu anayejaribu kukushawishi ununue kitu, kila anayekushawishi utoe fedha yako anaiwinda fedha yako. Kuna watu wengi sana wanaokuzunguka ambao wanawinda fedha yako, hivyo usipokuwa makini utashangaa umefanya kazi miaka mingi ila huoni kikubwa ulichobadili kwenye (more…)

BIASHARA LEO; Kabla Hujaanza Biashara Yoyote Mpya, Zingatia Jambo Hili Moja Muhimu Sana.

By | June 2, 2015

Biashara mpya zina kasi kubwa sana ya kushindwa. Hapa kwetu Tanzania hatuna tafiti za kutosha ila kwa nchi zilizoendelea na zilizofanya tafiti, biashara 8 kati ya 10 zinazoanzishwa hufa mwaka mmoja baada ya kuanzishwa. Hii ni hatari sana na kwa uzoefu tu hapa kwetu hali inaweza kuwa mbaya zaidi. Kuna (more…)

UKURASA WA 153; Huyu Ndio Pekee Anayefanana Na Wewe Kwa Kila Kitu.

By | June 2, 2015

Katika dunia hii ambayo ina watu zaidi ya bilioni saba, kuna mtu mmoja tu ambaye anafanana na wewe kwa kila kitu. Hii ni kuanzia uwezo, ubunifu, vipaji na hata mipango mbalimbali ya kimaisha. Kwa kumjua mtu huyu na kushirikiana naye vizuri kutakuwezesha wewe kufikia mafanikio makubwa sana. Utafikia mafanikio makubwa (more…)