UKURASA WA 454; Chakula Cha Mawazo Hasi.

By | March 29, 2016

Ni sheria ya asili kwamba chochote kinacholishwa kinakua, na chochote kinachokosa chakula kinadhoofu na kufa. Wote tumewahi kuona watoto wadogo, kadiri anavyopata chakula kizuri, yaani mlo kamili anakua vizuri na kuwa na afya bora. Lakini anapokosa chakula kizuri afya yake inakuwa dhoofu na anaweza kufariki. Sasa mawazo hasi nayo huwa (more…)

Kitu muhimu kwa mteja wako kuliko fedha anayokupa.

By | March 28, 2016

Mara nyingi wafanyabiashara tumekuwa tukijiuliza iwapo bidhaa au huduma tunayomuuzia mteja wetu inaendana na thamani ya fedha anayotoa. Kwa njia hii tumekuwa tunachukulia fedha ya mteja kama ndiyo kitu muhimu sana kwao, na hivyo kuhakikisha hawapotezi fedha zao kwa kufanya biashara na sisi. Ni kweli kabisa fedha ya mteja ni (more…)

UKURASA WA 453; Baada Ya Kupanda Mlima….

By | March 28, 2016

Katika kurasa zilizopita, tuliona ya kwamba hakuna mtu anaweza kuibukia kileleni. Badala yake unahitaji kupanda hatua moja baada ya nyingine ndipo ufike kileleni. Na pia tuliona safari hiyo siyo rahisi, ndiyo maana wengi huwa wanaishia njiani. Unaweza kuisoma hapa; UKURASA WA 451; Kuibukia Kileleni… Sasa kuna kitu kimoja ambacho hatukukiangalia (more…)

FALSAFA MPYA YA MAISHA; Kinachotuzuia Kuishi Maisha Ya Furaha.

By | March 27, 2016

Habari za leo mwanafalsafa mwenzangu? Ni imani yangu kwamba maisha yako yanazidi kuwa bora kadiri unavyojifunza kupitia falsafa hii mpya ya maisha na kufanyia kazi yale ambayo unajifunza. Kama ambavyo wote tunajua, dhumuni kuu la maisha yetu, kinachotusukuma tufanye kile ambacho tunafanya ni furaha. Kila mtu anapenda kuwa na maisha (more…)

UKURASA WA 452; Baadaye…

By | March 27, 2016

Baadaye ni njia rahisi ya kujitoa kwenye mvutano mkali unaokuwa nao sasa. Kwenye mvutano kwamba nifanye au nisifanye, njia rahisi ya kujitoa hapo ni kusema nitafanya baadaye. Lakini baadaye ni mara chache sana inatokea tukafanya tulichotaka kufanya, au tukaleta mabadiliko ambayo tunataka kuleta. Baadaye tunayosema huwa haifiki na hata ikifike (more…)

UKURASA WA 451; Kuibukia Kileleni…

By | March 26, 2016

Mtu yeyote ambaye amewahi kupanda mlima mrefu, Kilimanjaro au mwingine wowote, atakuambia kitu kimoja muhimu, hakujikuta kileleni. Badala yake alianza kupiga hatua moja baada ya nyingine, na kidogo kidogo akapanda mpaka kufikia kileleni. Huu ndio ukweli wa maisha, huwezi kuibukia kileleni, yaani ukajikuta tayari upo kileleni, hakujawahi kutokea muujiza wa (more…)

BIASHARA LEO; Viashiria Kwamba Umeshaingia Kwenye Ushindani Utakaokupoteza Kibiashara.

By | March 25, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nasisitiza mara nyingi, ushindani wa moja kwa moja kwenye biashara, ndiyo mchezo mbaya kuliko yote unaoweza kufanya kwenye biashara yako, kwa sababu utakupoteza haraka sana. Mfanyabiashara mwenzetu aliandika maoni kutaka kujua ni viashiria gani mfanyabiashara anaweza kuwa navyo pale anapokuwa ameingia kwenye mashindano ya kibiashara.Aliandika maoni yake (more…)

Karibu Kwenye Kundi Jipya La AMKA MTANZANIA, Hakuna Gharama Na Nafasi Ni Chache.

By | March 25, 2016

Habari za wakati huu rafiki yangu? Nina imani kubwa kwamba wewe rafiki yangu unaendelea kuweka juhudi ili kufanya maisha yako kuwa bora zaidi. Maana hiyo ndiyo njia pekee ya kuwa na maisha bora, siyo kusubiri, siyo kulalamika, siyo kulaumu, bali ni kufanya, kuweka juhudi, na matokeo utayaona. Leo napenda kuchukua (more…)

UKURASA WA 450; Sababu Mbili Za Kuweka Juhudi.

By | March 25, 2016

Mpaka sasa nina hakika unajua hili, ya kwamba ili kuweza kufikia mafanikio makubwa, unahitaji kuweka juhudi kubwa sana, yaani sana. Kama wenzako wanafanya kwa kawaida, wewe unahitaji kwenda mbali zaidi. Na kama mpaka sasa hukubaliani na hilo, usiendelee kusoma. Sasa kuna sababu mbili za kuweka juhudi kubwa sana. Sababu ya (more…)

UKURASA WA 449; Makosa Ya Wengine.

By | March 24, 2016

Makosa ya wengine ni kitu cha kipekee sana kwetu, Makosa ya wengine yanaonekana haraka sana, kuliko hata makosa yetu. Makosa ya wengine yanatupa vitu vya kujadili na kukosoa. Makosa ya wengine yanatupa ahueni kwamba angalau sisi tuko vizuri, kuliko hao wenye makosa hayo. Makosa ya wengine tunaweza kuamua kuyatumia tutakavyo, (more…)