1458; Thamani Ya Kitu Ukiwa Nacho Na Ukikipoteza…

By | December 28, 2018

Kuna vitu vingi sana huwa tunavyo, tunakuwa tumevizoea na kuvichukulia kawaida sana, kwa sababu tumeshakuwa navyo kwa muda na tunajua tutaendelea kuwa navyo. Kwa kuzoea kwetu  vitu hivyo, huwa tunaona havina thamani kubwa sana kwetu, na tunaweza kuviacha hovyo hovyo na kusahau kabisa kwamba mwanzoni tuliteseka sana kuvipata. Pale inapotokea (more…)

1457; Unachopaswa Kufanya Kwa Wakati Ulionao…

By | December 27, 2018

Ni kile ambacho umepanga kufanya, kile ambacho ni muhimu zaidi kwa wakati huo. Unapaswa kuweka akili yako yote na nguvu zako zote kwenye kitu kimoja ambacho umechagua kufanya. Kugawa akili yako na nguvu zako kwenye mambo mengi kwa wakati mmoja ni kupunguza ufanisi wake. Chukua mfano wa jua, jua likitawanywa (more…)

1454; Kuacha Kila Kitu Kwa Sababu Ya Kitu Kimoja…

By | December 24, 2018

Hakuna kitu kimoja pekee ambacho kitakupa wewe kila unachotaka, hakipo. Lakini wengi huwa tunaweka matumaini makubwa sana kwenye kitu fulani ambacho tunakuwa tunakitegemea. Labda kuna kitu tunataka kufanya, ambacho tunaona ni kikubwa na kitakuwa na matokeo bora sana. Basi mawazo yetu yote yanakuwa kwenye kitu hicho na kusahau kabisa vitu (more…)

1453; Kupata Usichotaka Siyo Sawa Na Kukosa Kabisa…

By | December 23, 2018

Watu wengi huwa hawapendi pale wanapopata wasichotaka, huwa wanaona kama wamepoteza muda wao na juhudi walizoweka kwenye kile walichofanya. Lakini hilo siyo sahihi, kupata usichotaka siyo kupoteza muda wala nguvu, bali ni kujisogeza karibu zaidi na kile unachotaka. Kupata usichotaka siyo sawa na kukosa kabisa. Kwa sababu kwa kupata usichotaka (more…)

1452; Acha Kujipa Sababu Za Kwa Nini Ni Sahihi…

By | December 22, 2018

Rafiki, Umewahi kugundua kwamba mara nyingi huwa unajipa kila aina ya sababu kwa nini kile ulichonacho au unachofanya ndiyo sahihi? Labda ni kazi au biashara fulani unafanya na unajiambia hiyo ndiyo sahihi kufanya. Halafu baadaye unaondoka kwenye kazi au biashara hiyo na kwenda kwenye nyingine, unajipa tena sababu kwa nini (more…)

1451; Pesa Ipo Kwenye Matatizo Magumu…

By | December 21, 2018

Kila unapotaka kupata fedha zaidi, nakushauri uangalie sehemu moja, matatizo magumu ambayo yanawasumbua wengi kisha yatatue hayo. Fedha ipo kwenye matatizo magumu na yanayowasumbua wengi. Kwa sababu ni magumu, hakuna wengi wanaohangaika nayo, na hivyo unapoyatatua, unajiwekea upekee ambao unapatikana kwako tu. Usikimbizane na vitu rahisi, vitu ambavyo kila mtu (more…)

1450; Tatizo Siyo Kupata Wazo Jipya, Bali Kusahau Wazo La Zamani…

By | December 20, 2018

Kupata wazo jipya siyo kazi, mawazo mapya yapo mengi mno. Hakuna aliyeshindwa kwenye maisha kwa sababu hakupata wazo jipya na zuri. Watu wengi wanashindwa kwenye maisha kwa sababu wanashindwa kusahau wazo la zamani, wanashindwa kuachana na wazo walilokuwa wanafanyia kazi siku za nyuma. Huwa tunapenda sana vitu vyetu, na tunaendelea (more…)