UKURASA WA 630; Hatua Za Kuchukua Kama Huwezi Kudhibiti Hasira Zako…

By | September 21, 2016

Moja ya vitu unahitaji ili kuwa na maisha ya mafanikio, ni kuweza kudhibiti hisia zako, hasa kudhibiti hisia za hasira. Hisia za hasira zina nguvu kubwa na zinaweza kuharibu misingi yote ambayo umeshaijenga kwa ajili ya mafanikio. Wakati unafanyia kazi kudhibiti hasira zako, kama bado hujaweza kuzidhibiti, kuna mambo mawili (more…)

UKURASA WA 629; Muda Unaosubiri Ni Muda Unaopoteza…

By | September 20, 2016

Kila mtu kuna kitu ambacho anataka au kupenda sana kufanya, lakini hajaanza kufanya mpaka sasa. Kikubwa ambacho kinawazuia watu kuchukua hatua ni kusubiri kwa kufikiri kwamba wakati wa kufanya bado. Wengi wamekuwa wakifikiri kwamba bado hawajawa tayari, au bado mazingira hayajawa mazuri kwa wao kuanza. Lakini rafiki yangu, mwana mafanikio (more…)

UKURASA WA 628; Jinsi Ya Kuwafundisha Watoto Wako Thamani Ya Fedha….

By | September 19, 2016

Huwezi kuijua thamani ya fedha mpaka pale umeifanyia fedha hiyo kazi, umeumia na kusumbuka kisha ukaipata fedha. Hapo ndipo utaona thamani yake na kuiheshimu fedha hiyo. Hivi ndivyo hali ilivyo kwetu wanadamu, tunathamini kile ambacho tunajua hatukipati kwa urahisi. Na ndiyo maana wale wanaopata fedha kwa urahisi huwa wanazitumia hovyo (more…)

UKURASA WA 627; Haraka Ya Zama Hizi Itakupoteza…

By | September 18, 2016

Tunaishi kwenye zama za tofauti kabisa ukilinganisha na zama zilizopita. Kwa sasa kila kitu ni haraka. Tunataka vitu haraka na tunavitaka sasa, subira imekuwa kitu adimu mno. Kasi ndiyo kipimo cha ubora kwa sasa, tunataka kusafiri kwa kasi, tunataka mtandao uwe na kasi kubwa, kusubiri dakika chache ni mtihani mgumu (more…)

UKURASA WA 626; Kuwapa Watu Kile Wanachotaka, Ni Hatari Kwa Mafanikio Yako…

By | September 17, 2016

Ukiangalia watu na makampuni yaliyoleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yetu na kuwa na mafanikio makubwa, walifanya kile ambacho wengi hawawezi kufanya. Badala ya kuwapa watu kile ambacho walikuwa wanataka, waliwapa watu kile ambacho ni bora zaidi. Kwa mfano, kabla ya kuja kwa magari usafiri mrefu ulifanyika kwa njia ya treni (more…)

UKURASA WA 625; Jinsi Ya Kujijengea Na Kuilinda Sifa Yako.

By | September 16, 2016

Sifa yako ni vile ambavyo watu wengine wanakuchukulia wewe. Hii inatokana na vile unavyofanya mambo yako na unavyowafanyia wengine. Maneno pekee hayakujengei sifa, bali matendo yako. Watu wanaamua wakuchukulieje kulingana na unavyoathiri na kugusa maisha yao. Siyo wewe unayeamua watu wakuchukulieje, bali ni wao wenyewe. Japo huna nguvu ya kuwaambia (more…)

UKURASA WA 624; Hatua Iliyo Ngumu Zaidi Kwenye Safari Ya Mafanikio…

By | September 15, 2016

Kila hatua kwenye safari ya mafanikio ni ngumu, na ndiyo maana wengi safari hii inawashinda, hata kuanza tu ni changamoto kwa wengi. Lakini kuna hatua ambayo ni ngumu zaidi ukilinganisha na hatua nyingine. Leo tunakwenda kuangalia hatua hii iliyo ngumu, na jinsi tunavyoweza kufanya kuwa rahisi kwetu. Kabla hatujaiangalia hatua (more…)

UKURASA WA 623; Tofauti Ya Darasani Na Duniani.

By | September 14, 2016

Kama duniani kungekuwa kama darasani, basi kila mtu angekuwa na yale maisha anayotaka kuwa nayo. Ila kuna tofauti kubwa sana kati ya darasani na duniani, wengi hawaelewi tofauti hii na ndiyo maana wamekuwa wanafanya mambo ya ajabu. Kama hujaelewa, darasani namaanisha mfumo wote wa elimu, kuanzia chekecheka mpaka chuo kikuu, (more…)

UKURASA WA 622; Rahisi Kufanya, Rahisi Kutokufanya.

By | September 13, 2016

Kama ambavyo nimekuwa nasema na kusisitiza mara kwa mara, ili tufanikiwe, tunahitaji kwenda tofauti na baadhi ya mambo yetu ya asili ambayo yanatufanya tuwe na maisha fulani. Akili zetu, saikolojia yetu na hata miili yetu, ina mazoea fulani ambayo yamekuwa kikwazo kwetu kupiga hatua. Kwa mfano, vitu ambavyo ni rahisi (more…)

UKURASA WA 621; Furahia Vikwazo Unavyokutana Navyo…

By | September 12, 2016

Unaweza usielewe lakini unatakiwa kufurahia vikwazo unavyokutana navyo kwenye safari yako ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa. Iwe ni kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Kwa nini? Kwa sababu vikwazo hivyo ndiyo vinawazuia wengi kufanikiwa. Vikwazo hivyo ndiyo vinawafanya wengi kukata tamaa na kushindwa kuchukua hatua. Vikwazo hivi ndiyo (more…)